Maswali magumu juu ya ujio wa Lowassa UKAWA

Mr EWA

JF-Expert Member
Mar 15, 2007
332
225
Wadau heshima kwenu,

Nitangulize kwa kusema kuwa mimi ni mdau wa ukawa na namini kuwa kwa tafiti zote zilizofanyika kabla ya uchaguzi huu kwa maana ya namba zinadhihirisha kuwa kwa ujio wa Mhe. Lowassa ushindi kwa ukawa si jambo la kuwa na mashaka kutokana na namba zilizowahi kutolewa.

Maswali magumu ya kujiuliza si kwa maana ya kugawa au kukatisha watu tamaa na kuna falsafa inasema tunapaswa kujiandaa na yatakayokuja hata kama hatuyapendi.

•Je, Ikibainika kuwa ujio wa Lowassa Ukawa ni mpango wa kiufundi uliopangwa na CCM ilikuhakikisha kuwa ikishinda CCM au UKAWA ushindi unabakia kuwa wao kwa maana ya dola.

•Je, Ikitokea ushindi ukapatikana kwa upande wa ukawa na uongozi wa juu kwa maana ya Rais ukashindwa kutekeleza kwa vitendo falsafa ya upinzani au ukawa, Nini kifanyike ili kutii kiu ya wananchi wengi kutaka mabadiliko?

Maoni yangu juu ya mashaka haya ambayo kimsingi si ya kubeza kutokana na matumaini makubwa ya mabadiliko waliyonayo watanzania.

1.Team yote ya ukawa inahitajika kuwa makini kuliko kipindi kingine chochote kwa maana ya kujiridhisha kwanza na maamuzi yeyote kabla ya kufikia hitimisho la maamuzi ya aina yeyote.

2.Team ya ukawa kupanga mipango mikakati ya kiutekelezaji na udhibiti wa taasisi ya urais baada ya ushindi kutokana na nature ya muungano wa ukawa ulivyo kwani Rais anaweza tumia nguvu zake kufanya mambo ayatakayo yeye mwenyewe ambayo yanaweza kuwa na mtizamo tofauti na matarajio ya wadau wa mabadiliko.

3.Kama ushindi utakuwa upande wa ukawa basi ni jambo jema kuwa au kukubaliana utaratibu utakao tumika katika kujaza nafasi za uteuzi ili kudhibiti zoezi hilo lisije kuwa na taswira ambayo inaonekana kwa sasa kwani matamanio yetu ni kuwa na mfumo bora na Imara katika kuendesha Taifa na unaotanguliza masilahi mapana ya Taifa.

Mtizamo wangu juu ya Mhe. Lowassa:

•Lowassa anaonekana ni mtu mwenye kiu kubwa ya kuwatumikia watanzania na kuwaletea maendeleo ya kweli napengine ndoto zake zimekuwa zikizimwa mara kwa mara.

•Lowassa anaonekana ni mtu ambaye amebezwa sana na baadhi ya wanachama wa chama chake cha zamani kuwa hawezi au hana sifa za kuwa kiongozi mkuu wa taifa na hasa kusemekana na baadhi ya watu kuwa Rais hawezi kutoka kazikazini, Mambo hayo yanaonyesha kumsononesha na huenda ndio imempelekea kufanya maamuzi magumu ya kujiunga na ukawa ili atmize ndoto zake na kuuhakikishia umma kuwa Rais anaweza toka upande wowote wa taifa letu.

•Ombi langu kwa Lowassa wakati ikitimiza ndoto zake za kuwa Rais akumbuke kuwa wanamabadiliko pia wako na ndoto zao za muda mrefu ambazo wanaimani zitatekelezwa na upinzani au ukawa na wanatamani ndoto hizo ziweze kufikiwa, akumbuke kuwa kutokufikia malengo makubwa ya ndoto za wadau wa mabadiliko kufaidi matunda au raslimali za taifa utakuwa umeturudisha nyuma hatua nyingi sana ambazo hatukuwa na sababu ya kurudi nyuma kwani mbele ni karibu zaidi kufikia matarajio yetu ya kuwa na taifa lenye uchumi bora na imara.

Karibuni kwa kuchangia kwa maana ya kujenga.
 
1st AID

JF-Expert Member
Jul 29, 2014
1,080
1,225
Salaam

Kunavitu navyoendelea kuvifikiria labda kwa sasabu sina taarifa sahihi au kwa sababu naamini siasa nimchezo unaofanywa na kundi la watu wachache kutumia watu wengi kufanikisha malengo yao binafsi kwa njia ya kura..

Nikiangalia hili linaloendelea ndani ya UKAWA nahisi kuna wanaoelewa kinacho endelea na wanakiendeleza na wapo wanao buruzwa na hawana namna ya kujikwamua kutokana na kutokuwa na matumaini zaidi tofauti na walichonacho vichwani mwao na kuna ambao hawaelewi chochote nawapo tu kwa sababu wapo, yaani mashabiki na hawa ndio wanaotumika kufanikisha malengo ya wachache.

Nikiwa kama raia mwingine yeyote ambaye najaribu kuangalia mstakabali wa nchi yangu nafika mahali nahisi kuvurugikwa akili. Labda niweke wazi kwamba binafsi si mfuasi wa itikadi ya chama chochote kwa hiyo naangalia kila mtangaza nia ya uongozi kwa tiketi ya chama Fulani kwa ukaribu ili niweze kuamua kura yangu niipeleke kwa yupi kutokana na imani yangu kwake bila kujali chama,anacho pitia... vigezo vya imani yangu ni vingi japo muhimu ni utendaji, uaminifu,dhamira na uwezo wa mtu binafsi.

Lakini kila kukicha kunatokea kioja kipya hasa upande huu wa UKAWA inakuwa kama kila kitu kimewatokea kwa kushitukizwa na hakuna aliyejipanga kukipokea. Mwanzo waliniaminisha kuwa wanamisingi thabiti na dhamira ya kweli ya kuleta mageuzi ya kimfumo. Nilivutiwa nafikra hizo pevu kwa kiasi nilianza kuwaamini, ingawa nilitatizika na kusita kwao kumtangaza mgombea wa nafasi ya urais mpaka baada ya CCM kuwa wamepata mgombeawao. Au walichelewa ili kuangalia upepo wa atakae simamishwa na Sisiem ili wapangemashambulizi dhidi yake.

Ingawa kwa kiasi niliwaelewa UKAWA kwa ucheleweshaji wao …nilihisi kulikuwa na majadiliano yakimaslahi ikiwa ni pamoja na faida zipi zitapatika kwa kila mmoja kutokana na muungano huo, ambao nao ulianza katika mazingira tatanishi, hakukuwa na makubaliano yakiamandishi MOU kabla ya wote kugomea uchakachuaji wa mapendekezo ya katiba yaliyowakilishwa na Jaji Warioba. Anae fahamu kama kulikuwa na makubaliano hayo anisaidie au atusaidie maana tupo wengi tunao tatizika.

Naendelea kufikiria nje ya boksi je UKAWA iliendelea kuwepo kwa nguvu ya nani? Je ni wao kama wao viongozi wa vyama pinzani au kulikuwa na extra invisible godfather ambae alikusudia kuifanya UKAWA ni mpango "B" baada ya kuona muungano huo utakuwa rahisi kuwakamata wote kwa urahisi kama kutatokea haja ya kuwavuruga au kunufaika?.

Kwa msingi huu wa UKAWA ambao muungano wao nao amini ulitokea ghafla pale Dodoma ninamashaka kama kutakuwa na uimara katika muungano huu ambao ni kama umeshikiliwa na hali ya kisiasa iliyopo bila kuwa na mipango thabiti ya umoja huo toka awali au kabla ya kuundwa kwake.

Naendelea kujiuliza vipi ikiwa kuingia kwa EL ..CDM ni plan ya CCMM katika kuua kabisa upinzani nikiwana maana kuwavuruga kwa sababu naamini kuna wasio kubaliana na ujio wake nawamekaa kimya wanafahamika …. Maana kulikuwa na vikao vya majadiliano si chini ya kumi na 13 kwa nilivyo sikia. Maana yake kunahofu na kutoaminiana. Ikiwa kweli EL ameamua kutimiza ndoto yake kwa kuwatumia CDM itakuwaje baada ya kuingia magogoni na akawageuka! ikumbukwe anajiamini kwa ukwasi na karsima ya wengi kuliko kutegemea chama!Mwenye fikra na uelewa zaidi anisaidie na atakuwa ametusaidia sisi tusiofahamu sana uhalisia.Ni mtazamo wangu tu.
 
ajobwe

Member
May 5, 2015
11
0
Lowasa ameenda kuchunguza hua wanatoa wapi siri hadi kufikia kumchafua asipate urais
 
GreenCity

JF-Expert Member
May 28, 2012
5,613
2,000
Umeandika vema sana mkuu! Kizuri zaidi na majibu umewawekea, bila shaka mada hii sio nzuri sana kwa CCM!
 
H.T.P

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,169
2,000
Hujaandika vizuri hata kidogo acha janja ya nyani mnafiki wewe...watu humu wanaakili sana na zaidi sisi wana CDM huwezi kitu black mail...Lowasa hajaja CDM kuchunguza amekuja kuleta mabadiliko na ukombozi wa nchi yetu kutoka katika utumwa wa farao CCM...tafakari Mr Ewa
 
Jun 18, 2013
47
95
hayana maana sasa hivi vijiswali waulize. CCM kwanini yanawakuta yanayowakuta

Bora sasa kuliko baadae maana usifikirie kumuuondoa ccm fikiria nini kitakuja baada ya kumuondoa ccm kumbuka ukawa sio chama na haiwezi kushika madaraka so automatically chadema ndo mwenye dola je cuf watasemaje?
 
Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,414
2,000
Lowasaa akishinda ndo mwisho wa CDM kwani naamini ataingiza mambo yake ambayo kimsingi hayashabihiani na CDM original, atafanya hivyo kwasababu kwanza yeye anaonekana ndo kaombwa na CDM ili awasaidie na kwasababu hata akishinda si kwasababu ya CDM, Lowassa hategemei chama ili kushinda kwasababu yeye anaamini ana watu wake tayari na ana pesa tofauti na magufuri anayesubiri kukampeniwa na chama ..sasa mtu ambaye hategemei chama ili ashinde akishinda chama kitawezaje kumcontrol ? atatii? kwa magufuri kwasababu anasaidiwa na chama chake anaamini chama vhake kitaendelea kuwa nguzo yake lakini kwa Lowassa atakuwa kama yeye na hata kama itahitajika kuwa na chama yeye ndo atakuwa juu ya chama either kwa direct ama indirect na kwa chochote atakachokifanya itabidi wote wakubali vinginevyo utaambiwa utoke ..hiki kitakuwa ni chama cha wachache wenye ukwasi ndo watakuwa na hold ya chama
Naionea sana huruma CDM, si kwasasa hivi ila baada ya sahivi, poleni wanamapinduzi.
 
Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,414
2,000
Hatuwezi kuendelea kwa kufanya siasa za watu badala ya kujikita kwenye sera ..kila siku hatuachi kujuta kwa ujinga wetu huu na leo tumetegwa tena na tumeingia wenyewe, tunafanya siasa za watu na tunashinda tunajadiri watu badaka ya sera zao na vyama vyao ..vyama vilete siasa za sera badala ya watu, tuna maswali ya msingi juu ya mambo mengi, tunahitaji sera si watu.
 
kigogo warioba

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
5,689
2,000
Lowasaa akishinda ndo mwisho wa CDM kwani naamini ataingiza mambo yake ambayo kimsingi hayashabihiani na CDM original, atafanya hivyo kwasababu kwanza yeye anaonekana ndo kaombwa na CDM ili awasaidie na kwasababu hata akishinda si kwasababu ya CDM, Lowassa hategemei chama ili kushinda kwasababu yeye anaamini ana watu wake tayari na ana pesa tofauti na magufuri anayesubiri kukampeniwa na chama ..sasa mtu ambaye hategemei chama ili ashinde akishinda chama kitawezaje kumcontrol ? atatii? kwa magufuri kwasababu anasaidiwa na chama chake anaamini chama vhake kitaendelea kuwa nguzo yake lakini kwa Lowassa atakuwa kama yeye na hata kama itahitajika kuwa na chama yeye ndo atakuwa juu ya chama either kwa direct ama indirect na kwa chochote atakachokifanya itabidi wote wakubali vinginevyo utaambiwa utoke ..hiki kitakuwa ni chama cha wachache wenye ukwasi ndo watakuwa na hold ya chama
Naionea sana huruma CDM, si kwasasa hivi ila baada ya sahivi, poleni wanamapinduzi.

acha uoga ww
 
Nzowa Godat

JF-Expert Member
Jun 15, 2011
2,756

Acheni woga Lowasa ni mwanasiasa mkongwe fullstop. Maswala ya Fedha, anazo za kawaida tu yaani ni tajiri kama matajiri wengine.
 
data

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
22,793
2,000
UKAWA ni nini hakuna kitu kama UKAWA kushika nchi. its abstract concept. Mnawajaza watu ujinga tu.
 
Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,414
2,000
UKAWA ni nini hakuna kitu kama UKAWA kushika nchi. its abstract concept. Mnawajaza watu ujinga tu.

Wahuni tu kama mwenyekiti wao mbowe wala hata hoja hawana viroba vinawahangaisha
 
Bahati furaha

JF-Expert Member
Jul 11, 2012
2,948
2,000
Lowasaa akishinda ndo mwisho wa CDM kwani naamini ataingiza mambo yake ambayo kimsingi hayashabihiani na CDM original, atafanya hivyo kwasababu kwanza yeye anaonekana ndo kaombwa na CDM ili awasaidie na kwasababu hata akishinda si kwasababu ya CDM, Lowassa hategemei chama ili kushinda kwasababu yeye anaamini ana watu wake tayari na ana pesa tofauti na magufuri anayesubiri kukampeniwa na chama ..sasa mtu ambaye hategemei chama ili ashinde akishinda chama kitawezaje kumcontrol ? atatii? kwa magufuri kwasababu anasaidiwa na chama chake anaamini chama vhake kitaendelea kuwa nguzo yake lakini kwa Lowassa atakuwa kama yeye na hata kama itahitajika kuwa na chama yeye ndo atakuwa juu ya chama either kwa direct ama indirect na kwa chochote atakachokifanya itabidi wote wakubali vinginevyo utaambiwa utoke ..hiki kitakuwa ni chama cha wachache wenye ukwasi ndo watakuwa na hold ya chama
Naionea sana huruma CDM, si kwasasa hivi ila baada ya sahivi, poleni wanamapinduzi.
"Sijawahi kuajiriwa au kufanya kazi mahali popote nje ya CCM na asienitaka yeye ndiye atoke ndani ya CCM." - ENL
 
J.I.M.S1237

Member
Jul 27, 2015
74
0
mambo magumu haya,mi naona enl ni mwanachadema,chama kitampgia kampen atake asitake,akiachwa anaweza kucheza karata dume kuwaua ukawa... lakin haya ni maon,naamin uwezo wake na sifa vinambeba japo jamii haina picha nzur kuhusu yeye, nasema hvo kulingana na wapga kura weng wapo vjijn ambako kuelewa ni ngumu kidogo,
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom