Wadau heshima kwenu,
Nitangulize kwa kusema kuwa mimi ni mdau wa ukawa na namini kuwa kwa tafiti zote zilizofanyika kabla ya uchaguzi huu kwa maana ya namba zinadhihirisha kuwa kwa ujio wa Mhe. Lowassa ushindi kwa ukawa si jambo la kuwa na mashaka kutokana na namba zilizowahi kutolewa.
Maswali magumu ya kujiuliza si kwa maana ya kugawa au kukatisha watu tamaa na kuna falsafa inasema tunapaswa kujiandaa na yatakayokuja hata kama hatuyapendi.
•Je, Ikibainika kuwa ujio wa Lowassa Ukawa ni mpango wa kiufundi uliopangwa na CCM ilikuhakikisha kuwa ikishinda CCM au UKAWA ushindi unabakia kuwa wao kwa maana ya dola.
•Je, Ikitokea ushindi ukapatikana kwa upande wa ukawa na uongozi wa juu kwa maana ya Rais ukashindwa kutekeleza kwa vitendo falsafa ya upinzani au ukawa, Nini kifanyike ili kutii kiu ya wananchi wengi kutaka mabadiliko?
Maoni yangu juu ya mashaka haya ambayo kimsingi si ya kubeza kutokana na matumaini makubwa ya mabadiliko waliyonayo watanzania.
1.Team yote ya ukawa inahitajika kuwa makini kuliko kipindi kingine chochote kwa maana ya kujiridhisha kwanza na maamuzi yeyote kabla ya kufikia hitimisho la maamuzi ya aina yeyote.
2.Team ya ukawa kupanga mipango mikakati ya kiutekelezaji na udhibiti wa taasisi ya urais baada ya ushindi kutokana na nature ya muungano wa ukawa ulivyo kwani Rais anaweza tumia nguvu zake kufanya mambo ayatakayo yeye mwenyewe ambayo yanaweza kuwa na mtizamo tofauti na matarajio ya wadau wa mabadiliko.
3.Kama ushindi utakuwa upande wa ukawa basi ni jambo jema kuwa au kukubaliana utaratibu utakao tumika katika kujaza nafasi za uteuzi ili kudhibiti zoezi hilo lisije kuwa na taswira ambayo inaonekana kwa sasa kwani matamanio yetu ni kuwa na mfumo bora na Imara katika kuendesha Taifa na unaotanguliza masilahi mapana ya Taifa.
Mtizamo wangu juu ya Mhe. Lowassa:
•Lowassa anaonekana ni mtu mwenye kiu kubwa ya kuwatumikia watanzania na kuwaletea maendeleo ya kweli napengine ndoto zake zimekuwa zikizimwa mara kwa mara.
•Lowassa anaonekana ni mtu ambaye amebezwa sana na baadhi ya wanachama wa chama chake cha zamani kuwa hawezi au hana sifa za kuwa kiongozi mkuu wa taifa na hasa kusemekana na baadhi ya watu kuwa Rais hawezi kutoka kazikazini, Mambo hayo yanaonyesha kumsononesha na huenda ndio imempelekea kufanya maamuzi magumu ya kujiunga na ukawa ili atmize ndoto zake na kuuhakikishia umma kuwa Rais anaweza toka upande wowote wa taifa letu.
•Ombi langu kwa Lowassa wakati ikitimiza ndoto zake za kuwa Rais akumbuke kuwa wanamabadiliko pia wako na ndoto zao za muda mrefu ambazo wanaimani zitatekelezwa na upinzani au ukawa na wanatamani ndoto hizo ziweze kufikiwa, akumbuke kuwa kutokufikia malengo makubwa ya ndoto za wadau wa mabadiliko kufaidi matunda au raslimali za taifa utakuwa umeturudisha nyuma hatua nyingi sana ambazo hatukuwa na sababu ya kurudi nyuma kwani mbele ni karibu zaidi kufikia matarajio yetu ya kuwa na taifa lenye uchumi bora na imara.
Karibuni kwa kuchangia kwa maana ya kujenga.