Izato
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 5,425
- 11,628
Hayajaisha mpaka yote yaishe ndani ya chumba hiki chenye kumbukumbu nyingi za kutisha na kuogofya!
Nakumbuka siku nilipopangiwa chumba hiki, asubuhi na mapema ilionekana ni siku iliyotulia kama nyingine zozote zilivyokuwa.
Mlango ulikuwa wazi na ndani ya chumba kulikuwa na sanduku jeusi tu pembezoni mwake, ambalo lilikuwa limeandikwa "ZINGATIA USIFUNGUE".
Niliwahoji baadhi ya wahudumu pamoja na meneja, na wote walisema, "Ni lazima kwa kila anayelala katika chumba hiki ni lazima azingatie takwa hilo, la sivyo majuto makuu yatamkuta.
Ilipofika saa tano mchana, sanduku lilianza kutetemeka. Sauti ndogo ikatokea ndani ya sanduku na ikaniita kwa jina langu, Tanzaniaa...
Kwa hofu na udadisi, nililisogelea na nikalifungua.
Kulikuwa na barua nyingi, saa zilizosimama, na picha za viongozi wazalendo zilizofifia.
Mojawapo ya barua ilikuwa ni kubwa size ya A4 na juu yake iliandikwa maneno yafuatayo,
" Sisi tulioishi humu tuliacha hofu zetu humu, na kwa kuwa umeamua kufungu sanduku hili basi unabeba lawama yote ya yatakayo kupata tangu sasa"
Ghafla, chumba kikawa cheusi. Dirishani, mwanga wa asubuhi ukaingia kwa shida kubwa, na kutia shaka ya kesho yangu na ya familia yangu.
Na hapo ndipo nikagundua Pandora Box haikuwa laana bali ni "fear of unknowns" kutoka kwa watu waliopewa dhamana juu ya watu. Ilikuwa ni gereza la hofu walizozificha kutokana ufedhuli na dhuluma walizokwisha kufanya juu ya maisha ya watu
Tume ya kwanza iliundwa na ilishindwa kuponya majeraha na hata ikataifishwa na mtuhumiwa mkuu, na hii ya sasa ni "Pandora Box" na hakika italeta sokomoko, pata shika na nguo kuchanika ndani ya chumba hiki.