Masuala ya Kingereza na Kiswahili Tanzania

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
32,229
50,380
Kuna issue fulani naifuatilia huko Bongo, halafu mojawapo wa vigezo ni kwamba, lazima mhusika awe anaongea Kingereza kwa ufasaha. Haya hapa maneno ya tangazo lenyewe "Strong communication skills in English", halafu Kiswahili hakijatajwa mahali. Nikajiuliza maswali mengi.

Hivi mbona Watanzania huwa hamueleweki linapokuja suala la lugha. Wakenya tukiongea Kingereza mnatuita watumwa, tukiongea lugha zetu za asili mnatuita wakabila na washamba. Yaani eti lazima tuongee Kiswahili ndio tuonekane kama watu waliostaarabika, Kiswahili chenyewe chanzo chake ni Mwarabu na Mwafrika pale Pwani kwenye biashara za utumwa.

Binafsi nakipenda Kiswahili sana, lakini pia napenda kuongea lugha zingine kadhaa. Hususan lugha yangu ya asili (Kikikuyu), naongea pia lugha za makabila ya hapa kwetu kadhaa. Na zaidi naongea Kingereza sana haswa nikiwa kwenye mishe zangu mjini. Halafu kipindi nikiwa Bongo nilijaribu kujifunza Kinyakyusa, Kihaya, Kipare japo hapakua na wahusika wengi wa kunifunza.

Sasa kusudi la huu uzi, mbona huwa mnaonekana kama mnachukia Kingereza halafu kwenye matangazo yenu mnaweka kama kigezo. Tatizo huwa nini, ama ni ule msemo wa sizitaki mbichi maana kimewakataa lakini inakua hamuwezi kujitoa.
 
Sio watanzania wote.Ni ambao kinawapiga chenga.Hawaishi kutafuta visingizio visivyo na msingi.I hope you understand me.
 
Iv ww aliokwambia hatuwez nan? Sisi hautuongei kiingereza kbovu km chenu
 
Sa mtani mbona unauliza jibu?
Kama wamesema "strong communication skills in English" halafu kiswahili hakijatajwa mahali ina maana tangazo hatujaweka sisi. :)
 
Sa mtani mbona unauliza jibu?
Kama wamesema "strong communication skills in English" halafu kiswahili hakijatajwa mahali ina maana tangazo hatujaweka sisi. :)

Hehehe!! Dah..avatar yako bana.. I love it.

Tangazo mumeweka nyie maana ni issue ya kiserikali...
 
  • Thanks
Reactions: kui
Kimsingi tunatakiwa kuzijua na kuzitumia lugha zote mbili, yaani kiswahili na kiingereza. Hizi ni lugha pekee zinazoweza kutuunganisha sisi watu wa Afrika mashariki na duniani kote.
 
Back
Top Bottom