Aina za maneno katika lugha ya Kiswahili

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,803
4,467
Salaam Wakuu,

Leo turudi shule kidogo tujikumbushe aina mbalimbali za maneno katika lugha. Mada hii itaeleza kwa ufupi aina mbalimbali za meneno zilizopo halafu mada zijazo ntagusia aina moja moja kwa upana wake. twende kazi hapa chini:

Kabla hatujaenda kiundani kuelezea aina za maneno kwanza ni muhimu tukajua dhana ya neno. Ushawahi kujiuliza neno ni nini?

Maana ya neno au maneno

Neno au maneno ni kipashio/ Vipashio kidogo zaidi kinachojihimili katika sentensi. Kiungo hiki (neno) huwakilisha maana inayokubalika katika sarufi ya lugha maalum.

Aina za maneno
Kuna mijadala kadhaa kuhusu idadi halisi ya aina za maneno katika lugha, wapo wanaoamini kuwa aina za maneno zipo saba na wengine wanadai zipo nane. Katika andiko hili sitajihusisha kabisa na mjadala huo isipokuwa nitafafanua idadi nane za aina za maneno zinazoelezwa na wengi. Hivyo zifuatazo ni aina nane za maneno katika lugha ya Kiswahili.
  • Nomino (N)
  • Vitenzi (T)
  • Viwakilishi (W)
  • Vivumishi (V)
  • Vielezi (E)
  • Viunganishi (U)
  • Vihusishi (H) au Vibainishi
  • Vihisishi (I)
NOTE: Herufi zilizowekwa katika kila aina ya neno ndio kifupi kinachotambulika kwa neno husika.

1. NOMINO (N)
Nomino ni maneno yanayoeleza majina ya watu, vitu, mahali, hali, tabia au taratibu. Kwa mfano, Fatma, uvivu, nyumbani. Zipo aina mbalimbali za Nomino ambazo nitazifafanua kiundani katika andiko linalofuata. (Zaidi soma: Aina za Nomino katika Lugha Kiswahili)

2. VITENZI
Vitenzi ni maneno yanayoarifu kuhusu jambo linalotendwa au kutendewa nomino. Vitenzi huwa na mzizi ambao kwamba ndio unaosimamia tendo lenyewe na mzizi huo huambatanishwa na viambishi ili kuleta maana inayokusudiwa. Kwa mfano, alipita. (zaidi soma: Aina za Vitenzi (T) katika lugha ya Kiswahili)

3. VIWAKILISHI
Viwakilishi ni maneno yanayotumika badala ya nomino(vibadala vya nomino). Nomino husika huwa haitajwi katika sentensi. Kwa mfano, yule ni mtunzi mbuji wa mashairi. (Zaidi soma: Aina za Viwakilishi (W) katika lugha ya Kiswahili).

4. VIVUMISHI
Kivumishi ni neno au fungu la maneno linaloeleza zaidi juu ya nomino. Kivumishi ‘huvumisha’, yaani hueleza mtu namna alivyo au kitu nama kilivyo, kinavyofikirika au kufikiriwa. Pia huonyesha idadi fulani ya kile kinachozungumziwa. Kuvumisha ni kutoa habari. Pia, tunaweza pia tukasema, Vivumishi ni maneno yanayosifu au kufasili sura za nomino. (Zaidi Soma: Vivumishi (V) na aina zake)

5. VIELEZI
Vielezi ni maneno yanayotumika kufafanua kitenzi, kivumishi au kielezi kingine. Wakati mwingine vielezi tunaweza vifafanua kama maneno yanayosifu au kufasili sura za vitenzi, vivumishi au vielezi vingine. (Zaidi soma: Vielezi (E) na maana zake)

Vielezi vinapotumika kufafanua vitenzi

- Mfano;
Mweha aliteleza vibaya.

vielezi vinapotumika kufafanua vivumishi

- Mfano: Kijana aliyekuja jana ni mrefu sana

vielezi vinapotumika kufafanua vielezi vingine

- Mfano: Agnes alipika chakula vizuri sana

6. VIUNGANISHI
Viunganishi ni maneno yanayotumiwa kuunganisha vipashio mbali mbali vya lugha. Kwa kawaida, huunganisha vipashio vifuatavyo: (Zaidi soma: Viunganishi (U) na aina zake)
  • Neno na neno
  • Kirai na kirai
  • Kishazi na kishazi
  • Sentensi na sentensi
7. Vihusishi au Vibainishi
Asili ya kwa ni a-unganifu. Hutumika kwa namna mbali mbali. Kwa mfano:
  • Mahali
  • Jinsi/namna
  • Kilichotumiwa/kifaa
  • Sababu

Mifano katika sentensi:
  • Pale ni kwa kaka yake.
  • Tukwenda kwa basi.
  • Amejawa na majoniz tele.
8. VIHISISHI
Haya ni maneno ya mshangao au ya kutoa hisia za ndani za mhusika. Vihishi huishia kwa alama (!)

Mwisho, baada ya kuona aina za maneno kwa ufupi katika maandiko yajayo tutachimba katika kila aina ya neno moja moja ili tuelewe kiundani. Waswahili wanasema fupi tamu ndefu inakera. Basi Waaaape salaam ndugu zetu wa huko Uswahilini.

Mwakisyala Signed

Credit kutoka vitabu:
- Kimani Njogu na Dorothy K. Nganje, kiswahili kwa vyuo vya ualimu: Jomo Kenyatta Foundation 2006

- Kimani Njogu, Alice Mwihaki na Aswani Buliba, Sarufi ya kiswahili: uchanganuzi na matumizi: Jomo Kenyatta Foundation 2006.

- Jamvi la Uhakiki wa Kiswahili
 
Back
Top Bottom