Masters inalipa Sana katika ajira kwa sasa?

Masters inalipa Sana katika ajira kwa sasa?

Nitapanga hapa Na wewe utakuja Na list yako according Na vIgezo vyako.
1. Masters in project Management
2. Masters in Education Administration and Planning policy
3.Masters in Public Health
4.Masters in Logistic Management
5. MBA in Finance, Accounting,Procurement
Tanzania kuna chuo kinachotoa Master of Arts in Special Education.....?? nauliza?
 
Masters ya education faida yake no moja tu daraja litaendelea kupanda mbali na hapo sidhani kama inalipa kulinganisha na hizo nyingine
Naomba kuuliza,kuna chuo chochote Tz kinatoa Master of Arts in Special Education....??
 
Hiyo #5 ni usanii mtupu, hamna kitu kama hicho, na kama kuna chuo kinatoa hiyo koz ni kuvutia watu tu, labda utuambie pia ni miaka mingapi?
 
Masters ya education faida yake no moja tu daraja litaendelea kupanda mbali na hapo sidhani kama inalipa kulinganisha na hizo nyingine
Binafsi simshauri kabisaaaa huko kwenye education,kwa sababu hata akiisoma kama yupo serikalini haitaongeza kitu,atasubiria daraja,wakat baadhi ya kada akirud na masters na stories zinabadilika hapo kazini,promotion fasta.
Ndo maana rais na waziri mkuu waliachana na ualim.
Ualim miyeyusho sana,daraja waweza pandishwa leo,ila mshahara ukausubiri hata miaka mitano.
Nilipata MA EDU na MA dev maganement nikaona nikasome hyo ya Development Management walau naweza kujiajiri nikiwa na laptop yangu chumbanj,UALIM yatosha
 
Engineering like CoET wanatoa ila pia Dept of Geography wanatoa,hapo nazungumzia UDSM
Course inaitwa Project Planning and Management ni evening program
Asante kwa info mkuu, je unafahamu course requirement? Like what background should I have to qualify for it.
 
Asante kwa info mkuu, je unafahamu course requirement? Like what background should I have to qualify for it.
Mdau ile cousre haina requirements,maana ni ya Social Science.Kama una back ground ya sosho science unaweza soma tu.
Muhim ujue utaratibu wa ada,cause ni mil 8 na pia ni 24 months,sijui wanalipajelipaje
 
UOGA WA KUJIAJIRI HIYO ADA YA MASTERS MILIONI 7 UKIFUGA KUKU LAZMA UTOKE KIMAISHA
 
UOGA WA KUJIAJIRI HIYO ADA YA MASTERS MILIONI 7 UKIFUGA KUKU LAZMA UTOKE KIMAISHA
Ni wazo zuri mdau umetoa,hop watu watasoma hapa,ila hizo 7 hazitolew kwa mkupuo,na bado kusoma kuna logic.
Mfano mimi nilichoenda kukisomea hakihusiani na ajira yangh,na nashukuru nimeanza kukifanyia kazi nje ya mfumo rasmi wa ajira yangu,mwaka huu naongeza juhud ili nifanikishe zaid
 
unaeza soma MPH ,andaa ada !application ni april ,vyuo ni viwili paka sasa,udsm and muhimbili.
 
Nadhan
Masters ya education faida yake no moja tu daraja litaendelea kupanda mbali na hapo sidhani kama inalipa kulinganisha na hizo nyingine
Nadhani hii masters italipa endapo serikali itaweka bayana kwamba mtu akiwa nayo apande daraja moja kutoka lile alilopo maana kwa sasa unapata increment mbili ambapo hailingani na maarifa unayoyapata na matumizi ya shule hii uwapo darasani au kwenye administration post
 
Back
Top Bottom