Masters inalipa Sana katika ajira kwa sasa?

Yaani vijana wa Tanzania bwana utasema wamerogwa.....kila jitu mawazo yake ni kuajiriwa.......
Jitu linakuuliza eti nikisoma kozi hii nitaajiriwa kweli.........

Yaani kuna mijitu ipo radhi hata kuuza nyumba ili isome na baadaye ije kuajiriwa na kuna mijitu ipo tayari hata kukaa miaka ishirini inasubiria ajira tu......yaani yenyewe inawaza kuajiriwa tu.......katika vichwa vyao.......
Alafu eti ikikaa pamoja inajiita misomi na kazi kutwa nzima ni kusoma magazeti ya kiingereza na kuangalia BBC.......Msomi gani unashindwa hata kubuni kamradi ka kukuingizia kipato mpaka unangoja uajiriwe.......

Halifikirii kuwa kwenye hayo mashirika binafsi anayoyangoja yampe ajira yalianzishwa na watu......

Pamba.vuu zao kabisaaaaa.....

Kutokana na upeo wako ni haki yako kuropoka na kutukana, naomba nikueleweshe kitu, mtoto wa familia ya kitanzania kasomeshwa na kwa taabu amemaliza degree yake, wale waliokuwa wakimsupport baada ya kumaliza degree yake, hawamsupport tena anaingia soko la ajira anatafuta kazi kwa mda mrefu hata mwaka mmoja, anakuja na miradi ya kujiajiri , anaangalia fursa zilizopo mtaani kwake mpango biashara unakaa vizuri kabisa, anakuja na idea ya kuzoa takataka, anakuja na idea ya kilimo, ni sawa tatizo atapata wap mtaji, kama hana mtu wa kumshika mkono, anenda seminar, anajifunza kwenye kwa matendo ishu inabakia atapata wap mtaji, anakuja na idea ya kupull capital anakusanya watu. Wanaanza ila sababu mtaji wao ni mdogo changamoto zinapokuja zinakula mtaji au kutingisha mtaji maana bado si mzoefu, wale waliomsomesha hawamuelewi wanampa pressure kuwa kasoma alafu anafanya kazi ambazo za wasiosoma, mwisho wa siku anatakiwa apate kazi ahudumie familia yake, ni mda wa kurudisha fadhila kwa waliokusomesha, ni mda na yeye asomeshe ndugu zake kama yeye alivyosaidiwa, kwa sababu ya mtaji mdogo hawezi kuajiri watu mambo yote anafanya yeye, mwisho wa siku unajiuliza uyu kasoma ili iweje tofauti ya kazi anazofanya na wasio soma hakuna, na bado hata izo ela hazimtoshi kuiishi, kwa iyo watu wanaonyooshea watu vidole eti hawajiajiri, eti hawatumii akili zao je umewashika mkono? Umewatafutia wafadhili wa kuwasaidia mipango biashara yao? Mfumo uliopo si rafiki kwa vijana wasomi kujiajiri, kumejaa rushwa, kumejaa urasimu, kila mahali serikali inangilia kati, kila mtu anataka pesa toka kwako wanaosurvive ni wale wenye mtaji mkubwa. Lakini huku chini unapoteza mda tuu, watu ajira
 
Wanaenda sababu hakuna jinsi, mazingira hayaruusu kijana kujiajiri hasa kijana msomi, badala ya kuwanyoshea vidole njoo na policy, njoo na solution za mitaji watapata wapi? Wakaibe? Mazingira ya Tanzania kazi kwanza ndipo upate mtaji wa kufanya biashara, tofauti na hapo upate mtu wa kukushika mkono.
 
Kutokana na upeo wako ni haki yako kuropoka na kutukana, naomba nikueleweshe kitu, mtoto wa familia ya kitanzania kasomeshwa na kwa taabu amemaliza degree yake, wale waliokuwa wakimsupport baada ya kumaliza degree yake, hawamsupport tena anaingia soko la ajira anatafuta kazi kwa mda mrefu hata mwaka mmoja, anakuja na miradi ya kujiajiri , anaangalia fursa zilizopo mtaani kwake mpango biashara unakaa vizuri kabisa, anakuja na idea ya kuzoa takataka, anakuja na idea ya kilimo, ni sawa tatizo atapata wap mtaji, kama hana mtu wa kumshika mkono, anenda seminar, anajifunza kwenye kwa matendo ishu inabakia atapata wap mtaji, anakuja na idea ya kupull capital anakusanya watu. Wanaanza ila sababu mtaji wao ni mdogo changamoto zinapokuja zinakula mtaji au kutingisha mtaji maana bado si mzoefu, wale waliomsomesha hawamuelewi wanampa pressure kuwa kasoma alafu anafanya kazi ambazo za wasiosoma, mwisho wa siku anatakiwa apate kazi ahudumie familia yake, ni mda wa kurudisha fadhila kwa waliokusomesha, ni mda na yeye asomeshe ndugu zake kama yeye alivyosaidiwa, kwa sababu ya mtaji mdogo hawezi kuajiri watu mambo yote anafanya yeye, mwisho wa siku unajiuliza uyu kasoma ili iweje tofauti ya kazi anazofanya na wasio soma hakuna, na bado hata izo ela hazimtoshi kuiishi, kwa iyo watu wanaonyooshea watu vidole eti hawajiajiri, eti hawatumii akili zao je umewashika mkono? Umewatafutia wafadhili wa kuwasaidia mipango biashara yao? Mfumo uliopo si rafiki kwa vijana wasomi kujiajiri, kumejaa rushwa, kumejaa urasimu, kila mahali serikali inangilia kati, kila mtu anataka pesa toka kwako wanaosurvive ni wale wenye mtaji mkubwa. Lakini huku chini unapoteza mda tuu, watu ajira
Ukweli unaoukataa ni kwamba vijana wengi wasomi ni wanachagua kazi balaa...nina mtoto wa kaka yangu amemaliza chuo na huu ni mwaka wa nne sasa yupo nyumbani anasumbukia kazi....
Mdogo wake aliyeishia kidato cha sita...akaanza kuuza viazi sokoni kwa kupanga chini.....sasa hivi anaagiza gari nzima ya viazi yeye mwenyewe......na amefungua maduka mawili ya tigo pesa yanayomuingizia fedha mzuri tu....
 
Nadhani kama taifa tuna tatizo. Elimu yetu imekuwa ikijengwa katika misingi ya madaraja. Kuna baadhi ya kozi unasoma ukiuliza matumizi yake unaambiwa itakusaidia ukienda masters kana kwamba kila mtu lazima aende masters.

Hii ndio sababu mtu anamaliza degree ya kwanza na mambo yakiwa magumu ama kwakukosa kazi au kuwa na maslahi madogo then chakwanza anachowaza ni masters. Kuna vijana wengi sana leo hii wenye masters na kwa bahati mbaya bado wengi wao hawajapata kazi kwakuwa wengi walienda kusoma.ili tu wawe na masters degree kitu ambacho sio sahihi.

Nafikiri ingekuwa vema.kama tungeweza kuwa na mfumo ambao mtu anakwenda mastees kwakuwa anaona anahitaji.maarifa fulani zaidi na kutaka kuwa na tija zaidi kazini. Hii ingesaidia sana kwakuwa watu pia wangesoma kozi wanazozipenda ila sio kama ilivo leo.

Sasa kuhusu MA ED waalimu wanapata shida kwakuwa hata wakiwa nayo mishahara haibbadiliki. Hapa kuna hoja nyepesi na nzito kuhusu hili.

HOJA NYEPESI
Waalimu ni wengi kwa hiyo wote wakiruhusiwa kuengezewa mishahara kwasababu tu ya kuwa na masters then serikali itakuwa na mzigo mkubwa sana. Kwa idadi yao na wengi kwa sasa wanavopenda kusoma itakuwa ni fedha nyingi sana kuwalipa wote.
Pili hali hii.itakuwa kichocheo kikubwa sana cha walimu kukimbilia kusoma zaidi kuliko.kufundisha hali inayoweza leta upungufu mkubwa wa walimu mashuleni. Kwahiyo kuzui hayo inabidi masters isiwe na mshahara kwa kada ya ualimu.

HOJA NZITO
Kuwa na masters maana yake ni kuwa na ujuzi na maarifa zaidi ambavyo vitaleta tija na ufaninisi. Sasa mtu mwenye MA ED halafu anafundisha form ONE somo lolote eg geography ni kwanamna gani ufanisi wake utaongezeka kwa yeye kuwa na masters? Nadhani hakuna uwiano wa moja kwa moja kati ya kilicho somwa na anachofundisha. Sasa hapo mshahara uongezwa kwa sababu gani yani?
Elimu ni moja kati.ya.vitu vinavyoleya WAGE DIFFERENTIAL ila lazima iwe na mchango katika kazi vinginevyo itakuwa haina tija kuwa na elimu kubwa. Hata hivyo kwakuwa tumekuwa kimaslahi zaidi nashauri tu tufanye tafiti kwa muda kabla ya kuamua.kwenda kusoma tusijejikuta hakuna badiliko au.kazi hata kwa kutumia vyetu vetu vya masters.....
 
Nnapenda kazi ya ualimu kutoka kwenye uvungu wa moyo, sijawaza kabisa kama nitaiacha hivo nitasoma masters ya education tena
Safi sana unaweza kuwa moja kati ya walimu wache sana ambao wanaipenda kazi.yao,mmoja kwa malaki. Hongera sana ila nadhani ukisoma MA ED baada ya miaka.kadhaa unaweza jikuta umekuwa SLO ,DEO siku hizi kuna WEO. Je kwa mazingira hayo si utaacha kufundisha na kuwa mtawala? Na je si utamiss wale watoto wako.wa.form three B? Hudhani.ingekuwa vyema kutokujiendeleza ili ubaki kuwa mwalimu darasani.zaidi?
 
Yaani vijana wa Tanzania bwana utasema wamerogwa.....kila jitu mawazo yake ni kuajiriwa.......
Jitu linakuuliza eti nikisoma kozi hii nitaajiriwa kweli.........

Yaani kuna mijitu ipo radhi hata kuuza nyumba ili isome na baadaye ije kuajiriwa na kuna mijitu ipo tayari hata kukaa miaka ishirini inasubiria ajira tu......yaani yenyewe inawaza kuajiriwa tu.......katika vichwa vyao.......
Alafu eti ikikaa pamoja inajiita misomi na kazi kutwa nzima ni kusoma magazeti ya kiingereza na kuangalia BBC.......Msomi gani unashindwa hata kubuni kamradi ka kukuingizia kipato mpaka unangoja uajiriwe.......

Halifikirii kuwa kwenye hayo mashirika binafsi anayoyangoja yampe ajira yalianzishwa na watu......

Pamba.vuu zao kabisaaaaa.....
My friend kuajiriwa sio dhambi and for your info. watu wameajiliwa na wanaproject pembeni zinawalipa tu. Mi nadhani kama shule yako inakuruhusu kuajiriwa ajiriwa then through your salary anzisha project pembeni ili multiplier effect tuione maana utawapa watu wawili watatu ajira ambao serikalini au kwa private sector hatuwezi tosha wote
 
Safi sana unaweza kuwa moja kati ya walimu wache sana ambao wanaipenda kazi.yao,mmoja kwa malaki. Hongera sana ila nadhani ukisoma MA ED baada ya miaka.kadhaa unaweza jikuta umekuwa SLO ,DEO siku hizi kuna WEO. Je kwa mazingira hayo si utaacha kufundisha na kuwa mtawala? Na je si utamiss wale watoto wako.wa.form three B? Hudhani.ingekuwa vyema kutokujiendeleza ili ubaki kuwa mwalimu darasani.zaidi?
Hao kina DEO na MEO ni kupeana kwa kujuana na hela pia, kuna jamaa aliambiwa atoe hela apewe uDEO akatoa akalamba cheo, kuna watu wana masters na wote tunafundisha, nadhani mie nitaendelea kufundisha pia sitaki utawala
 
Hapo umesema kweli maana hivi vyeo......
 
Master of edctn kwa kweli ili uheshimike sana ukasome nchi nyingine ,kwanza tunazungushana kupeana hiyo mastres, yan vyuo vyeyu hvi sijui vikoje mtu Master mwaka mmoja utakuta unappiga hadi 3 yrs sasa si ujinga huoooo
 
Master of education ndo iko powa na ina matter kuliko hizo zingine ulizo orodhesha
 
Hivi ulimwengu huu wasomi wetu mnawaza kuajiriwa tu.kwa nini msiwaze mkimaliza masomo mtengeneze ajira kwa wasiofanikiwa kwenda shule?
 
Back
Top Bottom