Master programmes kwa kichina | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Master programmes kwa kichina

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by kamikaze, Mar 17, 2011.

 1. kamikaze

  kamikaze JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  Natumai wana jf wote ni wazima. Kuna kitu naomba nieleweshwe, nimekua nikisikia baadhi ya wanafunzi wa kitanzania wakienda china kusoma masters programmes mbalimbali zinazofundishwa kwa lugha ya kichina.Swali langu ni kuwa huwa wanaelewa vizuri masomo kama ambavyo wangesoma kwa kiingereza maana naona kichina ni kigumu na vp kuhusu ubora wa elimu ya china ukilinganisha na ya hapa kwetu Tanzania.Majibu ya haya yanaweza nipa mshawasha nami nikatafuta nafasi ya kwenda kusoma huko.
  Natumai humu jf kuna watu wamesoma china na wengine angali wanasoma au ndugu zao wamesoma huko, hivyo nategemea kupata majibu ya kuridhisha.
  AKSANTENI
   
 2. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,603
  Likes Received: 6,770
  Trophy Points: 280
  Kwanza Inategemea Chuo unachokwenda, kuna vyuo wanatoa Mastyers kwa Kiingereza mfano kuna Chuo kinaitwa Huazhong University of science and technology, hawa wana Masters zinazofundishwa kwa Kiingereza.

  Pili, iwapo chuo unachotaka kusoma hakina kozi zifundishwazo kwa kiingereza, basi inakubidi usome mwaka mmoja wa Kichina kwanza, ili uielewe lugha, then baada ya hapo unaanza kozi yako.

  Kuhusu kuelewa, kuna mambo mawili, moja inategemea background yako katika bachelor incase unachukua masomo yanayoendana, pili uwezo wa kuelewa wewe binafsi.

  Kuna nyenzo nyingi za kumsaidia Foreigner kujifunza kozi yake bila ya kukimaster kichina vizuri sana, mathalani Kuna vitabu vingi vya Kiingereza navyo ni cheap, unakuta kitabu anachokitumia mwalimu cha kichina lakini ni direct translation ya kitabu cha kiingereza ambacho kinapatikana. pia Kuna Material Kibao online, kwa hiyo kama ni kujisomea ushindwe wewe tu.

  Linapokuja suala la mitihani, Kuna vyuo vinaruhusu foreigner kuchanganya Kichina na Kiingereza katika Kujibu maswali, iwapo utaamua kutumia kichina tupu katika swali la kwanza au idadi yoyote, then ukaamua kutumia Kiingereza kujibu maswali mengine Hewala, lakini siyo "KICHIENG" katika kujibu swali moja.

  Hata kama Mwalimu anafundisha kwa Kichina, Walimu wa sasa hivi wa Kichina ni Rika la vijana ambao wengi wako open minded, wanajua kiingereza vizuri, kwa hiyo Ni wewe tu kumsumbua mpaka uelewe unachokitaka kukisoma.

  Kichina ukikisoma vizuri, itafikia wakati unasoma kitabu hata cha sayansi na kuelewa vizuri kabisaa, ila tatizo litakuja pale utakapotaka Kuyaandika hayo uliyoyaelewa!, kwa hiyo kichina cha kuandika ni kigumu kwa foreigners wengi, isipokuwa zipo nyenzo za kusaidia katika hilo, kuna electronic dictionaries, kuna translation softwares kama vile GOOGLE LANGUAGE TOOL.

  Kitu kingine ni kwamba Kichina si cha kusoma na kukiacha, kinahitaji progressive learning. Hata Sisi tunaozungumza Vichina tunazidiana, ukimsikiliza mwenzio anapokibonga kichina unaweza kujua kwamba huyu mwenzio maji marefu au si mkali kivile.

  欢迎你到中国来读书(KARIBU CHINA USOME)
   
Loading...