Walaka kwa wabunge wote na idara za elimu

Mshinga

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,532
1,124
TUINUSURU ELIMU YA TANZANIA

hali ya elimu ya tanzania ipo katika hali mbaya sana inayohitaji hatua za dharula.

KWA
1.WABUNGE WOTE
2.WAZIRI WA ELIMU SHUKURU KAWAMBWA(MB)
3.TUME YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA(MB)
4.HAKI ELIMU
5.WAZIRI KIVULI WA ELIMU
6.JAMES MBATIA(MB)

7.TSNP(TANZANIA STUDENTS NETWORKING PRORAM)
8.TAHOSA(TANZANIA HEADS OF SECONDARY ASSOCIATION)
9.WAZIRI MKUU
10.WANAFUNZI WOTE NCHINI
11.WALIMU WOTE NCHINI
12.NECTA

0683 783379(MWANAFUNZI),09/05/2013



HALI ILIVYOKUWA KABLA YA KUFIKIA ANGUKO HILI BAYA KABISA

1.shule za serikali zilikuwa chache sana kiasi cha kusababisha wanafunzi wengi waliohitimu elimu ya msingi kwa kiwango kinachokubalika kisheria kushindwa kupata elimu ya sekondari kwa sababu tu hakuna pa kuwapeleka hata kama walipenda kuendelea na masomo na sababu hii iliwanyima haki yao ya msingi kuendelea na masomo.
NAMNA PEKEE YA KUTATUA TATIZO HILI ILIKUWA KUONGEZA SHULE.

2.shule chache zilizokuwepo kwa kiasi kikubwa zilikuwa shule za bweni na kwa maana hiyo wanafunzi walikabiliwa na changamoto sawa katika huduma za kijamii mfano:changamoto za maji na umeme na kwa kuwa shule zilikuwa za bweni hapakuwa na tatizo la usafiri kwa shule za mijini ama umbali mrefu kwa wale wanafunzi wa vijijini.
KUWAAWEKA WANAFUNZI PAMOJA ILIRAHISISHA KUTATUA MATIZO YA UMEME,MAJI,USAFIRI NA ATHARI ZA MIJUMUIKO YA KIJAMII[effects of social interaction]WAKATI WA KIPINDI CHA SHULE NA MASOMO NA PIA WANAFUNZI WALIEPUKA KAZI ZA NYUMBANI JAPO WALIFANYA KAZI KWA RATIBA ZA SHULENI.
Kwa ufupi wanafunzi walikuwa na mda mwingi wa ziada kujisomea wenyewe na kwa kufata ratiba za shule za kila siku maarufu kama PREPO

3.vitabu vya shule kwa kiasi kikubwa vilikuwa vya aina moja na ubora wake ulikuwa wa kuridhisha sana na vilitolewa na kusambazwa na serikali yenyewe kwa kiwango cha kuridhisha.kwa upande wa A LEVEL serikali haikuwa na vitabu vyake hasa vile vya masomo ya sayansi lakini ilitumia vitabu vya kimataifa kama vya cambrige,oxford nk.
KWA MKUTADHA HUU WANAFUNZI WOTE NCHINI WALIKUWA NA MAZINGIRA SAWA KATIKA VITABU VYA KUJIFUNZIA NA HILI LILIONDOA TABAKA KATIKA MATUMIZI YA VITABU

4.upungufu wa walimu pia ulikuwepo na kupelekea shule nyingi kutokuwa na idadi ya walimu kwa mahitaji ya kila shule.
CHANGAMOTO HII ILIATHIRI UBORA WA ELIMU KWA WANAFUNZI.
NJIA PEKEE YA KUTATUA HILI ILIKUWA KUANGALIA NAMNA YA KUPATA AMA KUONGEZA WALIMU

5.mishahara midogo ya walimu nalo lilikuwa ni tatizo kubwa,kudhihirisha hili japo nilikuwa mdogo sana lakini nimepata kusimuliwa mara nyingi WAKATI WA UTAWALA WA MZEE WA RUKSA WALIMU WALIAACHA KAZI NA KUAMUA KUFANYA BIASHARA(WALE WALIOKUWA WAKUBWA KAMA MASHUHUDA MNAWEZA KUDHITISHA AMA KUSAHIHISHA MAELEZO HAYA)

6.Kuna wakati hasa miaka ya 2000(2000s) kulikuwa na tatizo kubwa la kuvuja kwa mitihani na hili nililishudia katika miaka ile na kabla ya hapo sifahamu tatizo hili lilikuwa na ukubwa kiasi gani kwani nilikuwa ndo kwanza shule ya msingi.

7.wanafunzi bado hawakufundishwa inavotakikana hata pale walimu walipokuwepo, wanafunzi walilazimika kujisomea na kujifundisha wenyewe kwa wenyewe na hili liliwezekana kwa sababu wanafunzi walikuwa wanakaa pamoja na ilikuwa msaada mkubwa kwao kukabili tatizo la walimu na tatizo la uzembe wa walimu.

SERIKALI ILICHUKUA HATUA ZA KUTATUA MTATIZO YA UPUNGUFU WA VITABU,WALIMU NA SHULE.

TATIZO LA VITABU
serikali iliruhusu watunzi binafisi wa vitabu lakini ilichukua tahadhari kwa kuanzisha chombo cha kuhakiki na kudhibiti ubora wa vitabu kabla havijapewa vibali vya kutumika kama vitabu vya kiada.chombo kile kinajulikana kama EMAC(education matereal approval comitee, kama sijakosea)
VITABU VINGI VILITUNGWA MWANZONI NA BAADA YA MWAKA 2000,NA HAPO NDIPO VITABU VINGI VILITUNGWA NA NYAMBARI NYANGWINE KWA MASOMO YA ARTS NA ALIFADHIRI PIA UTUNGAJI WA VITABU VINGI KATIKA MASOMO MENGINE YALIYOKUWA NJE YA TAALUMA YAKE,kwa wale wanafunzi wenzangu mtakumbuka vizuri sana japo si wanafunzi wengi waliweza kununua vitabu vile ila ilikuwa neema kwani wakati ule tayari kulikuwa na mashine za kutoa kopi(photocopy mashine) na hivyo wanafunzi wengi tuliweza kutoa kopi ya vitabu hivyo.
NA NIKIRI NA KUTOFAUTIANA NA WENGI WANAOVIPINGA,VITABU VILE VILITUSAIDIA SANA MANA VILIKUWA SUMMARIZED NA ILIKUWA RAHISI KUVITUMIA.
vilikuwa ni vitabu sahihi kwa mfumo wa wakati ule wa kukariri(CONTENT) na ni kweli kuwa visingefaa kwa mfumo wa uelewa mpana wa kutoa maelezo(COMPITENCY).wapo walimu waliovipinga kwa kuwa vilikuwa summarized japo hili haliondoi ukweli kwamba walimu wengi walivitumia kufundishia hasa wale waliokuwa wazembe kuandaa notisi.
UTUNZI WA VITABU KUFUATIA SYLABUS MPYA 2005 na 2007
Serikali ilibadili mitaala lakini cha kusikitisha zaidi ni kwamba vitabu vya serikali kwa mitaala mipya vilichelewa kutoka na ilichukua mpaka miaka mitatu mpaka minne ndipo vilitoka.
Waandishi binafsi walitoa vitabu kwa hitaji la mitaala mipya mapema zaidi na haikuchukua zaidi ya mwaka kwa waandishi binafisi kutoa vitabu vipya .
HAPA ITOSHE KUSEMA KUWA SERIKALI HAIKUJIANDAA KUKABILI MAHITAJI YA MITAALA MIPYA KWA KUTOA VITABU MAPEMA KAMA ILIVYOHITAJIKA NA KUWAACHIA WAANDISHI BINAFSI PEKEE.

UBORA WA VITABU BAADA YA MITAALA MIPYA 2005
Nianze kwa kutoa pongezi kwa vitabu vyote bora ama vizuri kwani vinasaidia jamii ya watanzania,najua ni EMAC pekee iliyo na mamlaka kisheria kudhibitisha ubora wa vitabu lakini hili halinizuii kueleza hisia na mawazo yangu kwani katiba inatambua uhuru wa mawazo ya kila mtu.
NI MASIKITIKO MAKUBWA KUWA VITABU VINGI VYA SERIKALI VINAVYOTUMIA MAMILIONI YA SHILINGI YA PESA YA WALIPA KODI MASIKINI NDIO VITABU VIBOVU KABISA NA VIKIUZWA KWA BEI KUBWA ZAIDI MFANO NI KITABU CHA HESABU KIDATO CHA PILI (mtaala wa 2005) kilichotolewa na wizara ya Tanzania bara,KWA WANAOJUA HESABU ANGALIA NA KUPITIA TOPIKI MOJA TU YA LOGARITHM,kitabu hiki hakifai maana mwanafunzi akisoma hapa atakuwa ameshafeli hata kabla hafanya mtihani.

Nitambue vitabu vizuri vilivyotungwa na wizara ya serikali ya Zanzibar kwa ushirikiano na watu wa marekani USAID hasa chemistry,physics na biology,kama kuna mapungufu basi ni yale ya kawaida

Pia nitambue pia vitabu vizuri toka kwa waandishi binafisi(sitataja vitabu hivyo) hata kama vitabu vile havikuwahi kupewa nembo ya EMAC ama vilipewa baada ya mda mrefu kupita.
LAKINI NISEME PIA KUWA EMAC IMESHINDWA KABISA KUTEKELEZA WAJIBU WAKE ,MANA NI AIBU KUKUTA VITABU VINA NEMBO YA EMAC LAKINI NI VIBOVU AMA VINA MAPUNGUFU MAKUBWA WAKATI KUNA WATU WAMEAJILIWA KUHAKIKI VITABU HIVI KABLA HAVIJAPA RUHUSA YA KUWA VITABU VYA KIADA
HUJUMA YA VITABU VYA MSAADA KUTOKA WATU WA MAREKANI USAID.
Vitabu vilivyotolewa kwa msaada wa USAID vingi vilikwapuliwa na kuuzwa kwa bei ya chee sana na wafanyabiashara waliviuza madukani kwa kukwangua maandishi yaliyosomeka NOT FOR SALE.hili halikubaliki kwa wale waliokabidhiwa dhamana ya kusambaza vitabu hivi.

TATIZO LA UCHACHE WA SHULE ZA SEKONDARI
Serikali iliazimia kupunguza ama kuliondoa kabisa tatizo hili lililokuwa linasababisha wanafunzi waliofauli na kufikia mashariti ya kusoma kidato cha kwanza kukosa fursa hiyo kwa sababu tu ya uchache wa shule kama ambavyo mimi mwenyewe na wanafunzi wote tuliomaliza ILOLA SHULE YA MSINGI-SHINYANGA(2001) tulikosa kupata fursa hiyo LICHA YA KUFAULU MAANA UCHACHE WA SHULE ULITUPONZA.kimsingi lilikuwa ni jambo jema kumaliza tatizo hili na ndio maana watanzania waliitikia kwa kiasi kikubwa na kujenga shule za kata nchi nzima kwa kushilikiana na serikali,maana walijua ni jambo jema.
KOSA KUBWA ILILOFANYA SERIKALI KATIKA MPANGO HUU NA LIWE FUNZO KWA MIRADI NA MIPANGO MINGINE MIKUBWA YA NCHI.
Serikali ama haikufanya uchunguzi ama ilifanya feasibility study yenye udhaifu mkubwa ambao umepelekea anguko kubwa la elimu kiasi ambacho takribani 95% ya wanafunzi wote kufeli kabisa mwaka 2012.
NAJUA PIA KUWA KWA MIAKA MITATUMFULULIZO KUANZ IA 2010 MATOKEO YA FORM 4 YALIKUWA NI MABOVU KUPINDUKIA HASA KWA SABABU YA SHULE ZA KATA.
Najua pia kuwa ni mwaka huu pekee ndio mjadala umekuwa ni mpana zaidi kuliko ilivyokuwa 2010 na 2011.
NA HAPA NITOE MASIKITIKO MAKUBWA KWA SERIKALI KUSHINDWA KULISHUGHULIKIA TATIZO HILI TOKA 2011 KWA SABABU TU WALIOPIGA KELELE KUBWA WALIKUWA WACHACHE AMA WANASIASA HAWAKULISEMA HILI KWA NGUVU KUBWA.
KATIKA UCHUNGUZI WANGU nimegunduwa kuwa bila ya wapinzani kupiga kelele kubwa kwa jambo lolote serikali haioneshi kujali sana.
ILIKUWA NI BAHATI KUBWA NA NIMPONGEZE JAMES MBATIA KWA KULETA HOJA YA UDHAIFU WA ELIMU NA KUFANIKIWA KUIBUA MJADALA MKUBWA KUHUSU UBORA WA ELIMU YETU.
WAKATI AMBAPO MJADALA UKIWA NI MKUBWA KABISA KUHUSU ELIMU(DISCUSION WAS AT THE PEAK) MATOKEO YA FORM FOUR YALITOKA YAKIWA KATIKA HALI MBAYA KIASI CHA KUSEMA KAMA ALIKUWA MGONJWA BASI WANAOMUUGUZA WALIKUWA WAMEKATA TAMAA NA KUPOTEZA MATUMAINI KAMA MGONJWA ANGEPONA NA HAPO NDIPO ILIKUWA NI SAWA NA KUWEKA PETROLI KWENYE MOTO ULIOKUWA MJADALA WA MBATIA NA KILA MTU ALIWEZA KULIZUNGUMZIA HILI KWA NAMNA YAKE NA YA PEKEE.
KWA KIFUPI MADAI NA USHAURI WA MBATIA YALIYOTUPILIWA MBALI NA BUNGE LILILOPUUZA UKWELI YALIPATAUSHAHIDI MKUBWA NA WA WAZI
NA HII NDIO SABABU KUBWA NA PEKEE KUWA KWA MJADALA WA MWAKA HUU KUWA MPANA ZAIDI NA KUJADILIWA NA WATU WENGI ZAIDI NA WENGINE HAWAJUI KUWA NI MIAKA MITATU MFULIZO MATOKEO YALIHITAJI MJADALA NA MUAFAKA KAMA INAVYOTOKEA SASA

KOSA WALILOFANYA SERIKALI .
Serikali haikutoa mwongozo wa mahali gani shule zijengwe ili kurahisisha utatuzi wa matatizo ya huduma za kijamii,kwa taarifa tu mwanafunzi wa kitanzania anaweza akajitahidi kwa kujisomea mwenyewe akishirikiana na wenzake NA AKAFAURU kama atakuwa katika mazingira yafuatayo.
(i)AWE SHULE YA BWENI(BORDING SCHOOL)
(ii)AWE NA UMEME
(iii)AWE NA MAJI
(iv)AWE NA VITBU SAHIHIN NA BORA
NAANDIKA MANENO HAYA NIKIWA NA AKILI TIMAMU NA NIKIWA SHUHUDA WA SHULE ZA SERIKALI NA ANAEBISHA UKWELI HUU AKUSANYE TAKWIMU KWA WANAFUNZI WOTE WALIOSOMA NA KUFAURU KUPITIA SHULE ZA SERIKALI IWE O LEVEL AMA A LEVEL NA JIBU ATAKALOLIPATA NI KWAMBA WALIFAULU KWA KUJISOMEA NA KUFUNDISHANA WENYEWE MANA HATA WALIMU WALIOPO HAWAFUNDISHI KABISA AMA NI WAZEMBE KIASI AMBACHO MSAADA WAO NI SAWA NA HAKUNA.
Sipuuzi walimu ila nilichokiandika ndio ukweli wenyewe na pia sipuuzi nia ya serikali kutatua tatizo la walimu na pia hata kidogo sipuuzi madai ya walimu nchini.
ILA WALIMU PIA WANAHITAJI KUBADILIKA NA KUWA NA MOYO WA KUJITUMA KUFANYA KAZI.

FAIDA KWA MWANAFUNZI KUKAA BOARDING
(i)anaweza kusoma kwa kushirikiana na wenzake ama kupata msaada kirahisi toka kwa wenzake.
(ii)hawezi kupatwa na tatizo la usafri kwa namna yoyote ile na kupelekea usumbufu na uchovu wa safari unaoweza kumzuia kusoma usiku na pia anakwepa tatizo la kuamka mida ya saa 10 adhuhuri kuanza safari na badala yake ataamka mda huo na kuanza kujisomea moja kwa moja
(iii)serikali inakuwa na nafasi nzuri ya kutatua matatizo ya maji na umeme kirahisi kwa sababu wanafunzi wapo sehemu moja na hili linakuwa kivutio hata kwa walimu kukaa kwenye shule yenye huduma za maji na umeme
(iv)ni rahisi sana kuwa handle wanafunzi na kuwafanya wasome na kujisomea na pia wanaepuka mwigiliano wa moja kwa moja na jamii wakati wa shule ama masomo na kupunguza MAAMBUKIZI YA UKIMWI NA MIMBA ZINAZOPELEKEA WANAFUNZI WA KIKE KUACHA SHULE na zaidi wanaondokana na kazi za kila siku za makwao
NASISITIZA KUWA KUZIFANYA SHULE NYINGI NA KARIBIA ZOTE KUWA ZA DAY NI SABABU KUBWA KABISA ILIYOPELEKEA MASSIVE FAILURE TULIYOIONA NA SABABU HII HAIZUNGUMZWI KABISA NA NDIO ILIYONISUKUMA KUANDIKA USHARI WANGU HUU AMA UKOSOAJI WANGU HUU KWA KUZINGATIA HALI HALISI KWANI HATA HATA A LEVEL SHULE ZA SERIKALI HAZIFUNDISHI KABISA AMA KUNA UPUNGUFU MKUBWA WA WALIMU ILA KITU PEKEE KINACHOSAIDIA NI KWAMBA SHULE NYINGI ZA SERIKALI A LEVEL NA KARIBIA ZOTE NI ZA BOARDING.

KUHUSU TATIZO LA WALIMU
JIBU NI FUPI SANA,MSHAHARA HAUTOSHI NA KAMWE TATIZO HILI HALIWEZI KUISHA KWA SABABU SI WOTE WANAENDA KUFUNDISHA BAADA YA KUHITIMU MASOMO YAO HASA WALIMU WENYE DEGREE KWA KUWA WAKIPATA KAZI NYINGINE YENYE MSHAHARA MZURI WANAENDA HUKO,NA AMBAO TAYARI WANAFUNDISHA WENGI WANAACHA KAZI NA KUAJILIWA KWINGINE AMA WANATAMANI KUACHA KAZI PINDI WAKIPATA KAZI YA MSHAHARA MZURI.
KWA ASIYESMINI KUWA TUNA WALIHU WA KUTOSHA HATA KWENYE MASOMO YA SAYANSI BASI SERIKALI ILIJARIBU HATA KWA MWAKA MMOJA KUWEKA MISHAHARA MINONO KUZIBA UPUNGUFU ULIOPO NA WATASHANGAA KUONA WALIMU WANAMIMIKA KUTOKEA KUSIKOJULIKANA MAANA WENGI WATAACHA KAZI HUKO WALIKO NA KUJA KUTAKA KAZI YA UALIMU.
KWA MUHUTASARI MATATIZO YALIYOPELEKEA KUFELI KWA WANAFUNZI NA KUPOROMOKA KWA ELIMU YETU.
(i)shule kuwa za day
Kosa nililolieleza kuwa serikali ilikosea kushindwa kutoa mwongozo kuwa shule zijengwe katika mazingira gani,nilimaanisha shule zingejengwa katika maeneo yenye maji karibu ama yenye uwezekano wa kupata maji karibu na yenye uwekano wa kupata nishati ya umeme kirahisi.ISIPOKUWA KWA maeneo AMBAYO UWEZEKANO HUO HAUKUWEPO KABISA.MAANA SHULE NYINGI KUTOKANA NA MAENEO ZILIPOJENGWA ZITAENDELEA KUWA NA MATATIZO YA MAJI NA UMEME HATA BAADA YA MIAKA 6O
(ii)upungufu mkubwa wa walimu
(iii)uzembe wa walimu ambao inawezekana kuwa unatokana na mishahara kuwa midogo kiasi cha walimu wengi kutothamini kazi yao,na kupelekea kutofundisha kabisa ama kufundisha kwa namna wanavyojisikia
(iv)upungufu mkubwa wa vitabu bora na vizuri na uwepo wa vitabu vibovu vingi visivyokidhi kiwango stahiki ikiwa ni pamoja na vitabu vya serikali na watu binafisi
(v)upungufu wa vifaa vya kujifunzia ikiwa ni pamoja na maabara
(vi)kukosekana kwa mwongozo wa kudumu kwa elimu mfano kuondoa mtihani wa form two ilikuwa impact mbaya sana mana si tu wanafunzi wengi wabovu walipita bila kuchujwa bali pia mtihani huo ulikuwa unawapa hofu wanafunzi na waliutumia kuhakikisha wana clear mapungufu yote waliyokuwa nayo katika form one and form two,kama kuna topic hawakuisoma walijitahidi wakaisoma,KWA SABABU HII WANAFUNZI WALISOMA MIAKA MITATU MFULULIZO BILA KUWA NA HOFU YOYOTE NA WALIANZA HOFU MWAKA WA NNE WAKIWA NA MADENI NA MAPUNGUFU MENGI AMBAYO KWA NAMNA YOYOTE WASINGEWEZA KUFANYA GENERAL AND CLEAR STUDY KWA KU-COVER MAMBO YOTE WALIYOYARUNDIKA KWA MIAKA MITATU NA HUKU YALE YA FORM FOUR YANAWASUBIRIA(there was no way out to survive from massive failure) na TATIZO WALILOLIELEZA NECTA KUWA WANAFUNZI WOTE KATIKA BAADHI YA SHULE HAWAKUJAZA CHOCHOTE KATIKA SOMO LA BIOLOGY KISA HAWAKUWAHI KUFUNDISHWA KABISA WANGEWEZA KULIGUNDUA MAPEMA KWENYE MTIHANI WA FORM TWO MANA HATA PALE WASINGEANDIKA CHOCHOTE KWA SABABU HAWAKUWA WAMESOMA CHOCHOTE NA SERIKALI INGECHUKUA HATUA ZA DHARURA NA HARAKA MAPEMA
(vi)kushindwa kwa EMAC kusimamia kazi yake na kutoa vibali kutumika kwa vitabu vibovu ikiwa ni pamoja na vya watu binafisi na vya serikali(TUHUMA ZA RUSHWA AMA UZEMBE WA KUPINDUKIA ZINAZOPELEKEA KUTOLEWA KWA VIBALI BILA KUZINGATIA UBORA),na inashangaza kuona kitabu chenye nembo ya EMAC KIKIWA NA MAPUNGUFU YASIYOSTAHIMILIKA KIASI CHA KURUHUSIWA KUTUMIKA

"KUJUA TATIZO NI NUSU YA JAWABU"BY PRESDENT KIKWETE
KWA MUKUTADHA HUU SITATOA USHAURI NINI KIFANYIKE ILA NI RAHISI KUJUA NINI CHA KUFANYA KUTOKANA NA MATATIZO NILIYOYAELEZA.

PIA NITUMIE MDA HUU KWA UFUPI KUELEZA KUWA MABADILIKO YASIFANYWE NA KUTEKELEZWA KWA HARAKA KAMA ILIVYOKUWA WAKATI WA KUUNGANISHA PHYSICS NA CHEMISTRY,KUFUTWA KINYEMELA KWA BAADHI YA MASOMO NA HLI LILINIATHIRI MAANA SHULE YANGU HAUKUTAKA KUMLIPA TENA MWALIMU WANGU WA AGRICULTURE MAANA HAIKUONA TENA UMUHIMU WA SOMO LILE NA ILIBIDI WANAFUNZI WOTE TUACHE KUSOMA AGRICULTURE TUKIWA FORM THREE JAPO TULIPENDA KULISOMA NA WENGINE SOMO LILE LILIBEBA NDOTO ZAO NA KIMSINGI HAPO NDIO ILIKUWA MWISHO WA NDOTO ZAO NA SERIKALI ILIFANYA HILI BILA YA KUPATA MAONI YA WADAU HASA WALIMU NA WANAFUNZI.

PIA SERIKALI IMEKUWA IKIWAACHA KATIKA DILEMA WANAFUNZI WASIJUE LA KUFANYA KIPINDI IMECHELEWA SANA,mfano wanafunzi wa form six waliohitimu 2012 hawakujua wangeenda kufanya mtihani kwa format ipi kati ya ile ya zamani ama mpya iliyotolewa na serikali na mpaka dakika za mwisho hawakujua NA HILI NI TATIZO KUBWA na hata wanafunzi wa waliohitimu mwaka huu form six 2013 hawakujua kama wangemaliza mwezi wa pili ama wa tano kufatia mabadiliko yaliyofanywa na serikali na hakukutolewa taarifa ambayo ingewaweka wazi mana walisumbuliwa na rumours nyingi na mimi ni shahidi nilipigiwa simu na wanafunzi mbalimbali marafiki zangu waliokuwa shule mbalimbali wakiniuliza na mimi sikujua la kuwaambia wala sikupata taarifa sahihi ambazo ningewajibu

Mawasiliano mabovu kati ya NECTA ,WIZARA YA ELIMU NA IDARA ZA EMAC NA ILE INAYOHUSIKA NA KUTUNGA VITABU VYA SERIKALI PIA NI TATIZO LINALOPELEKEA KUTUNGWA KWA MASWALI NJE YA MITAALA JAPO HILI SI KUBWA SANA ILA NALO LIPO.

TATIZO KUHUSU LUGHA YA KUFUNDISHIA
Kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusu lugha ya kufundishia.
Wengine wakidai lugha ya kiingeleza ndio iendelee kutumika na wengine wakidai lugha ya Kiswahili ndio iwe lugha ya kufundishia kwa ngazi zote kama ilivyo ama ilivyowahi kuwa mjadala katika matumizi ya lugha bungeni na uchanganyaji wa maneno mengi ya kiingeleza hasa wabunge wanapochangia hoja mbalimbali kiasi cha wananchi kulalamika kuwa huwa hawaelewi hasa wakati ule ambapo miiswaada mingi ilikuwa inaletwa kwa lugha ya kiingeleza na kupelekea chuo kikuu cha dare es salaam(1995 kama kumbukumbu zangu ziko sahihi)kufanya utafiti wa matumizi ya Kiswahili bungeni na kwenye baraza la wawakilishi .
YAFUTAYO NI MAONI YANGU
NAKUBALIANA NA WENGI KUWA LUGHA YA KUFUNDISHIA NI TATIZO LINALOWEZA KUMFANYA MWANAFUNZI AFELI MTIHANI KWA KUSHINDWA KUJIELEZA VIZURI HATA KAMA MAJIBU ANAYAJUA.
Lakini napingana na wadau wa Kiswahili na wale wote wanaosema lugha ndio chanzo kikubwa kabisa kufelisha wanafunzi.
Maswali ya kujiuliza
1.kwa nini hata somo lenyewe la Kiswahili linalofundishwa kwa Kiswahili wanafunzi wengi wanafeli ama wanafaulu kwa ule ufaulu wa alama za chini yaani D?
2.Kwa nini shule ya msingi mahala kunakofundishwa masomo yote kwa Kiswahili ukitoa kiingeleza wanafunzi wanaufaulu mdogo ulio chini ya asilimia 60% wakati kwa mfano nchi ya Uganda imefaulisha wanafunzi wake kwa asilimia 88%?
3.kwani wakati ambapo serikali ilifikia kiwango kikubwa cha kufaulisha wanafunzi wa sekondari huko nyuma walikuwa wanatumia lugha tofauti na kiingeleza?kwa nini ishindikane sasa kufaulisha wanafunzi kwa lugha ile ile iliyowahi kuzaa matunda?
4.kama serikali imeshindwa kutunga na kusambaza vitabu kwa ubora na wakati unaotakiwa hata kwa somo hilo la Kiswahili je itakuwaje rahisi kwa nchi kujitegemea kutunga vitabu vyake yenyewe katika mazingira ya sasa ambapo kila kitu kinabadilika kwa kasi na kila baada ya mda mfupi?tena kuanzia darasa la kwanza mpaka chuo kikuu
5.mamlaka zetu za usimamizi wa utungaji wa vitabu ndio kama EMAC ilivyo sasa je hii inaleta picha gani kama vitabu vyote vitahakikiwa na EMAC?tofauti na ilivyo sasa ambapo vitabu vingi vya sayansi HASA A LEVEL NI VYA NJE?
MSIMAMO WANGU KWA MAZINGIRA TULINAYO LUGHA YA KUFUNDISHIA SIO TATIZO KAMA WENGI WANAVYOLIPIGIA KELELE
Hivi hatujiulizi kwa nini wazee wa waliosoma zamani walimudu kutumia lugha hii na ushadi upo maana mpaka sasa wazee wengi hata walioishia la nne na la nane wanakimudu sawasawa kiingeleza?na hata wanafunzi wengi wanaohitimu sasa form four ama form six wanauwezo kidogo wa kuongea kimombo ukilinganisha na wale wazee wa la nne na la nane la zamani.
UKWELI NI KUWA WALIMU WAMESHINDWA KUWAANDAA WANAFUNZI KUKIJUA KIINGELEZA KAMA WALIVYOSHINDWA KATIKA MAENEO MENGINE KAMA NILIVYOOLEZA KUHUSU SABABU ZA WANAFUNZI KUFELI.
NA USHAHIDI WA HILI NI KWAMBA HATA KISWAHILI CHENYEWE KINACHOTUMIKA SANA SI FASAHA AMA KILE CHA KUFUNDISHWA NA HILI NDIO USHAHIDI KUWA HATA KISWAHILI KINACHOPIGIWA UPATU SI KIRAHISI AMA HAKIELEWEKI KILAHISI KAMA INAVYODAIWA.
Ushahidi mwingine ni hata ndani ya ukumbu wa bunge,wabunge wengi wanatumia maneno ya mtaani zaidi na si Kiswahili fasaha na hata uchunguzi/utafiti uliofanywa na UDSM miaka ya tisini ulibainisha haya.
6.mbona kuna watanzania walipelekwa kusoma na bado wanapelekwa kusoma nchi kama URUSI,CHINA,UJERUMANI,UARABUNI NK LAKINI BADO WANAMUDU AMA WALIMUDU KUSOMA.
Japo hapa nisiwe mzunguzaji sana maana muliosoma nje mpo naomba msaada na ushuhuda wenu kwa hili mutueleze mliwezaje kuhilimi lugha za kichina na kirusi kwa mfano,LETICIA NYERERE(MB) NAJUA ULIKUWA URUSI KAMA NILIVYOKUSIKIA UKISEMA MWENYEWE BUNGENI PAMOJA NA WOTE ULIOWATAJA NAOMBA MCHANGIE KUHUSU LUGHA HUKO URUSI,CHINA NK.

HOFU YANGU KAMA TUKIAMUA KUTUMIA KISWAHILI KAMA LUGHA YA KUFUNDISHIA KILA MAHALI KAMA ALIVYOWAHI KUPENDEKEZA MHESHIMIWA (MB) TUNDU ANTIPUS MUGHWAI LISU.
Nchi yetu pamoja na wasomi waliopo hawafanyi tafiti ama wanafanya katika kiwango kidogo sana na hata hatuna chombo kinachoratibu tafiti zote nchi nzima na ushahidi ni kwamba hata machapisho ya tafiti nyingi hatuoni na hata watafiti binafsi hawaandiki vitabu na hili nina uhakika nalo.
Na kwa hali hii Napata picha kwamba hata elimu na technology yetu ni tegemezi ama inategemea nini kinaendelea huko nje na kamwe haitegemei tafiti zetu za ndani.hapa kitakachotokea ni kwamba tutatumia Kiswahili huku tukisubiri wakati wote kila kutakapo kuwa na uvumbuzi mpya basi tuwe tayari kutafisri na kutohoa maneno maana watu wetu hawataweza tena kupa update za moja kwa moja kama tunavyofanya sasa maana watakuwa hawajui hata punje ya kiingeleza.
NA HAPO NDIPO TANZANIA ITAKOSA HATA FURSA NYINGI ZA AJIRA MAANA VIFAA TUNAVYOTUMIA NI MADE FROM ABROARD TOFAUTI NA NCHI KAMA CHINA AMBAYO INAANDIKA VIFAA VYAKE KICHINA NA WATU WOTE WANAILEWA.
USHAHIDI ULIOPO MPAKA SASA NCHI YA KENYA RAIA WAKE WAMEPATA AJIRA HAPA NCHINI KATIKA SEKITA ZA UTALII NA HOTELI NA HATA KAZI ZINGINE KWA SABABU YA KUJUA KIINGELEZA TU,BAADA YA KUANZA KUTUMIKA KISWAHILI NA KUZIKA RASMI KIINGELEZA SIPATI PICHA YAKE MAANA HATA MOJA YA MAKAMPUNI YALIWEKEZA KWENYE UCHIMBAJI WA DHAHABU LILIWAHI/LINAAJILI KWA KIGEZO PIA CHA KUJUA KIMOMBO ILI KURAHISISHA MAWASILIANO NA INTERVIEW YA MWISHO MWAKA FULANI ILIKUWA NI KUPEWA MDA MCHACHE WA KUZUNGUMZA NA MZUNGU NA KAMA UKISHINDWA KUONGEA KIMOMBO BASI UMEKOSA KAZI MANA WALE HAWAWEZI KUHITAJI MKALIMANI KILA MAHALI.
MWISHO HATA KISWALI CHENYEWE KWA KIASI KIKUBWA WANAFUNZI WANAANZA KUJIFUNZA NA KUKIONGEA WANAPOANZA SHULE NA HATA MIMI SIKUJUA KABISA KISWAHILI MPAKA NILIPOANZA LA KWANZA NA LUGHA NILIYOKUWA NATUMIA NI LUGHA YA NYUMBANI(MOTHER TONGUE NA HUU NDIO UTAMADUNI WANGU HASA MAANA NDIO LUGHA NILIYOKUWA NAIZUNGUMZA TOKA NILIPOANZA KUONGEA) LAINI BAADAE NILIWEZA KUONGEZA LUGHA ZINGINE MBILI KUPITIA DARASANI YAANI KISWAHILI NA KIINGELEZA.
7.we can't translate everything in the field of history and science whatsoever happened before creating a closed room for learnig to our people where they will lack the search of the supplement materials as we can easly do now
Kama nilielewa Kiswahili kupitia darasani nilipashwa pia kuelewa kiingeleza kupitia darasani.

DHANA YA VIBOKO MASHULENI
Swala la viboko kama sababu sikubaliani nalo na wala hakuna ushadi wa wazi kuwa linasaidia.walimu wengi wanatumia vibaya fimbo na inajenga mazingira makubwa ya uoga kati ya mwalimu na mwanafunzi na wale walimu wasiomudu vyema kufundisha hutumia fimbo kama ngao yao na kupelekea wanafunzi wengi kumuchukia mwalimu na somo lenyewe na mwisho wake wote wanafeli.KUNA USHAHIDI WA WAZI KUWA WANAFUNZI WAKIMPENDA MWALIMU HATA SOMO LAKE HULIPENDA NA KUONGEZA ARI YA KULISOMA NA UPANDE MWINGI NE WANAFUNZI WAKIMCHUKIA MWALIMU HATA SOMO LAKE WANALICHUKIA NA MWISHO WA SIKU WANAFELI.nakumbuka primary mwalimu wangu wa hesabu alikuwa mkali na viboko vilikuwa kawaida na kila alipoingia kwanza darasa zima linakosa raha na unaomba mungu asikuulize swali maana ukikosea unazioga fimbo na kimsingi ilikuwa haiwezekani ku concentrate zaidi ya hofu.PIA O LEVEL NILISOMA SHULE ISIYORUHUSU MATUMIZI YA AINA YOYOTE YA FIMBO NA HAKUNA MAHALA AMBAPO MAMBO YALIENDA MLAMA NA SHULE ILIKUWA NZURI SANA NA HADI LEO WAMEENDESHA SHULE VIZURI KABISA KWA ZAIDI YA MIAKA 18 NA WANAFUNZI WANAJISIKIA FARAJA KWA HILI NA WAPO VERY CONFORTABLE.na kama fimbo ndo ingekuwa sababu ya kufaulisha sijui shule hii ingekuwa wapi ila nadhani wangeshaifunga maana ingekuwa inapata matokeo ya ajabu na watu wangeacha kwenda pale.

MATOKEO YA FORM FOUR 2012.
MWISHO SIKUBALIANI NA HATUA YA SERIKALI KUFUTA NA KUPANGA UPYA MATOKEO YA FORM FOUR 2012.
RAI YANGU SERIKALI IPIME SABABU NYINGI ZILIZOPELEKEA WANAFUNZI KUFELI KWA KIWANGO HIKI KULINGANA NA ZILIVYOTOLEWA NA ZINAVYOTOLEWA NA WANANCHI,WAHUSIKA NA WAALIMU NA ITATUE TATIZO LA MSINGI.
Maana siwezi kushawishika hata kidogo kuwa mitihani ikisahishwa ama kuwa graded upya matatizo ya vitabu,walimu,umeme,maji,ukosefu wa mabweni nk YATAKUWA YAMEONDOKA.
PIA BADO SIPATI MAJIBU NI KWA NAMNA GANI WALE WANAFUNZI AMBAO HAWAKUJAZA CHOCHOTE KWENYE SOMO LA BIOLOGY WATANUFAIKA NA KUYAPANGA UPYA MATOKEO HAYA?labda nikieleweshwa nitaelewa ila najua hili halina msaada kwao.
Nawasilisha

0683 783379(MWANAFUNZI)

09/05/2013
 
Mbona na nyinyi mnakuwa wagumu kuelewa mbona serikali imejieleza wazi wazi kwamba imefuta kutokana na njia iliyotumika kupanga grade kuwa tofauti na ile ya siku zote sasa hapo tatizo linakuwa wapi!Pia wakasema njia mpya iliyotumika kupanga grade wadau wa elimu hawakushirikishwa ktk kuichagua.Walifafanua zaidi kwamba matatizo mengine yatatatuliwa taratibu ila kwa sasa suluhisho la haraka ni kupanga grade kwa njia iliyozoeleka.Ningefurahi kama mngehoji kwamba kwa nini Ndalichako (Katibu wa baraza la Mitihani) aliamua kutangaza matokeo bila hata kufanya Standardization wakati inakubalika ktk elimu hadi vyuo vikuu!Mnataka zile zero zote zibaki mtaani ili mfurahi harafu mnasema mnatutakia mema kweli?Hivi mnajua hata wanafunzi waliokuwa wanasoma shule za seminary kwenye facility zote mnazotaja nao wamefeli kutokana na njia mpya ya grading?Mimi binafsi naipongeza Serikali kwa uamuzi walioufanya cha Msingi wawe serious na waendeleee kuwabana Mafisadi ili fedha zilizopangwa ktk sekta mbalimbali ziwafikie walengwa.Pia wahakikishe kila anayestahili kulipa kodi na afanye hivyo kwa kupinga rushwa, undugu ktk ajira ili watu wanaopatikana wawe wachapa kazi ili kuokoa sekta mbalimbali siyo elimu pekee.
 
Mimi sio mgumu kuelewa ila pengine hujasoma kwa makini.
NIMEANDIKA MATOKEO YALIKUWA MABAYA KIASI HIKI 2010 NA 2011.
SASA NA HAPO ILIKUWA GRADING?Ama serikali wanataka kutuaminisha kuwa matatizo wanayoyapigia kelele watanzania si sababu zaidi ya hiyo ya grading.
NO WAY,ama hujui matokea ya miaka mitatu mfululizo?kuna mtu hajaandika chochote unagrade nini?
 
Back
Top Bottom