Mastaa ‘chapombe’


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,977
Likes
5,350
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,977 5,350 280
risasi mchanganyiko
pix.gif
1267600760_chapombe.jpg


Tabaka la mastaa nchini, linaendelea kukabiliwa na aina ya watu wapenda starehe, wanaotumia muda wao mwingi wa usiku viwanja na asubuhi wakiipitisha usingizini, katika aya zinazofuata Risasi Mchanganyiko lina 'spesho kesi' kuhusu watu maarufu na pirika zao za 'naiti kali' pamoja na masanga...
Katika habari hii, gazeti hili ambalo hadhi yake ni nyota tano kwa habari za mastaa, limekusanya picha za watu maarufu katika matukio tofauti ya usiku ambayo walinaswa wakibugia maji yaingizayo kilevi mwilini.

Hata hivyo, kati ya matukio hayo ni moja tu la msanii Juma Kassim Ali Kiroboto ‘Sir Nature’ ndilo lililochukuliwa mchana lakini mengine yote yalifanyika usiku.
Mastaa hao na maelezo kuhusu picha zao ni kama ifuatavyo;
Juma Nature

Alipigwa picha akiwa na chupa yenye maji ya kilevi, mchana wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka juzi. Habari ya msanii huyo kuhusu tukio hilo, iliripotiwa na magazeti ya Global Publishers (Ijumaa Wikienda na Amani).
Hadija Shaibu ‘Dida’

Akiwa ameshikilia kopo mbili za maji yenye kilevi, ‘alikong’otwa’ picha na paparazi wetu katika moja ya matukio ya usiku kwenye Ukumbi wa Travertine, Magomeni, Dar es Salaam.

Usiku huo, ndani ya ukumbi huo kulikuwa na ‘shoo’ kali kutoka kwa Kundi la Jahazi Modern Taarab, hivyo Dida akiwa kama mwana-mipasho wa ‘levo’ ya juu Bongo, alihudhuria lakini akaona mirindimo bila kilevi ‘stimu’ hazipandi.
Mr. Nice Lucas Nkenda

Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, Dar es Salaam ukiwa umefurika watu katika usiku mmoja hivi, paparazi wetu alimnasa Mr. Nice akibugia maji ya ‘bruarizi’ lakini katika kuonesha kwamba ile si bahati mbaya, msanii huyo alisema kwamba pombe ndiye mke wake mpya.

“Sina faraja nyingine zaidi ya pombe, kwahiyo ukiniona nimeshika chupa kama hivi, ujue ndiyo nipo na my wife, tumeelewana?” Alisema Mr. Nice kwa mtindo wa kuhoji.

Jacqueline Pentezel
Paparazi wetu alimnasa kwenye harusi ya msanii mwenzake wa filamu nchini, Irene Uwoya, Julai, mwaka jana akibugia kinywaji bila hofu tena akionesha utulivu wa kiwango cha juu kudhihirisha kwamba ni starehe ambayo siyo tu anaipenda bali pia anaiheshimu.

Hashim Kambi ‘Wingo’
Kama ilivyo kwa Jacqueline, naye alifumwa akichapa maji kwenye harusi ya staa wa filamu Bongo, Irene Uwoya Julai, mwaka jana katika hali ya utulivu kuonesha kwamba koo lake limezoea kupitisha aina hiyo kimiminika.
Jumanne Kihangala ‘Mr. Chuz’

Yeye ni mnywaji mzuri lakini ushahidi ulipatikana kwenye harusi ya Irene Uwoya baada ya kugongwa picha ya mnato akiwa ‘vere bize’ akikamata ‘masanga’ Julai, mwaka jana.

Aunt Ezekiel
Naye siyo tu kwamba ni staa wa filamu bali pia kwenye ‘kilaji’ naye yumo. Picha yake ambayo ‘alikong’otwa’ mwaka jana inathibitisha jinsi alivyo hodari katika ‘kufakamia’ maji yenye kilevi.
 
Sumbalawinyo

Sumbalawinyo

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2009
Messages
1,285
Likes
26
Points
0
Sumbalawinyo

Sumbalawinyo

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2009
1,285 26 0
Udaku wa nini??
Je hii habari ya kuchunguza maisha ya watu inatusaidia nini sisi?
Umeleta mapungufu ya watu, mbona mapungufu yako hujayaweka hadharani?
Au wewe umekamilika?
Tunaomba ujirekebishe, mambo ya ngoswe mwachie ngoswe mwenyewe.
 
Soulbrother

Soulbrother

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2009
Messages
408
Likes
4
Points
35
Soulbrother

Soulbrother

JF-Expert Member
Joined Apr 14, 2009
408 4 35
kwani MziziMkavu kaajiriwa na Risasi kuwauzia magazeti JF?

ungeweka link sio ukurasa wote wa risasi hapa.
 

Forum statistics

Threads 1,237,663
Members 475,675
Posts 29,296,562