Masoud kipanya asimulia jinsi alivyotimuliwa kazi cloudz fm

Issue ilivyotokea walienda kufanya kipindi na Balozi wa US ofisini kwake,.
wakati wanafanya kipindi Mic zilikuwa zinazingua kwa hiyf kipindi hakikufanyika fresh,.
Kwa kuwa tatizo kama hilo lilishatokea mara kadhaa ikawa imewa pain wakaona waonyeshe kukwazwa kwao kwa kutoenda kazini..
wakakubaliana yeye, Fina Mango na G. Hando kesho yake wasiende kwenye kipindi..
Cha ajabu kesho yake Hando akawasaliti akaenda, wao wakaambiwa waandike barua ya kujieleza, Wakaandika issue ilivyokuwa lakini baada ya ka siku nne wakafukuzwa


Nadhani hapa sheria mpya ya kazi haikuwa implemented haiwezekani mfanyakazi ajieleze kwa barua then unamfukuza ndani ya siku nne!nadhani idara ya rasilimali watu hapo clouds imeshindwa kazi au imekufa kabisa,namshauri masoud aende CMA kufile kesi maana kama hayo maelezo hapo ni ya kweli moja kwa moja hii ni unfair termination.sheria zipo tuache kulalamika kwenye vyombo vya habari wakati nchi yetu inaendeshwa kwa sheria na katiba.rules of law
 
matope yako kwenye visigino au mpaka ubongoni? sasa kama yeye ame quote alichosema kipanya hizo sababu atatoa wapi kama kipanya hakubainisha vizuri!? na wala si yeye aliekuwa akimhoji!

ina maana huo mpangilio hapo juu unauona ni sahihi. Kipanya hawezi kutoa habari kama hiyo.
 
Haya ni mahojiano ya KP na BC
BC: KP,kwa muda wa wiki kadhaa sasa kumekuwepo na tetesi,minong’ono,udaku nk kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwenu katika kipindi chenu maarufu cha PowerBreakfast kupitia CloudsFM.Hivi leo,blog ya Michuzi(bila shaka umesoma kilichoandikwa) iliweka kidogo kuhusiana na kilichokuwa kinazungumzwa mitaani. Je ukweli uko wapi? Upo au haupo tena katika PowerBreakfast?Nini kimetokea?

Nae akafunguka namna hii.....msome na ubishi uishe


KP: Nimepata bahati ya kusoma blog ya Michuzi muda mfupi uliopita na nimeona taarifa pamoja na maoni mbalimbali ya wadau. Pengine bila ya kutoa ufafanuzi, watu wataendelea kuongea mambo ambayo hayapo kabisa. Ukweli ni huu ufuatao; Nitajizungumzia zaidi mimi kwa vile ishu yetu na Fina ni moja ila maamuzi yanatofautiana kidogo na yanatofautiana si kwa sababu ya upendeleo, la hasha, nataka kuamini ni kwa sababu ya aina ya mikataba tuliyokuwa nayo.Wa kwangu ulikwisha February 28 mwaka huu ingawa nilishaanza kuutumikia mkataba mpya wa miaka miwili, wa Fina unakwisha nadhani mwishoni mwa mwaka huu(sina uhakika)

Mimi sikuacha kazi Clouds Fm kama inavyosemekana, mimi nimepewa barua ambayo inazungumzia ku-revoke (kutengua,kuahirisha) mkataba wangu na Clouds.Nitazungumzia sababu za kupewa barua hiyo, ila kabla sijaingia ndani zaidi, mwisho wa barua ile niliyopewa imesema, nainukuu, ‘we wish you all the best in your future endeavors’ mwisho wa kuinuukuu barua niliyopewa na HR Manager wa Clouds Media Group. kwa lugha rahisi ikimaanaisha tunakutakia kila la heri katika mahangaiko yako ya mbeleni.

Kwa mantiki hiyo labda wasomaji waniambie sijaielewa maana ya barua ile, lakini kwa kifupi nilichoelewa ni kwamba, kutokana na makosa niliyoyafanya, Clouds imeonelea kuwa sina sifa za kuendelea kuwa sehemu ya timu ya Clouds Fm. Sasa basi, hebu tuangalie makosa niliyoyafanya mimi pamoja na Fina.

Tarehe 29th May 2008, kwa pamoja, mimi na Fina tuliamua tusiingie kwenye kipindi kuonyesha kutoridhishwa na utendaji wa baadhi ya wenzetu. Kama kuna waliosikia, siku moja kabla yaani tarehe 28th May tulifanya mahojiano na Balozi wa Marekani nchini Tanzania.Bahati mbaya (kwa sababu ambazo zilikuwa ndani ya uwezo wa Technical Department) mahojiano yale hayakusikika vizuri, yalisikika vibaya mno!!! Na hata vifaa pia havikuwa timilifu, mfano mmoja mdogo tu ni kwamba tulikuwa tunatumia mic moja.Yaani watangazaji watatu na balozi, kwangu ilinipa wakati mgumu sana hasa ikizingatiwa taarifa za interview zilipatikana karibu wiki nzima.Nilitegemea wenzetu wangejiandaa kwa kila kitu. Kwa kifupi watu wa technical walikuwa na uwezo wa kusema kwamba interview isingewezekana kutokana na ufinyu wa signal na vifaa, TUNGEAHIRISHA.Makosa kama haya yamekuwa yakijirudiarudia mara kwa mara na ndio maana nasi tukaamua kuweka msisitizo kwa njia ile ya kugoma.

Najua kuna watakaojiuliza, hapa Gerald anaingia wapi, kwa sababu alisikika wakati wa mahojiano na balozi, akayapata madhira lakini hakugoma. Hilo sitolitolea maelezo nikiamini yeye mwenyewe ndiye mwenye nafasi nzuri ya kufafanua atakapotakiwa kufanya hivyo ingawa halazimiki. Ila ieleweke kwamba, kwenye mpango wa kugoma, ALIHUSISHWA NA AKAUKUBALI.

Kilichofuatia ni kutakiwa tujielezee kwa nini hatukwenda kwenye kipindi, tukajielezea, na hatimaye mimi nikapewa barua niliyoielezea hapo juu na tetesi za uhakika nilizo nazo ni kwamba mtu wa technical kapewa barua ya warning.

Kwa hiyo basi, kuondolewa kwangu hakuhusiani kabisa na suala la masilahi yaani mishahara. Kosa ni hilo hapo juu na tulilifanya kwa nia njema ya kujaribu kujenga zaidi kwa vile tunaamini Clouds inazidi kukua siku hadi siku.

Ni juu ya atakayesoma waraka huu kupima uzito wa kosa na uzito wa adhabu.Kwangu naona sawa kwa sababu si kila kinachotokea lazima kiwe na sababu za msingi. Bado mwenye mali ana mamlaka ya kuamua nani awe kwenye timu na nani asiwemo.Na ninaamini kila anayekosea lazima aadhibiwe,nami nimeadhibiwa na nimeheshimu. Maisha yanaendelea.

Namshukuru mungu na nawahakikishia wachache waliokuwa wakitusikiliza kwamba kamwe hatukuwahi kulewa sifa kwa sababu kama ni kulewa sifa tungeshagoma siku nyingi zilizopita kama suala lingekuwa ni mshahara. Kwa wenye kumbukumbu, Power Breakfast ilianza kama ‘wake up show’, enzi hizo kipindi kilikuwa kinaanza saa 11 alfajiri, maana yake ni kwamba mimi na Fina tulikuwa tunaamka saa 10 alfajiri, kwa mshahara wa kawaida kabisa na bado tuliweza kulibeba jahazi.

Akaendelea kufunga namna hii......

Mwisho kabisa nawaomba radhi wale ntakaokuwa nimewakwaza kwa kuyaanika haya, ila kwangu ni kwa faida zaidi kwani ninapochora katuni nategemea wasomaji zaidi ambao ni watu, na ninapokuwa mmachinga wa nguo nategemea watu pia.Hivyo basi bila UFAFANUZI ni rahisi kwa watu hao ambao ni wasomaji wa katuni na wanunuzi wa nguo zangu kunishusha thamani kwa kudhani tumeacha Clouds kutokana na kudhani tumeshakuwa wakubwa hivyo basi tumeanza kuringa. LA HASHA!!!SIKUACHA CLOUDS, NIMETIMULIWA (nahofia kuuzungumzia mkataba wa Fina kwa kuwa una mambo yake haswa upande wa kisheria) NA SIJAPATA KAZI,ILA NINATAFUTA KAZI ILI WANANGU WAENDELEE KWENDA CHOONI. WALA SIJACHUKULIWA NA TBC, KWANZA UTUKUFU WALIONAO ZE COMEDY HATA ROBO SIJAUFIKIA

 
AKIONGEA KWENYE KIPINDI KINACHOÖNESHWA (kinachoonyeshwa) NA EATV, (please weka koma hapa) NA SALAMA JABIL KWENYE KIPINDI CHAKE CHA MKASI.(spacing)MASOD ANASEMA LICHA YA KUFANYA KAZ (kazi) KWA MIAKA 9 HUKU AKILAZMIKA(akilazimika) KUAMKA MAPEMA ALFAJIRI (alfajiri na mapema) BADALA YA KWENDA MSIKTIN (msikitini)ALIKWENDA KWENYE KIPINDI HUKU MASILAHI (maslahi) YAKIWA DUNI AKAJAFUKUZWA(kinyakyusa hiki hatukitaki) KAZI KWA SIKU MOJA TENA HUKU KOSA LIKIWA NI LA MAFUNDI MITAMBO.(spacing please)AKIELEZEA KWA MASIKTIKO ANASEMA ALIFUKUZWA KAZI KWA KOSA LISILO LAKE TENA KWA Siku moja!

okey who posted this??????
 
Wana JF,
Hatuna sababu ya kugombania fito wakati tunajenga nyumba moja.
Muandaaji wa kipindi, Salama alitaka ampe nafasi Masoud Kipanya ili aeleze ukweli juu ya kuachishwa kazi Clouds.
Pia msanii masoud apate muda muafaka wa kutujulisha kuwa DVD za upuuzi wa Masoud Kipanya kwa sasa zipo
tayari tusubiri kupata vipande vya keki 26.
Tunamwambia tupo tayari tunaisubiri hiyo DVD 7babu tunaelewa Masoud ni nani na kazi zake zinakubalika.
 
Mi nadhani tusipende kurumbana sana jamani napenda sana hii forum ya Great thinker, jana niliona kipindi vizuri sana alichokua anajaribu ni kusimulia ni jinsi gani alivyoachizwa kazi.Ni kweli ni kutokana na uzembe wa technician wale walioko behind the scene walikubaliana na wagome ila Hando akawageuka akaenda kwa kazi.Jamani haya mambo yapo kwenye jamii yoyote ile kwamba hamuwezi kugoma wote lazima kuna mmmoja atakuwa msaliti sana tu.Jamaa ilimuuma sana na sisi kama binadamu wa kawaida ni kweli lazma ikuume hata ungekuwa wewe kufukuzwa kazi kiholela tuu.Kweli jamaa nimempenda coz ni mchapa kazi sana and very creativity jamani.muacheni tu kwani huyo Hando yuko wapi...
 
Maelezo yako yana utata mkubwa sana unamaanisha nini kusema alifukuzwa kwa kosa la mafundi mitambo bila kueleza kosa lenyewe?????

Kama huna data si lazima kupost tread iliyojaa upupu kwenye jukwaa la Great thinkers.

Unabahati nimekujibunsidhani kama kuna mtu atajibu huu upupu wako

Shame on Uuuuuuuu.

Acha ukali usio na maana wewe! Great Thinker gani wewe unashindwa hata kuhariri maneno yako? Hebu angalia utumbo ulioandika hapo kwenye red!
 
Masoud kumbuka you were not born to work at Clouds forever.
Najua una kichwa cha ujasiria mali na kuna project tulishawai fanya nawe.
Acha kulaumu the past pambana na the currrent ili future yako iwe njema kwako na kwa familia yako.
Ulikuwa mpango wa mda mrefu wa kukutimua pale!
 
Maelezo yako yana utata mkubwa sana unamaanisha nini kusema alifukuzwa kwa kosa la mafundi mitambo bila kueleza kosa lenyewe?????

Kama huna data si lazima kupost tread iliyojaa upupu kwenye jukwaa la Great thinkers.

Unabahati nimekujibunsidhani kama kuna mtu atajibu huu upupu wako

Shame on Uuuuuuuu.
we matope kweli! inaonekana wakati una-post huu utumbo wako mshahara ulikuwa haujaingia eeh?
 
Back
Top Bottom