Simulizi za Othman Masoud

aleesha

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
776
1,121
Yaliyojiri ndani ya Bunge la Katiba na kulichopelekea kufukuzwa kwake.

Alichomwambia Dr. Shein baada ya kupora Ushindi wa Maalim Seif.

Maisha yake nje ya harakati.

Ukaribu wake na watu.

Anavyowajali Wazanzibari.

Simulizi hii ni sehemu ya pili ya muendelezo wa simulizi za Othman Masoud, (Makamu wa Kwanza wa Rais mteule) ambazo zinaonyesha kwa kiwango kikubwa zaidi umahiri wake, msimamo wake, mapenzi yake kwa Zanzibar na namna asivyoyumba kusimamia Maslahi ya Wazanzibari.

Kisa hiki kinachomuhusu yeye na aliekua rais wa Zanzibar, Dr. Ali Moh'd Shein ni kisa chenye kusisimua na kutupa Mafunzo ya namna mtu wa principles anavyopaswa kusimamia principles zake.

Kama kawaida yetu, mara zote tulipokutana na Othman tulikua tukipashana habari mbali mbali zinazohusu nchi, Vyama na Serikali. Siku moja katika masiku tukazungumza kuhusu vigeugeu vya Viongozi wa CCM Zanzibar hasa yanapokuja maswala ya nchi na hapo ndipo tukazungumza kuhusu yaliyojiri ndani ya Bunge la Katiba.

Othman akasema, moja ya jambo ambalo liliufanya mchakato ule ku-fail dakika za mwisho ni baadhi ya Viongozi wa Serikali (CCM) Zanzibar kuahidiwa vyeo. Mtego huo ndio mtego waliotegewa wakubwa wa CCM na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ndani Bunge la Katiba.

Othman akanambia kua, kabla ya kuepo kwa mtego huo, mambo yalienda vizuri na Wazanzibari wote walikua pamoja katika kuitetea Zanzibar na siku moja wakati wapo Dodoma, Viongozi wakubwa wa CCM Zanzibar ambao walikua ni Watendaji wa Serikali pia walimfuata Othman na kumpelekea mambo yao 19 ambayo wao kama Wazanzibari walitaka kwa vyovyote vile yapatikane (yaingizwe ndani ya Katiba) ili kuiokoa Zanzibar ndani ya mikono ya Tanganyika na kwa hivyo wakamuhakikishia Othman kua, endapo mambo hayo yatakosekana (Watanganyika watakataa kuyaingiza ndani ya Katiba) basi wao kama Wazanzibari wako tayari kugawana mbao na Tanganyika na hatimae wakamtaka Othman ayapitie mambo hayo vizuri na atoe usahuri wake.

Othman kwa kua ni Mwanasheria nguli na mzoefu wa muda mrefu wa masuala ya Sheria aliyapitia mambo hayo na kufanya marekebisho na hatimae yakawa saba (7) badala ya yale 19 ya awali na baadae akawapelekea marekebisho hayo ambayo yeye alihisi ni sahihi zaidi na hatimae Viongozi wale walikubaliana na mapendekezo na marekebisho yote ya Othman na kumtaka Othman ayapeleke mambo hayo 7 kwa rais wa Zanzibar wa kipindi kile Dr. Ali Moh'd Shein na amwambie kua, Wazanzibari walioko Dodoma bila ya kujaki itikadi zao za kisiasa wamekubaliana kwa pamoja kua, mambo hayo 7 ndio mambo ambayo yatasimamiwa ili kuikoa Zanzibar ndani ya mikono ya Tanganyika na kuipa nafasi nzuri zaidi Zanzibar ya kuweza kujipatia maendeleo.

Othman baada ya kupewa utumwa huo alisafiri kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kutekeleza agizo hilo alilopewa na wenzake na hatimae alikutana na Dr. Shein na kumueleza kama alivyotakiwa kumueleza.

Cha ajabu na cha kushangaza zaidi ni kwamba, baada ya kumueleza Dr. Shein alichotakiwa kumueleza, Dr. Shein nae akaongeza mambo yake matatu (3) na kuyafanya mambo hayo kua kumi (10) badala ya 7 ya awali na kumwambia Othman wende wakayasimamie.

Tukio hilo lilimpa moyo na imani kubwa Othman kwamba huenda kwa wakati huo, Zanzibar ikaweza kujikwamua katika Utawala wa Tanganyika. Hata hivyo; Othman anasema kua, alishtushwa na taarifa alizozipata kutoka kwa Balozi Seif wakati anajiandaa kurudi Dodoma.

Kwa mujibu wa simulizi hii, wakati Othman anajiandaa kurudi Dodoma alipigiwa simu na Balozi Seif akielezwa kua, mambo yameharibika Dodoma na kura haitakua tena ya wazi na kuambiwa kua, akili kichwani mwake.

Katika simu hiyo, Balozi Seif pia alimtaka Othman apige kura ya siri lakini Othman alikataa na kumwambia kua, kama alivyomwambia awali kua akili kichani mwake basi amuache atumie akili yake na sio kumshindikiza anavyotaka yeye.

Othman akawa ni mtu anaeshawishiwa na kutishwa sana ili akubali kufanya hivyo lakini alikataa na kumwambia Balozi Seif kua, suala lile baada ya miaka kadhaa mbele watu hawatokuja kumlaumu Dr. Shein wala yeye Balozi Seif bali watamlaumu yeye kama Mwanasheria Mkuu; "Kwenye suala hili wewe na Dr. Shein mukishakustaafu watu watawasahau lakini miaka mia ijayo watu wataulizana Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar alifanya nini kwenye hili? Hawatauliza rais au Makamu wa rais. Kwa hivyo suala hili ni langu sio lenu." Alisema Othman.

Baada ya msuguano mkali Othman akasimamia alichokiamini na hatimae tukashuhudia Othman akipiga Kura ya wazi ndani ya Bunge la Katiba na kuvikataa vipengele kadhaa vya Katiba Pendekezwa.

Kilichopelekea kufukuzwa kwake
Baada ya hapo Dr. Shein alimwita Othman Masoud na kumwambia kua anatakiwa ajiuzulu lakini Othman akakataa na kumwambia Dr. Shein; "Mheshimiwa mimi ninavyojua mtu akijiuzulu hua kafanya kosa. Kosa langu mimi lipi? Kusimamia maamuzi ya Wazanzibari ambayo hata wewe uliyabariki?" Othman akakataa na kumwambia Dr. Shein hawezi kujiuzulu labda amfukuze mwenyewe.

Othman akatwambia kua, alifanya hivyo kwasababu alijua kua, Dr. Shein alitaka kukwepa dhambi zake kwasababu kama angejiuzulu historia insigemwandika kama alifukuzwa kutokana na kusimamia maamuzi yake ambayo yalikua ya wengi bali ingemwandika alijiuzulu mwenyewe.

Maisha yake nje ya harakati
Othman kama tunavyojua kua ni mzaliwa wa Pemba, Mkoa wa Kaskazini (Pandani) lakini makazi yake kila anapokwenda Pemba ni Mkoroshoni karibu na alipokua alifikia Maalim Seif.

Othman ni mtu wa kawaida na ni mtu anaependa kwenda Pemba mara kwa mara na sisi mara nyingi tulipokwenda kumuulizia tuliambiwa kasafiri yupo Pemba.

Siku moja nilipomuuliza kuhusu sehemu anayoishi Pemba ndipo aliponambia kua, anaishi Mkoroshoni lakini hakai sana kwani akifika Pemba hukaa Mabondeni ambako hufanya shughuli zake za Kilimo cha Mikarafuu kuanzia asubuhi hadi saa 12 za jioni. Kwa hivyo, Othman nje ya harakati ni Mkulima wa kawaida anaependa kufanya shughuli zake hizo Kisiwani Pemba.

Je, Othman ni mtu alie karibu na watu?
Tofauti na watu wengi wanavyofikiria kuhusu ukaribu wake na jamii inayomzunguka, Othman ni mtu aliekaribu sana na watu. Fani yake na kazi zake za Kisheria zinamfanya awe hivyo na mara kadhaa nilipoenda kumuona Ofisini kwake alikua na watu wa itikadi tofauti. Othman si mtu ambae ungeweza kumuona akijichanganya na watu mara zote lakini sisi tuliobahatika kukutana nae tuliona kwamba, Othman ni mtu wa watu.

Anavyowajali Wazanzibari
Siku moja wakati tunazungumza kuhusu Zanzibar, Othman alitwambia kua, Mzanzibari kwake ndie kipaombele chake cha kwanza na akatuhadithia kua, wakati fulani alimpa kaka yake kazi ya kusimamia Ujenzi wa nyumba yake iliyopo kwao Pandani. Kaka yake huyo akaamua kutafuta Vijana kutoka Tanganyika na kuwapa kazi za kibarua. Siku moja alipokwenda kukagua akakuta Vijana wote wanaofanya kazi katika Jengo hilo ni Vijana kutoka Tanganyika ndipo alipoamua kumuuliza Kaka yake inakuaje Vijana wote wanakua ni Watanganyika wakati Vijana wa Kizanzibari wapo na hawana kazi?

Kaka yake akamjibu kua, kaamua kuwapa kazi Vijana hao kwasababu Vijana wa Kizanzibari hawawezi kazi za nguvu na kwa hivyo kama angewapa kazi hiyo Vijana wa Kizanzibari Ujenzi huo ungechelewa kumalizika.

Othman alikataa hoja hiyo na kumwambia kaka yake awape kazi Vijana wa Kizanzibari walnaoishi karibu na Ujenzi huo hata kama Jengo hilo halitomalizika milele.

Alichomwambia Dr. Shein baada ya kupora Ushindi wa Maalim Seif.
Kama tunavyokumbuka kua, Uchaguzi wa 2015 uligubikwa na giza nene ambalo liliiacha nchi katika Mgogoro mkubwa wa kisiasa. Othman kama mtu mwengine bila ya shaka alichangia na kupigana kadiri ya uwezo wake kuhakikisha kua, haki ya Wazanzibari inapatikana.

Siku moja anatusimulia kua, wakati anarudi zake msikitini alfajiri alikutana na ndugu wa Dr. Shein njiani na wakapiga stori kwa muda. Othman kwa kua alidhamiria kufikisha kile alichokiona yeye ni sahihi kumfikishia Dr. Shein aliamua kumpa salamu zake ndugu huyo wa Dr. Shein ili azifikishe kwa Dr. Shein. Akamwambia; "Mwambie Dr. Shein kua, ni heri akubali lawama na kulaaniwa na wachache muda huu kuliko kuja kulaumiwa na kulaaniwa na Wazanzibari wote baadae."

Nilipomuliza alikua na maana gani kusema hivyo akasema, maana yake ni kwamba, kama Dr. Shein angekubali kumpa haki yake Maalim Seif kipindi kile angelaumiwa na kulaaniwa sana na CCM (wachache) lakini angependwa sana na Wazanzibari (wengi) na kuendelea kwake kung'ang'ania madaraka kungemfanya apendwe sana na CCM (wachache) lakini baadae akishakustaafu angelaaniwa na wote na hicho ndicho tulichokishuhudia.

Kwa hivyo, tuliobahatika kukaa kitako siku chache na Othman Masoud tumejifunza mengi na ni wazi kua, kwa wakati tulionao tusingeweza katu kesema kua, Othman Masoud hatufai na hafai kuvaa viatu vya Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad. Ukiachana na uwezo wake mkubwa, Othman Masoud ni mtu mcheshi, anaependa kuzungumza na kuskiliza.

FB_IMG_1614661469689.jpg
 
Kumbe hakuna Zanzibar nje ya muungano kama hayati Baba wa Taifa alivyosema. Hawa wapemba huwa wanachukiwa sana na waunguja. Leo aleesha umenisaidia kuona chimbuko! Muungano ukifa lazima wapemba watafute nchi yao ya Pemba. Wapemba wanajificha katika koti la uzanzibari ila wao wana hangaika na kuifanya Pemba kuwa huru.
 
Kutokana na maelezo yako ni mtu anayechukia sana watanganyika pia alikuwa pandikizi la seif kwenye serikali ya Shein
 
Kumbe hakuna Zanzibar nje ya muungano kama hayati Baba wa Taifa alivyosema. Hawa wapemba huwa wanachukiwa sana na waunguja. Leo aleesha umenisaidia kuona chimbuko! Muungano ukifa lazima wapemba watafute nchi yao ya Pemba. Wapemba wanajificha katika koti la uzanzibari ila wao wana hangaika na kuifanya Pemba kuwa huru.
Hizo ni propaganda za watanganyika, zimepitw na wakati
 
Kama itawezekana wazanzibar wwjutawale wenyewe na hao wapemba nao wajitawale.

Yaani kuwalazimisha watu wasiokutaka.

Halafu waache hulka za kibaguzi
 
Na mie naomba kutoa ushuhuda wa Mhe Mason, haihusiani kabisa na siasa nashukuru kusema. Kuna taasisi moja hapa nchini inaitwa NBAA, Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi. NBAA ina kamati ya elimu na mafunzo, ikiripoti kwa Bodi kuu. Mie nilikuwaMjumbe (mimi ni Mhasibu) pamoja na yeye kutoka Zanzibar. He was, he is, a kind, articulate person. Alitusaidia sana umakini wake (as cool as a Judge) kila tulipopandwa jazba watu kufeli mitihani. Sijui kama NBAA iko kwenye CV yake.
 
Kama itawezekana wazanzibar wwjutawale wenyewe na hao wapemba nao wajitawale.

Yaani kuwalazimisha watu wasiokutaka.

Halafu waache hulka za kibaguzi
Hoja yako peleka uko kwenu butiama wazanzibari wameamka saiv
 
Hivi kwa nini hampendi kuitwa Watanganyika?
Mukiitwa kwa ilo jina mnakimbilia kwenye ubaguzi?
Nani amekataa kuitwa mtanganyika? Nilizaliwa kabla ya Uhuru na muungano ulinikita skuli ila natakani nasi tuwabague nyie wapemba mkome
 
Kumbe hakuna Zanzibar nje ya muungano kama hayati Baba wa Taifa alivyosema. Hawa wapemba huwa wanachukiwa sana na waunguja. Leo aleesha umenisaidia kuona chimbuko! Muungano ukifa lazima wapemba watafute nchi yao ya Pemba. Wapemba wanajificha katika koti la uzanzibari ila wao wana hangaika na kuifanya Pemba kuwa huru.
Mbona hayo hayakubainishwa kwenye mada hii?

Wewe umeyatoa wapi mchonganishi wewe??
 
Back
Top Bottom