SoC03 Masoko mtandao: Usimamizi wa taswira mtandaoni

Stories of Change - 2023 Competition

Mamshungulii

Senior Member
May 3, 2023
124
66
Taswira ya biashara mtandaoni ni muhimu sana kuhakikisha mfanyabiashara anajenga mtazamo chanya kwa wateja na kuendelea kunufaika na soko la mtandao.Biashara inaweza kupata misukosuko kutokana na mtazamo au hisia hasi za wateja. Kwa mfano inapotokea changamoto ya kutokukidhi ubora wa soko, ufafanuzi unapaswa kutolewa kwa haraka kwa lengo la kuendelea kulinda na kujenga taswira ya mfanyabiashara.

UMUHIMU WA KUSIMAMIA TASWIRA MTANDAONI
• Taswira ya biashara yako mtandaoni inavutia wateja kununua bidhaa
• Mambo yanayosemwa mtandaoni hayafutiki hivyo ni muhimu kkuyafuatilia na kuyatolea ufafanuzi
• Maoni ya wateja yana thamani kubwa katika kuboresha biashara yako

HATUA MUHIMU KATIKA KUSIMAMIA TASWIRA YAKO MTANDAONI
• Jiwekee mpango wa kusimamia taswira mtandaoni
• Hakikishaunafuatilia maoni yote yanayotaja biashara yako mtandaoni
• Fanya uchambuzi wa maoni kuhusu biashara yako kufahamu maoni hasi na chanya
• Tolea ufafanuzi wa haraka maoni yote yanayohitaji ufafanuzi wa haraka
• Andaa maswali na majibu yanayoulizwa sana kuhusu biashara yako.
• Toa ufafanuzi kuhusu maoni hasi hadharani
• Toa ofa/punguzo au kurejesha gharama kwa mteja kma sehemu ya kupunguza maumivu ya mteja
• Andaa maudhui yatakayoepusha mijadala isiyoendana na biashara yako.
• Kama unatumia waraghibishi chagua wwaraghibishi hao kwa makini
• Boresha biashara yako ili kuridhisha wateja wengi
• Wawekee kizuizii wateja wanaoonekana kujipanga kwa chuki kuharibu taswira ya biashara yako mtandaoni .Usimamizi wa taswira ya biashara yako mtandaoni ni Zaidi ya ulinzi wa biashara yako .Hatua hii haiepukiki kwani ndio huhakikisha biashara yako inaendelea kuwa haii na haiiyumbi ,kwa mfanyabiashara hata mtumiaji wa kawaida.

ULINZI NA USALAMA MTANDAONI
Masokomtandao yana faida nyingi kuliko hasara .Moja ya hasara chache ni hatari ya usalama mtandaoni,kutapeliwa katika kkufanya mauzo na manunuzi,kudukuliwa kwa kurasa za biashara.Mfanyabiashara unapaswa kuzingatia kkuchukua tahadhari kwa kufahamu kuhusu mashambulizi ya kimtandao na kuchukua hatua za ullinzi ili kufanya biashara yako kuwa salama na kuhakikisha pia wateja wako wako salama .Ulinzi na usalama mtandaoni unahusisha uwezo wa kkubainisha hatari,kuweka mipango ya kukabiliana na hatari na kuchukua hatua za kiusalama.

MAMBO YA KUZINGATIA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA MTANDAONI
• Weka nywila imara katika kifaa chako
• Tumia nywila tofauti ,kwa kifaa tofauti na ukurasa tofauti
• Hakikisha unafahamu kwa kina sera ya aplikesheni unayoitumia ili kutokukiuka sera hizo(kutumia brand au product inayojulikana ni ya Fulani)
• Hakikisha unafahamu kanuni za maudhui ili kuepuka maudhui unayoweka katika kurasa zako.

IDHAA ZA MASOKOMTANDAO
MasokoMtandao ni mchakato wa kutangaza na kutambulisha huduma na bidhaa kwa kutumia idhaa za usambazaji matangazo ya kibiashara kwenye mdahalisi, yaani majukwaa mbalimbali ya mtandaoni kama vile mitandao ya kijamii, majukwaa ya mtandaoni, tovuti, visakuzi, majukwaa ya maudhui. Masokomtandao ni tofauti na masoko ya asili yaliyozoeleka ambayo hujitangaza bidhaa kwa njia za mabango, televisheni, redio, vipazasauti, magari, magazeti na majarida. Biashara na makampuni nchini Tanzania zinatumia idhaa na majukwaa mbalimbali kujitangaza. Miongoni mwao, maarufu zaidi ni pamoja na ; tovuti za vyombo vya Habari,Facebook, Instagram, Twitter, LinkedIn, WhatsApp, Telegram, Messenger, na YouTube.

VIPENGELE VYA MASOKOMTANDAO AMBAVYO KWA KUVIFAHAMU VINASAIDIA UKUAJI WA JUHUDI KIMASOKO;
• Nia ya kufanya masoko ni suala la kwanza na muhimu katika kufanya masoko ya mtandaoni kwa ufanisi. Je unafanya masoko mtandaoni ili upate nini?Unalenga kuongeza mauzo au kutangaza biashara zaidi?
• muhimu kutambua na kuainisha walengwa wa biashara yako ili kufahamu sifa zao na namna nzuri zaidi ya kuwafikia.Kwa kufahamu sifa za wateja wako unaweza kuwafikia kwa wepesi zaidi.
• muhimu kufanya utafiti na kujua washindani wako na kujifunza kulingana na mazuri wanayofanya. Kwa kufahamu washindani wako pia unaweza kuongeza ubora wa bidhaa yako ili kuwa juu katika soko
• Mbinu ni njia za utekelezaji wa mkakati wako. Katika masoko mtandaoni unaweza kuwafikia wateja wako kwa tovuti, mitandao ya kijamii, matangazo mtandaoni, matumizi ya influencers na kupitia mbinu zingine.
• mbali na kuhimiza mauzo ya bidhaa ni muhimu kuwa na mkakati wa mawasiliano ya maudhui ili kusaidia wengine kupata taarifa na kujifunza kuhusu bidhaa kabla ya kupata na kununua.:

MASOKOMTANDAO KUPITIA VISAKUSI
Ni programu za kompyuta au simu ambazo hutumika kutafuta taarifa mtandaoni. Mfano wa visakusi ni Google, Mozila, Opera, Bing.

MASOKO MTANDAO KUPITIA BARUA PEPE
ni mfumo wa kidigitali wa kuwasiliana kwa kutumia anuani ya kielektroniki. Mawasiliano kwa njia ya barua pepe ni njia rasmi ya kuwasiliana baina ya taasisi na wateja wake. Kufuatia ongezeka la matumizi ya programu zinazompasa mtumiaji kuwa na anuani ya kielektoniki (email), wafanyabiashara wanatumia fursa hiyo kufanya masoko kwa watumiaji wa barua pepe.

MASOKOMTANDAO KUPITIA MAUDHUI mbinu zote za masoko hutumia maudhui lakini katika mbinu hii maudhui hufanyika kuwa njia kuu ya kuwavutia wateja. Mfanyabiashara huandaa maudhui mazuri yanaweza kuwavutia watu mahsusi na kupelekea walengwa kushawishika kununua au kutumia huduma fulani baada ya kushawishika na maudhui. Mfano wa mbinu hii ni kutumia mbinu za sanaa kama maigizo, vichekesho au muziki kuvutia wateja.

MASOKO MTANDAO KUPITIA MATANGAZO mbinu ya matangazo mtandaoni. hutumika kufikia watumiaji wengi zaidi wa mitandao kwa wakati mmoja. Matangazo ya mtandaoni yanahusisha kulipia kwa wamiliki wa mitandao au mawakala wa matangazo mtandaoni ili waweze kuweka matangazo ya bidhaa yako kwa watumiaji unaowalenga katika mitandao hiyo.

MASOKOMTANDAO KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII ni ambinu inayotumiwa na kukua zaidi hasa kufuatia ongezeko la matumizi ya mitandao ya kijamii. Mbinu hii pia ni rahisi hasa kwa wafanyabiashara wadogo kwani ni rahisi kutumia mitandao ya kijamii na kupata faida mbalimbali ikiwemo kufanya mijadala na wateja. Mitandao ya kijamii inahusisha idhaa kama Instagram, Facebook, Twitter.

MASOKOMTANDAO KUPITIA WARAGHIBISHI, mitandao mageuzi ya kijamii imeibua makubwa katika masoko, moja ya mageuzi hayo ni kuibuka kwa watu wenye ushawishi mkubwa mtandaoni (waraghabishi). Wafanyabiashara hutumia kundi hili kuwafikia watu wengi na kuongeza ushawishi kuhusu bidhaa na huduma zao Nimuhimu kwa mfanyabiashara kuzingatia kwamba mbinu za masokomtandao zinategemeana na mafanikio ya mbinu hizo yanategemea mikakati. Mfanyabisahara anapaswa kutekeleza mbinu hizi huku akifanya tathmini kwa lengo la kuboresha kila hatua ili kupata matokeo yanayotarajiwa.

Teknolojia imerahisiha namna ambavyo wateja wanachagua na kulipia bidhaa mtandaoni. Wateja wanaweza kuchagua, kulipia na kufikishiwa bidhaa bila kuonana ana-kwa-ana na wauzaji wa bidhaa.. Masoko ya Kidigitali kwenye visakuzi ni yale ya kuwekeza kwenye kuhakikisha kuwa mtu anapotafuta kuhusu jambo, bidhaa au huduma inayofanana na ya kwako, basi huduma zako zinatokea juu zaidi. Kuna aina mbili za masoko ya visakusi, masoko ya visakuzi vya kulipia na masoko ya visakusi kwa kutumia nguvu ya maudhui.
 
Back
Top Bottom