SoC02 Maskati, tuimarishe uchumi wetu kwa kilimo cha kisasa

Stories of Change - 2022 Competition

Bahati mahimbo

New Member
Sep 30, 2015
2
0
Maskati ni Kata inayopatikana upande wa Kaskazini Mashariki Mwa Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro. Wakazi wa Kata hii kwa kiasi kikubwa huishi kwa kutegemea shughuli za Kilimo hasahasa kilimo Cha Mahindi na Maharage.

Mazao mengine kama vile Ndizi, Mihogo, Kahawa, viazi, Njegere,nk. ingawa yanastawi vizuri katika vile hivi vya Milima ya Ngulu, hulimwa Kwa kiasi kidogo na hayatiliwi mkazo sana. Aidha Wakulima hawa hutumia Jembe la Mkono na huzalisha kwaajili ya chakula tu na kuuza kidogo ili kupatafedha za kujikimu.pia Wakulima hawa hutegemea tu mvua Richa ya uwepo wa Mito mingi na mikubwa isiyokauka Mwaka Mzima.

HALI YA HEWA NA JIOGRAFIA YA ENEO
Kata ya Maskati ni eneo lenye Milima, miinuko na mitelemko. Ni Eneo lililozungukwa na Misitu, Mito mikubwa ambayo mwaka mzima inatiririsha maji na ardhi yake Ina rutuba ya kutosha kuzalisha Kila aina ya mazao. Maskati ni Eneo la Ukanda wa baridi, pia Kuna nyanda za malisho ya mifugo.

Maskati panafikika kutoka wilayani Mvomero kwa Barabara. Hivyo kama wdkulima watabadilika na kufanya Kilimo Cha kisasa, wanaoweza kukuza uchumi wa kaya na kuchangia Pato la taifa

MABADILIKO
Wananchi wa Maskati kwa sasa wanahitaji kubadili aina ya Kilimo ili kupata tija zaidi. Kwanza wanahitaji kuacha kutegemea Mvua kwa Kilimo kwa sababu eneo hili Lina Mito isiyokauka Mwaka Mzima. Hivyo waanze kuwekeza katika Kilimo Cha Umwagiliaji. Hii itasaidia kupatikana Kila aina ya mazao mwaka mzima.

Pili, Wananchi wabadili aina ya mazao ya kulima. Waache Kilimo Cha mazoea ( traditional cultivation) yaani kulima Mahindi na Maharage Kila mwaka. Badala yake, waanze kuzalisha mazao yafuatayo kwa Umwagiliaji na yatawaletea pesa nyingi. Nayo ni:

Nyanya Maji: Hili ni zao la chakula na biashara. Kwa Eneo hili hustawi Sana na halichukui muda mrefu hadi kuvuna. Watu wa Maskati, ardhi tunayo, Maji tunayo, ni aibu kufuata Nyanya Kibati au Turiani badala ya sisi kuwauzia wao. Tubadili MTAZAMO, tuanze kuzalisha nyanya kwaajili ya matumizi yetu na biashara.

Nyanya Chungu: Zao hili pia hustawi Sana katika Eneo hili lakini halilimwi kwa wingi. Wananchi wa eneo hili wakihitaji Nyanya Chungu ni hadi zitoke maeneo mengine na kuletwa na wafanya biashara. Tubadilike tuzalishe na tuwauzie wao kwa sababu ardhi yenye rituba ipo, Maji yapo na hii ni fursa ya pesa na chakula.

vitunguu: Hili pia zao ambalo hustawi vizuri katika Eneo hili ila halipewi kipaumbele. Wenyeji wa hapa wakishavuna Maharage na Mahindi wakapata ugali, ni baasi wanasubilia hadi Msimu mwingine wa kilimo.
Tubadilike, zao hili ni la muda mfupi na ni fursa ya pesa kwani soko lipo la uhakika.

Mazao mengine kama haya ni: Karrot, Pilipili hoho, Mchicha, Kabichi, Chinese, nk. Haya yote yanastawi vizuri na soko lipo ndani na nje ya Kata.pia uzalishaji wa mazao haya unasaidia upatikanaji wa mboga badala ya kutegemea ugali maharage kiila siku jambo linalosababisha lishe duni.

Pia mazao yafuatayo;
Mahindi, Mihogo, Kahawa, Ndizi, Iriki, Malimao, machungwa tangawizi, Mbaazi, Kunde, yaimarishwe uzalishaji wake kwa kuongeza kuweka miundombinu ya Umwagiliaji kwani yanastawi na hakuna gharama kubwa za uhudumiaji.

Wananchi tusitegemee Kilimo Cha Msimu. Tujenge utamaduni mpya wa kuzalisha Kila aina ya Mazao katika vipindi vyote vya Mwaka. Mfano Msimu wa mvua nyingi unapanda mazao ya muda mrefu, na kipindi mvua zinapungua Kilimo kiendelee kwa kupanda mazao ya muda mfupi na kumwagilia. Hii itatusaidia mwaka Mzima kuwa na chakula na pia kupata fedha kwa kuuza nje ya Eneo lako na nje ya Wilaya.

MIFUGO
Katika mifugo pia tunahitajika kufanya mageuzi ili tuendane na kasi ya Maendeleo kitaifa na kidigitali. Maskati wanafuga Ng'ombe, Mbuzi, Kuku, Kondoo,nk. Lakini ugugaji bado haujaleta tija katika afya na kipato cha watu. Napo tunahitaji kubadilika.

Katika Sekta ya ufugaji tujitahidi kuwaona maafisa mifugo ili tuzalishe Maziwa na nyama kwa wingi, pia tunahitaji kugeukia ufugaji wa kuku wa kisasa ili tuzalishe Mayai mengi na vifaranga kwa ajili ya biashara na chakula. Hili ni Eneo lenye pesa nyingi ambalo watu wa Maskati kutokana na kuishi maisha ya asili (traditional life) bado hatujalifikilia. Tubadilike, hizi ni fursa muhimu sana.

NAFASI YA SERIKALI
Serikali katika ngazi ya kata na Harimashauri ya Wilaya, Wana jukumu kubwa la kuhakikisha maafisa kilimo wanatumia Taaluma zao kuwafundisha wakulina nanna Bora ya kuendeleza kilimo katika Eneo hili ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya biashara na chakula.

Pia, wanajukumu la kutoa mikopo kwenye vikundi ili wananchi waweze kununua Generator kwaajili ya umwagiliaji na mbolea na vitu vingine. Pia, serikali inahitajika kuboresha Barabara ili kusaidia usafirishaji wa mazao nje ya Kata ili kukuza soko.

Pia, ili kulete mabadiliko haya kwenye Kilimo na Uchumi, serikali inapaswa Kutatua changamoto ya Umeme ambayo mpaka nashika karamu hii bado Umeme hamna. ili kuzalisha kuku kwa wingi na Mayai, umeme unahitajika, ili kuboresha biashara ya Maziwa, Umeme unahitajika. Hivyo wakati tunahamasisha wananchi kuchangamkia fursa za Kilimo na ufugaji, serikali ilete Umeme ili site kwa pamoja tuijenge nchi yetu.

HITIMISHO
Kwa kufanya hivyo, tutakuwa tumesaidia kuboresha lishe katika kaya zetu, tutapunguza udumavu, tutaweza kuongeza pato la mtu mmojammoja na taifa kwa ujumla

Asanteni Sana,
 
Back
Top Bottom