Masikini Mrembo huyu awezi Kubeba ujauzito!!

NAPITA

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
5,076
2,000
Happiness-Millen-Magese.png
MISS Tanzania 2001 ambaye kwa sasa ni mwanamitindo wa kimataifa,Happiness ‘Millen' Magese amejitangaza kuwa mwathirika wa ugonjwa wa Endometriosis unaofanya mwanamke kushindwa kuwa na uwezo wa kubeba ujauzito.

Kutokana na kukumbwa na tatizo hilo,Millen ameanzisha kampeni ya kuhamasisha wanawake na vijana kupaza sauti zao wanaposumbuliwa na ugonjwa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,Millen ambaye aliongozana na daktari bingwa wa masuala ya wanawake na uzazi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,Dk Belinda Balanda,alisema ameteseka na ugonjwa huo kwa muda mrefu na kwamba amekata tamaa ya kuolewa,kwa vile hana uwezo wa kubeba ujauzito.

Millen alisema wanawake wengi na wasichana wamekuwa wakisumbuliwa,lakini hawajui kama ni tatizo kubwa linalohitaji utafiti mapema kwa ajili ya kutafuta suluhisho. "Huu ni ugonjwa ambao umenitesa kwa muda mrefu na umeniathiri, leo siwezi kuolewa kwa sababu sina uwezo wa kubeba mimba,ni mwanaume gani atakubali kukaa na mwanamke asiyezaa, wakati nikiwa mdogo sikujua ni tatizo kubwa,sasa kila siku ninaumwa," alisema. Alisema kutokana na jinsi alivyotaabika kwa ugonjwa huo kwa kufanyiwa upasuaji mara 12,bila mafanikio,sasa kupitia Taasisi yake ya Millen Magese itakuwa ikitoa mafunzo kuhusu ugonjwa huo na dalili zake kwa ajili ya kupatiwa matibabu haraka. Kwa kuanzia alisema Jumapili ya wiki hii watatoa mafunzo kwenye fukwe za Coco ambapo watu wataelimishwa athari na nini kifanyike ikiwa watagundulika kusumbuliwa na tatizo hilo. Magese alihimiza kampuni na wadau mbalimbali kuwaunga mkono katika kuelimisha jamii,lakini pia wanakusudia kujenga hospitali ya wanawake Dodoma kwa ajili ya kutibu ugonjwa huo ili kuwaokoa wanawake wengi kwa kuwapatia dawa na vipimo kwa bei watakayoweza kuimudu. Akizungumzia ugonjwa huo,Dk Balanda alisema ‘Endometriosis' ni seli za mji wa uzazi zinazokua nje ya uzazi ambazo hushambulia eneo hilo na kumsababishia mwanamke maumivu makali wakati wa mzunguko wa hedhi. Alisema mtu mwenye ugonjwa huo wakati wa hedhi huumwa hadi siku 10,wakati mwingine hutapika,hutokwa damu wakati akienda haja ndogo,hupata maumivu wakati wa tendo la ndoa na matibabu yake ni dawa za kupunguza maumivu au kufanyiwa upasuaji.
 

Attachments

 • MAGS.jpg
  File size
  28.3 KB
  Views
  802
 • MAGS.jpg
  File size
  79.8 KB
  Views
  835
 • MAGS.jpg
  File size
  22 KB
  Views
  795

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
39,257
2,000
Soma Gazeti la Habari leo wakati naweka mambo sawa ya kukopy hii story niiweke hapa.

Itakuwa Kachomoa Sana Injini Enzi za Ujana ( Usichana ) Wake Kudadadeki...............................!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 

bucho

JF-Expert Member
Jul 13, 2010
4,917
2,000
Imechapishwa Alhamisi,29 Mei 2014 00:09 Imeandikwa na Mwandishi Wetu Imesomwa mara: 44

MISS Tanzania 2001 ambaye kwa sasa ni mwanamitindo wa kimataifa,Happiness ‘Millen’ Magese amejitangaza kuwa mwathirika wa ugonjwa wa Endometriosis unaofanya mwanamke kushindwa kuwa na uwezo wa kubeba ujauzito.

Kutokana na kukumbwa na tatizo hilo,Millen ameanzisha kampeni ya kuhamasisha wanawake na vijana kupaza sauti zao wanaposumbuliwa na ugonjwa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,Millen ambaye aliongozana na daktari bingwa wa masuala ya wanawake na uzazi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,Dk Belinda Balanda,alisema ameteseka na ugonjwa huo kwa muda mrefu na kwamba amekata tamaa ya kuolewa,kwa vile hana uwezo wa kubeba ujauzito.

Millen alisema wanawake wengi na wasichana wamekuwa wakisumbuliwa,lakini hawajui kama ni tatizo kubwa linalohitaji utafiti mapema kwa ajili ya kutafuta suluhisho. “Huu ni ugonjwa ambao umenitesa kwa muda mrefu na umeniathiri, leo siwezi kuolewa kwa sababu sina uwezo wa kubeba mimba,ni mwanaume gani atakubali kukaa na mwanamke asiyezaa, wakati nikiwa mdogo sikujua ni tatizo kubwa,sasa kila siku ninaumwa,” alisema. Alisema kutokana na jinsi alivyotaabika kwa ugonjwa huo kwa kufanyiwa upasuaji mara 12,bila mafanikio,sasa kupitia Taasisi yake ya Millen Magese itakuwa ikitoa mafunzo kuhusu ugonjwa huo na dalili zake kwa ajili ya kupatiwa matibabu haraka. Kwa kuanzia alisema Jumapili ya wiki hii watatoa mafunzo kwenye fukwe za Coco ambapo watu wataelimishwa athari na nini kifanyike ikiwa watagundulika kusumbuliwa na tatizo hilo. Magese alihimiza kampuni na wadau mbalimbali kuwaunga mkono katika kuelimisha jamii,lakini pia wanakusudia kujenga hospitali ya wanawake Dodoma kwa ajili ya kutibu ugonjwa huo ili kuwaokoa wanawake wengi kwa kuwapatia dawa na vipimo kwa bei watakayoweza kuimudu. Akizungumzia ugonjwa huo,Dk Balanda alisema ‘Endometriosis’ ni seli za mji wa uzazi zinazokua nje ya uzazi ambazo hushambulia eneo hilo na kumsababishia mwanamke maumivu makali wakati wa mzunguko wa hedhi. Alisema mtu mwenye ugonjwa huo wakati wa hedhi huumwa hadi siku 10,wakati mwingine hutapika,hutokwa damu wakati akienda haja ndogo,hupata maumivu wakati wa tendo la ndoa na matibabu yake ni dawa za kupunguza maumivu au kufanyiwa upasuaji.
 

NAPITA

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
5,076
2,000
Bado yule mwenye Ule ugonjwa wetu wa kisasa kujitangaza sio unajificha uku SWEEDEN .
 

theki

JF-Expert Member
Nov 1, 2013
2,724
1,195
Dada kuna kitu hataki tuu aachie ya dunia apige magoti kwa mwenyenzi mungu kwa wakristo kama sisi amkabidhi Yesu maradhi atapona.Kuolewa asihofu ataolewa tuu sema bado moyo wake hajauachia
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
39,257
2,000
Usiseme hivyo unakosea labda ni tatizo la kuzaliwa na yeye linamtesa.kuna baadhi ya vitu ombea tu vitokee kwa wengine ila si kwako usingesema hivyo.

Nimekuelewa Mwana JF Mwenzangu Na Niwie Radhi Sana Kama Nimekukwaza ILA Tupo Pamoja Na JF Yetu na Tunalisongesha Kwa Raha Zetu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom