Masikini Mange Kimambi

Masikini Mange Kimambi

Namuhurumia sana Mange Kimambi kwa aibu atakayopata kutoka kwa Watanzania.

Binafsi natamani maandamano ya amani yawepo reforms zifanyike kusudi huko kupiga kura kuwe na maana kuliko maigizo haya ya kila siku ya kwenda kupiga kura wakati mshindi anajulikana tayari.

Kwa nguvu alizotumia Mange Kimambi nasikitika kusema watanzania wata mdisappoint na hatokaa aamini macho yake.

Kwa hali ilivyo huku uraiani hakuna mwenye nia ya kuandamana na ila kuna asilimia ndogo sana ya watu ambao watapiga kura.

Asilimia zaidi ya 70 tumeshakubaliana na hali ,na hiyo siku watu tutaichukulia kama zilivyo siku nyingine, hatupigi kura ila kuhusu kuandamana itategemea pia japo si rahisi kufanyika.

Nikikumbuka maandamano ya UKUTA yalivyotikisa kipindi kile na hakuna Mtanzania hata mmoja aliyejitokeza kuandamana licha ya kujazana upepo wa kuandamana ninadhani hata hii tarehe 29 mambo yatakuwa ni yaleyale.

Watu hatuwazi kabisa kuhusu uchaguzi kila mmoja yupo busy na shughuli yake na hatuna habari kabisa kuhusu huo uchaguzi feki.

Pole sana Mange, watanzania sisi ni kama kenge hatusikii mpaka damu zitutoke masikioni .
Mange, anasema viongozi wa cdm ni waoga wanaogopa kuitwa polisi, ila yeye kakimbia nchi kabisa! Yaani anawajaza watu kama wajinga,ilitakiwa aende bongo aongoze maandamano,sio kuwajaza wengine akiwa mbali.viongozi wa CDM wakijazwa wakafuata asemacho bila kujongeza,imekula kwao.
 
Mange ni mjumbe wa kuamsha kama unataka kujisahau, nafikiri anajua hilo, ila anajaribu kuwafanya wasijisahau.
 
Back
Top Bottom