Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,384
- 24,355
Masikini Mh Edward Ngoyai Lowassa, mwanasiasa machachari tuliyemjua kwa miaka mingi, ametangulia mbele za haki.
Si vizuri kumuongelea vibaya marehemu, lakini hata Rais Mwinyi aliwahi kusema, maisha ni kitabu, tuishi vyema ili watakao kisoma kitabu chako cha maisha, wafurahie hadithi ya maisha yako.
Hisia zangu ni ile miaka ya 94-2000 ambapo Lowassa alikuwa waziri wa Ardhi.
Alitenda kosa ambalo kimsingi nikajiambia, huyu mzee kajichotea laana isiyosameheka.
Lowassa kama watu wengi wa kaskazini wanapenda sana ardhi, iwe ya kudhulumu au haki.
Katika hili nasikitika kusema alidhulumu ardhi ya KKKT Mbezi Beach, pale Tangi Bovu.
Mzee mmoja maarufu anaitwa Arnold Kileo, alikuwa Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Breweries. Mzee Kileo alitoa ardhi yote karibia eka tatu au nne kwa kanisa, kama sadaka yake.
Naamini kabla ya kutoa ardhi hiyo ,mzee Kilewo aliomba kwa Mungu.
Maaombi yalipoenda wizarani kubadili jina, kiwanja kikakatwa nusu bin nusu.
Nusu moja akajimilikisha kwake Lowassa, ndugu zake na marafiki, kina Kimbisa, na nusu ndiyo akakibakishia kanisa.
Waumini wa hapo walishangaa kwani walijua Lowasa ni Mluteri, kwa nini afanye vile?
Wakamwomba Baba Askofu Sendoro akamwone waziri na kumsihi arudishe ile nusu ya eneo, Lowassa alikataa.
Alipokataa Baba Askofu alishukuru na kumtakia heri, Lawassa asijue kuwa hapo tayari ndipo laana ilipotoka.
Cha kushangaza, kila aliyeweka mradi katika kile kiwanja kilichoporwa, mradi ulikufa, TANESCO walikodi ofisi pale wakaishia kuhama. Ilikuwepo supermarket ya Imalaseko, Dry Cleaner na Gym , vyote vimekufa.
Hata jengo lililo na benki ya NMB pale nayo linakosa wapangaji.
Tukija kwa ndugu yetu Lowassa ,safari yake ya kisiasa ilienda kusuasua. Hata zlipochaguliwa waziri Mkuu, hakudumu.
Lowassa akakosana na rafikiye mkubwa, Jakaya Kikwete, na marafiki hao wakawa maadui.
Mwisho alihama CCM kabisa, na uamuzi bado haukuwa na tija, akarudi.
Lowassa akawa kama mwanasiasa anayetangatanga nyikani.
Pale kanisa la Mbezi KKKT, Lowassa hakuwahi kuslikwa shughuli yoyote ya harambee, ingawaje Sumaye alialikwa mara nyingi.
FUNZO, jamani tumwogope Mungu na tumtumikie hata tukiwa na vyeo vikubwa.
Kwa kufariki akiwa na miaka 70, Lowassa alikuwa bado mdogo mwenye miaka si chini ya 15-20 mbele. Lakini yote ni mapenzi ya Mungu RIP Edward Ngoyai Lowassa.