Masikini kaka huyu

nitajaribu muuliza rafiki yangu (kaka) kujua kama kuna watu wengine wanajua
 
ukimwi aliupata kabla ya ndoa au baada?
hapa hatujui ila hawakupima kabla ya ndoa .. imejulikana baada ya kubeba mimba na kuanza kuumwa ndipo hospital kuamua kupima na kugundua kuwa mke mwathirika mume ajaathirika ...
 
mmh si rahisi kijana kustick
 
sawa mkuu

kuna mtu mmoja humu alitoa mfano kwenye mada kama hii kuwa 'ukishituka usingizi ukakuta umemlalia nyoka na hajakuuma simama na chukua hatua mungu kakuamsha uchukue hatua...ila ukirudi kulala na ili hali huyo nyoka bado yupo hapo ukiamini Mungu aliyekulinda awali atakulinda tena huko itakuwa kumjaribu Mungu' utang'atwa tu hakuna namna nyingine...
 
point taken mkuu asante .. kiukweli kijana nacheza na mdomo wa mamba .. binti akiachwa chumbani anakuja sebuleni ni mitego na vilio anataka njunja
 
nimeisoma vizuri hii nyuzi
ila mpaka sasa naamini Mungu akiwa upande wako hakuna wa kupangua hilo

ila sasa je atamuachaje huyo mpenzi??
kama anampenda sasa itakuaje???
 
Afya kwanza haki ya ndoa baadae, anadhani jamaa akishaathirika ataweza hata kutoa hiyo haki ya ndoa anayodai? Huyo dada ni selfish na hamjali mwenzie hata kidogo anataka wote wawe kwenye safari moja ya kumeza dawa
 
Tatizo ninaloliona hapa ni unyanyapaa...Mume kamnytanyapaa mkewe...Na hilo ndilo litamuathiri zaidi

Baba ampende mke wake...alale nae kitandani...atumie Condom kwa uangalifu mkubwa.....kama anampenda atamtimizia....kabla ya kumuingilia ahakikishe amekuwa tayari haswa....

Wapo watu wengi wanaishi na wenza wenye Maambukizi ...Lakini hawawatupi wenza wao....

Dada anatakiwa kufanyiwa Counselling ya kufa mtu....amechanganyikiwa sana...anatakiwa ajikubali
 
Mkuu hapo jamaa amweke kitimoto huyo mchumba wake amuulize kavitoa wapi virus? Hicho ndo kiwe chanzo cha kuachana.... Akijifanya ana huruma atakwisha.
 
point taken mkuu asante .. kiukweli kijana nacheza na mdomo wa mamba .. binti akiachwa chumbani anakuja sebuleni ni mitego na vilio anataka njunja

Sisi tumepima baby? mimi na wewe
 
mwanume jamnyanyapaa ila kijana hana hisia ya tendo landoa dada anataka afanye tu na hataki kutumia ARV na hataki kutumia condom kwa iman kuwa ataponywa na Mungu ... mwanaume kachanganyikiwa haelewi
 
Tyta kijana ana moyo wa uvumilivu hata kuendelea kuishi naye ila binti kawa mkorofi analazimisha penzi na kilio juu.. mimi naona huruma sana kwa kijana analalamika maisha yake kaingiza doa japo kijana naye kafanya uzembe kuoana bila kupima

Yaan akifanya ujinga wa uvumilivu atapotea
 
Last edited by a moderator:
Ninavyojua kwa kweli hata huyo mmewe hataweza ku duu maana anajua kabisa pale maji ya shingo
:A S-baby::rockon:
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…