hapo wote wameshakosea kuamua kufunga ndoa bila kujua afya. sio kwamba huyo kaka hakuwahi kuwa na mwanamke kabla ya huyo, pengine hata yeye angeweza kuambukizwa. alimpenda huyo dada, akamuamini kwa tabia zake ndio maana akaamua kumuoa. kuathirika kwa huyo dada haimaanishi kua alikua na tabia mbaya ni bahati mbaya ktk mahusiano yake ya awali akaambukizwa, akaendelea na tabia yake nzuri akapata mchumba akaolewa.
kiubinadamu tu huyo kaka angekua yeye angependa ahurumiwe, asikimbiwe, atunzwe, apewe huduma zote. kwa vile imetokea kwa mwenzake basi amfanyie yaliyo mema, amtunze, bahati nzuri wamepata ujauzito wautunze vizuri wampate mtoto wao, mamlee kwa pamoja.
jitahidini kuongea na huyo wifi yenu akubali kutumia kondom maana hata yeye asingekubali pekupeku kama mumewe angekua mgonjwa. atumie dawa zake vizuri awe na afya nzuri aendelee kupendeza mpaka mungu atakapomchukua maana ukimwi sio kifo, anaweza kufa hata kwa kifo kingine na sio huo ugonjwa, wazima wanaweza kumtangulia yy akaishi miaka mingi zaidi.
yeye sio wa kwanza kuambukizwa. kaka akimuacha ni mbaya zaidi, atakua na stress, mawazo mengi atatutoka mapema. wasivunje ndoa please hilo ni jaribu lao.