Masikini alichomfanyia mkewe kilinifadhaisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masikini alichomfanyia mkewe kilinifadhaisha

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jacaranda, May 10, 2012.

 1. J

  Jacaranda Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watu husema unaweza kumfanya mwanamke kuwa malkia wa uingereza lakini kama hakupendi atakunyea tu bila kujali,hii yaweza kuwa kweli.Lakini niyoyashuhudia juzi yameniaminisha pia ukiwa na fedha unaweza kumnyea mwanamke na badala ya kuchukia akafurahi.Siku hiyo ilikuwa hivi

  Mziki ulikuwa unapigwa kwa sauti ya taratibu ,watu waliendelea kuingia ukumbini.Nilipoingia ukumbini nilikaa nyuma ya wanandoa wenye umri wa makamo ambao kwa mtazamo wa nje tu ulionyesha kuwa wana fedha za kutupa.Wakati wakiwa wamekazia macho kwenye jukwaa ghafla akapita msichana moja mrembo sana ambaye alimtambua mwanandoa wa kiume akasimama na kusalimiana naye na kisha wakapiga stor mbili tatu kabla ya kuwaacha wanandoa hao.

  Alipoondoka mke wa jamaa kwa sauti ya ukali akamuuliza “Huyo ni nani” Mume wake bila hata ya kumuangalia akajibu “ni nyumba ndogo yangu” Mkewe kusikia hivyo akakunja ndita kisha akamkunja shati mumewe na kumwambia kwa ukali”naomba taraka yangu sasa hivi” mumewe akatafakari kwa muda na kisha kwa sauti isiyo na hisia hata chembe akamjibu “Mke wangu naomba ufikirie vizuri.Si unajua maana ya taraka? Nikikupa taraka inamaanisha hutaendesha tena range,wala benzi,safari za Dubai,China na ulaya hautazipata tena na ina maana hautaishi tena kwenye nyumba za kifahari wala kufanya shoping Woolworth au ufaransa” Akaendelea “na kwa umbo lako hilo sidhani kama tena utapata mwanaume hata wa kukusimamisha ,tumia busara mke wangu” mkewe kwa kugundua ukweli akaliachia shati la mumewe akageuz uso wake stejini akaendelea kutazama show.

  Baada ya muda akapita msichana mwingine mrembo pia akasimama na kumsalimia jamaa na kisha akaendelea na hamsini zake.Mkewe akamuuliza tena jamaa “na huyo ni nani?” Jamaa akamjibu kwa pozi lilelie “hiyo ni nyumba ndogo ya rafiki yangu Fred” mkewe akamjibu kwa heshima kubwa ambayo ilinishtua mimi “,’Mhhh huyu wala siyo mzuri kama nyumba ndogo yetu’ ”
   
 2. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  anajua upande gani wa mkate una siagi

   
 3. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Chezea mapedeshee??lazima ukubali kupangiwa foleni..
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Maana ya "taraka" ni nini?

  Au ulimaanisha talaka?
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  una uhakika haya uliyashuhudia?
   
 6. Vaislay

  Vaislay JF-Expert Member

  #6
  May 10, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 4,512
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  unajua sanyingine dawa la jamaa kicheche ni kujitoa ufaham kama alivyomjibu bibie alipoonyeshwa nyumba ndogo ya shemej tho athari ni kubwa..wanaume wenye hela ni utumwa sana..hiyo inaonyesha bibie shida zake zitamfanya avumilie.kwakuwa amekubaliana na hilo akaendelee kupangwa tu..Na pia nimempenda sana huyo mume kwa kuwa mkweli,ningekuwa mimi ningemsaidia kumnunulia mabox ya kondom tu.
   
 7. Dr. Wansegamila

  Dr. Wansegamila JF-Expert Member

  #7
  May 10, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 1,233
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Umeniboa hujui kuandika kiswahili.......... Otherwise hadithi yako ni nzuri. Amekusimulia nani hadithi hii?
   
 8. Kilahunja

  Kilahunja JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 1,497
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  kwanini unakuwa muongo? Lini ulienda harusin ukakaa nyuma ya hao wanandoa? Hii ni stor ya ku2ngwa mara ya kwanza nlisimuliwa 2007 wakat nko form six then nkaisikia tena 2009 nko 2nd year..ACHA IZO PELEKA KWENYE GOSSIP..OVYOO.
   
Loading...