Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,428
MASHUJAA VITA YA KAGERA WANAENDELEA KULIPWA PENSHENI
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax amesema mashujaa wote waliopigana Vita ya Kagera na waliostahili malipo ya viinua mgongo na pensheni walikwishalipwa na wengine wanaendelea kulipwa kwa mujibu wa Sheria ya pensheni na viinua mgongo ya mwaka 1966, ikiwemo pia malipo ya ulemavu na kustaafu.
Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Rose Busiga bungeni Jijini Dodoma Aprili 28, 2025 Dkt. Tax amesema:
"Kundi ambalo lilishiriki vita na halikuwa limeajiriwa na vyombo vya ulinzi na usalama, baada ya vita lilipewa nafasi ya kujiunga katika vyombo vya ulinzi na usalama kwa kufuata taratibu. Kwa wale walioamua kutojiunga na wale waliokosa sifa katika kundi hilo walilipwa kifuta jasho Asante Nyerere kiasi cha Shilingi 5,000.00 na kurejeshwa makwao".
Ameongeza kuwa wizara imeandaa mapendekezo ya maboresho ya Sheria ya Pensheni na Viinua Mgongo ya mwaka 1966 na kuiwasilisha Serikalini, yakijumuisha Maveterani waliopigana vita ya Kagera ambapo Wizara imewasilisha Serikalini mapendekezo ya kuona uwezekano wa kuwaingiza Maveterani waliopigana Vita vya Kagera kwenye utaratibu wa Bima ya Afya.