Mashtaka ya barcelona dhidi ya bayan munich

Mashtaka ya barcelona dhidi ya bayan munich

Sheghwede

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2013
Posts
277
Reaction score
124
[h=5]Hati ya malalamiko na mashtaka ya FC Barcelona dhidi ya Bayern Munich
Mbele ya mahakama ya juu kabisa ya Hispania

Hata hii inaletwa kwa kuzingatia vifungu muhimu vya sheria na mikataba ya kimataifa juu ya haki za binadamu ikizingatiwa;

1. Kwamba kitendo cha Bayern kuifunga Barcelona ni cha kinyama, cha kudhalilisha na kilichovuka viwango vya kibinadamu;

2. Kwamba Bayern kwa kufanya hivyo kimevunja kwa kiwango cha juu kabisa haki muhimu za binadamu na hivyo kupelekea kufanya kosa kubwa kabisa dhidi ya ubinadamu (crimes against humanity)

3. Kwamba Bayern, ikiwa na akili timamu, bila kulazimishwa na mtu yeyote, na kwa makusudi kabisa, ikaifunga Barcelona 4-0 na kama haitoshi ikaongeza 3-0 uwanja wa nyumbani

4. Kwamba kitendo hichi ni cha kinyama kwani kimewaharibu wachezaji wa Barcelona kisaikolojia kiasi kwamba hawataweza kucheza angalau kwa kipindi cha miezi mitatu hivi

5. Kwamba jambo hili si tuu limewaumiza Barcelona bali pia watu muhimu duniani kama George Bush, Bill Clinton, Barack Obama, Bill Gates,Warren Buffet, Goodluck Jonathan, Goodluck Temu, Uhuru Kenyatta na Nelson Mandela.

6. Kwamba jambo hili halikubaliki kabisa kwani litawafanya watu waiogope burudani hii muhimu duniani.

Hivyo, kwa heshima, tunaiomba mahakama yako yafuatayo

a) Itamke kwamba ushindi wa Bayern wa magoli saba kwa mshangao haukubaliki na wala haukuwa muhimu (it was not warranted, unfounded, illegal and totally unacceptable). Ushindi wa magoli mawili ungetosha kabisa.

b) Itamke kwamba mpira sio ugomvi hivyo ni marufuku timu kuifunga timu nyingine zaidi ya goli tatu bila

c) Itamke kwamba kwa kuwa mpira ni urafiki, basi Bayern wawape Barcelona magoli mawili ili, for purposes of record, na kufita aibu ya mwaka, ubao usomeke 5-2!

d) Kutokana na maumivu waliyoisababishia jumuiya ya kimataifa, wachezaji wote wa Bayern waliofunga au kutengeneza goli la tatu mpaka la saba wafungiwe maisha maana walifanya hivyo kwa makusudi wakijua wenzao hawana hata goal moja.

e) Kila mechi ambaya Bayern imefunga zaidi ya magoli matatu, magoli yaliyozidi yaondolewe na kupewa Barcelona

f) Mahakama iiamuru Bayern kulipa gharama za kesi hii

g) Mahakama itoe adhabu nyingine yeyote inayoona kuwa inafaa kwa wanyama hawa wa Bayern[/h]IT IS A JOKE, DONT TAKE IT SERIOUSLY
 
Teh teh kwi kwi kwi
Wazee wa chenga 1000 wamenuna sana
maana jana hakuna rangi wameacha
kuona,ni kama kutembea uchu ukakutana
na Mkweo.

Ilikuwa ni kipiga cha Paka dokozi yaani
7 o'clock ,NIL

Haaaaa haaa haaa
walikuwa wanasema watashangaza Dunia
lakini si hii ya Dijitali labda warudi Analojia
.
 
MESI.jpg Hajielewi....Hii ni kwa hisani ya watu wa............
 
Namalizia kwa hisani ya watu marekani !

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom