Aliyoongea Mashishanga yalikuwa mawazo yake na alistahili kutumia uhuru wake.Lakini huyu mzee mashishanga ni mzee makini kuliko kawaida.Ni yeye mtanzania pekee aliyeweza kupaza sauti ya kumkataa kikwete akijua fika kuwa hawezi kuiongoza nchi na aliweza kusimamia hilo na ndiyo maana hakubadilika hata JK alipoteuliwa hadi alipoachwa kuteuliwa na akakubali kwenda kuchunga ng'ombe morogoro.Mzee mashishanga ni msukuma ambaye hababaiki na hana unafiki na ndiyvyo walivyo wasukuma wengine.Usukumani kwa sasa CCM haikubaliki na JK analijua hilo na wasukuma walishamfikishia ujumbe huo JK.Kwa sasa wanajua rais wa nchi ni Dr.slaa na huo ni msimamo wao hawatabadilika kama ambavyo wameamua CHEYO kuwa mbunge wa kuajiriwa na si wa kuchaguliwa, kwa Mzee mamose CCM hawatii timu wanajua aibu wanazovuna kila mwaka wa uchaguzi na sasa usukuma yote imegeuka hivyo kwa kulalia kwa Dr.slaha kama anavyojulikana usukumani.
Kwa wasiowajua wasukuma wao wako tayari kumfanyia ukarimu hata aduai yao, watacheka na wewe sana, lakini ukifika wakati wa kuamua nini kifanyike watakuambia msimamo wao kuwa ni tofauti na wako, lakini ukarimu utapata.Hiki ndicho kinachoipata CCM kwa sasa usukumani, Nape anapokelewa kwa shangwa kama mgeni lakini ukifika wakati wa kupiga kura watamuonyesha wako upande gani!!!!!! Hawa watu wanachana live hawaumi maneno.Aliyofanya mashishanga alikuwa anawafariji wana-ccm lakini mzee yule si wa ccm tena, ukifanikiwa kuona anachokifanya kwenye sanduku la kura ndiyo utaamini maneno yangu.Yaya lulu nalemaga!!!!!!