A
Anonymous
Guest
Habarini, naleta taarifa hii kwa masikitiko makubwa sana kwa mara nyingine tena kwa sababu jambo hili sio mara ya kwanza kuripotiwa
Mashine ya MRI (Magnetic resonance imaging) katika Hospitali ya Mloganzila ni mbovu takribani mwezi mmoja na nusu na hali ni mbaya, wagonjwa wengine inawapasa wapange foleni katika kupata huduma hii tena kwa kusubiri masaa mengi sana... Foleni hiyo sio hapo hapo hospitalini TU bali ni katika hospitali ya Taifa Muhimbili iliyopo Upanga
Ni aibu kwa Hospitali yenye hadhi ya TAIFA kama Mloganzila kukosa huduma hii muhimu, pamoja na jitihada za Mheshimiwa Rais kukuza sekta ya afya lakini kuna baadhi ya watendaji wanamuangusha. Kwa inavyoonekana kuna watendaji wazembe (Wakurugenzi na wakuu wa idara) hapo hospitalini wanasababisha Mashine hii kuharibika na kutofanyiwa matengenezo kwa wakati (Wakibisha ushahidi nitauweka hewani kwa sababu upo)
Wagonjwa wanahamishwa kutokea Muhimbili Mloganzila kwenda Muhimbili Upanga jambo ambalo ni usumbufu kwa wagonjwa wengine inawabidi wasile siku nzima kusubiria kipimo lakini mwisho wa siku hawafanyiwi, sasa kushindishana njaa siku nzima maana yake nini? Hii ni sawa kweli?
Vile vile wagonjwa wengine wanatoka mbali sana mwisho wa siku wanaamua kuondoka,kukesha hospitali na wengine kukata tamaa ya kupata huduma kwa sababu kunakuwa na mlundikano wa wagonjwa wanohitaji kipimo hicho kutoka Muhimbili Upanga na Muhimbili Mloganzila
Pia kwa kuwa Mloganzila wana mashine moja ya MRI napendekeza au kushauri waongezewe mashine nyingine ya MRI ili watoe huduma stahiki kwa wakati
Tunapaza sauti suala hili lifanyiwe kazi haraka na mashine ya MRI irudi kwenye hali yake ya kawaida.
ASANTE