Mashindano ya ubora wa bangi

Mashindano ya ubora wa bangi

Zinduna

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2011
Posts
2,378
Reaction score
3,392



Huu si mzaha, bali ndiyo ukweli wenyewe. Mashindano hayo ya kushindanisha ubora wabangi yanayofanyika kila mwaka yakihusisha miji kadhaa ya Ulaya na Marekani ambapo yamejizolea umaarufu zaidi katika jiji la Amsterdam nchini Uholanzi yatafanyika hivi karibuni.

Mashindano hayo hukutanisha wadau wanaotumia uraibu huo ambapo wanapata fursa ya kujaribu bure aina mbailmbali za Bangi zilizoletwa na wakulima wanaolima bangi kutoka pande mbalimbali za dunia na kisha kuchagua iliyo bora kuliko zote.

Labda unaweza kushangaa zaidi kwamba mashindano hayo huwa yanafadhiliwa na gazeti moja maarufu linaloitwa HIGH TIMES na mashindano hayo yamekuwa yakifanyika kwa miaka takriban 27 sasa.

Mashindano hayo ambayo yamejizolea umaarufu yanajulikana kama The Cannabis Cup na kwa jiji la Amsterdam nchini Uholanzi yatafanyika kuanzia tarehe 23 mpaka 27 Novemba 2014 na kwa nchini Marekani yatafanyika tarehe tofauti tofauti kwa kila mji na yatahusisha miji yote huku yakipambwa na matamasha ya wanamuziki maarufu watakaoalikwa kutumbuiza.

Kwa wale wakulima wa uraibu huo watakaotaka kushiriki katika mashindano hayo wanaweza kujipatia tiketi za kushiriki kupitia mtandao wa Cannabiscup.com

Kwa maelezo Zaidi mnaweza kupitia mtandao huu:

http://remainintheknow.blogspot.co.uk/2014/11/high-times-cannabis-cup.html.

CC:
Asprin, Jiwe Linaloishi, Kipaji Halisi, DEMBA, Karucee, miss chagga, lara 1, miss neddy, charminglady, Tumboo, Madame B, cacico, King'asti, Elizabeth Dominic, miss strong, Kibo10, mdida, tinna cute
 
Last edited by a moderator:
Ngoja nipeleke cha Tarime yaani unakitoa shambani kibichi na cha kijani halafu unachimba shimo unaweka matawi ya migomba chini unaweka kitu unamalizia na matawi unafukia siku saba baada ya hapo unakitoa kinakuwa kimeiva kimeiva kimekuwa cha njano unakitoa unakipeleka unakiweka

kwenye choo shimo ndani mpaka kinanyauka na kukauka ukikitoa hapo mtu akavuta lazima avue nguo Asante bhangi umetusomesha wengi na hauna madhara mengi kama sigara.
 
Ngoja nipeleke cha Tarime yaani unakitoa shambani kibichi na cha kijani halafu unachimba shimo unaweka matawi ya migomba chini unaweka kitu unamalizia na matawi unafukia siku saba baada ya hapo unakitoa kinakuwa kimeiva kimeiva kimekuwa cha njano unakitoa unakipeleka unakiweka kwenye choo shimo ndani mpaka kinanyauka na kukauka ukikitoa hapo mtu akavuta lazima avue nguo
Asante bhangi umetusomesha wengi na hauna madhara mengi kama sigara.


Weweeeee kuna CHA ARUSHA acha bana
Wapi Preta, Arushaone, PakaJimmy, Mzee wa Rula, Filipo, Erickb52
 
Last edited by a moderator:
maisha yetu ya kila siku yanapelekwa na ndum,i like out door skunk.:smokin:
 
Moro kitu cha Doma usipime!! Arusha kitu cha Ngaramtoni na Kisimiri usipime!! Afu kuna kitu cha Malawi
 
'Jani likulie milimani kwenye baridi na maeneo ya mawe mawe....au miamba....' pafu moja tu kama unaanza uvutaji, unafyatuka palepale nakuanza kutembea umeina ukiulizwa kwa nini unatembea umeinama unawajibu...nyie hamuoni hiyo mbingu ilivyo karibu nikitembea wima wima sitanigonga kichwa.!!

UVUTAJI WA BANGI NA UTUMIAJI WA AINA NYINGINE YA MADAWA YA KULEVYA NI HATARI KWA AFYA YAKO YA MWILI NA KIAKILI; PIA NI HATARI KWA NDUGU ZAKO JAMAA ZAKO, KIZAZI CHA SASA NA VIZAZI VIJAVYO.

KOMESHA KWA NGUVU ZOTE MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA
 
'Jani likulie milimani kwenye baridi na maeneo ya mawe mawe....au miamba....' pafu moja tu kama unaanza uvutaji, unafyatuka palepale nakuanza kutembea umeina ukiulizwa kwa nini unatembea umeinama unawajibu...nyie hamuoni hiyo mbingu ilivyo karibu nikitembea wima wima sitanigonga kichwa.!!

UVUTAJI WA BANGI NA UTUMIAJI WA AINA NYINGINE YA MADAWA YA KULEVYA NI HATARI KWA AFYA YAKO YA MWILI NA KIAKILI; PIA NI HATARI KWA NDUGU ZAKO JAMAA ZAKO, KIZAZI CHA SASA NA VIZAZI VIJAVYO.

KOMESHA KWA NGUVU ZOTE MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA

Bangi ni tiba, bangi ni starehe, bangi ni ibada na mwisho bangi SIO madawa ya kulevya. Mtoto koma!
 
Back
Top Bottom