jebs2002,
Ama kwa hakika hii ni moja katika mada nzuri sana nilizopata kuziona humu JF, nakupa pongezi kwa hilo.
Watoto wa kike wa Kitanzania, Waislaam kwa Wakristo, walio na dini na wasio na dini. Wanatembezwa nusu uchi wakionesha uzuri na haiba za kwa maslahi ya wengine zaidi. Kama si utumwa ni nini?
Ukitazama hayo makampuni yanayo dhamini hayana zaidi ila ni kuhakikisha wanatangaza biashara zao kupitia watoto zetu wakike, wakipita kuonyesha maungo yao na jinzi walivyoumbika. Jee, kama huu si utumwa ni nini?
Tunaiga mambo ambayo si mila wala za Kitanzania wala za Kikristo wala za Kiislam ni za kishetani. Hao watoto maskini ya mungu utakuta wana support yote kutoka kwa wazee wao. Jee, ni tamaa ya maisha, ulimbukeni au ni ujuha unaowapelekea wazee wa hawa watoto kuona kuwa wanafanya cha maana wanapofikia kuwauza watoto zao kwa njia hii?
Halafu wengine utaona wakishindwa hujiliza kwa uchungu wa kukosa. Na wanaoshinda utaona eti wanajiliza kwa furaha! Ni nini wanacholilia? kukosa fedha za ushindi au furaha ya kuwa sasa watakwenda kuanikwa zaidi?
Halafu kinachokera zaidi ni pale viombo vya habari vinapowafanya hawa kuwa ni mabalozi wa mambo mema na kuwapeleka sehemu za kulelea watoto wadogo ili waige dada zao wanafanya nini.
Hii ni laana na ushetani na siungi mkono hata kidogo. Ndio hayo, leo mwanao anapita nusu uchi anajianika wewe mzee wake unashangilia. Khaaa.
ayo makampuni kama voda na mengine sio ya kulaumiwa, wao wako kimaslahi zaidi. Wakuwalaumu ni hao wanaoshiriki.
makampuni yanataka kutangaza bidaa zao kupitia mradi huo, yenyewe yamekosa nini ? hao watoto wa kike hawana wazazi,binafsi mwanangu kwa ruksa yangu hawezi,lakini kwa maamuzi yake siwezi kumzuia akiprove kwamba she is grown up and can take her own course in life...
Mtoa mada asante sana kwa kuling'amua hili,na cha kuongezea si kwenye umiss tu hata kwenye matangazo ya biashara,wanawake ndio wanaotumiwa sana,hebu fikiria tangazo la sigara lakini mwanamke lazima awekwe pale,ila kinachofanya tuwe hapa ni kwa sababu ya Ubepari,mfumo huu ndio unaofanya mwanamke adhalilishwe sana,kwa sababu BEPARI huangalia fursa,tazama hayo makampuni yanayodhamini,yoooote ni ya kibepari,wanaamin bila kumtumia mwaamke hakuna faida,pili angalia waandaaji,mwandaaji wa miss tanzania ni mwanaume na wa miss utalii ni mwanaume,angalia wanamitindo weengi ni wanaume,lakini wanawalenga nani???WANAWAKE,kingine ni kuikubali,kama watanzania wangeyakataa haya baasi hakuna ambae angeyaendekeza,lakin hata viongoz wetu wanaunga mkono,sijamsikia nchimbi akikemea hili,amekemea big brother tu,kwakuwa haipo TANZANIA,kwa mabinti nao wana tamaa zao,wanataka pesa,umaarufu na kuendesha magari,watafanyaje????kukubali kuuza utu wao ili wafikie malengo yao,hapo sasa!!!!!majaji ndio huwabeba,mda mwingine hata waandaaji,ajabu mashindano haya huwa na majaji wanaume,dah

makampuni yanataka kutangaza bidaa zao kupitia mradi huo, yenyewe yamekosa nini ? hao watoto wa kike hawana wazazi,binafsi mwanangu kwa ruksa yangu hawezi,lakini kwa maamuzi yake siwezi kumzuia akiprove kwamba she is grown up and can take her own course in life...

Ni kweli bwana bajabiri na uyasemayo, hasa kwa watoto wa kike kutaka kuendesha gari, kupata vihela labda vya kuanzisha biashara na kujikomboa. Lakini kwa makampuni kuwatumia mabinti zetu namna hii ni hatari sana. Mabinti zetu itakua rahisi kwao kufikiria kuwa haya mashindano ndio yatakayowatoa kwenye umaskini, si kweli, zaidi ya kuwaletea madhara.

Hatukatai kwa makampuni haya kutumia wanawake au wanaume, swala wanawatumia kwa njia zipi, kwanini wasi promote nembo na biashara zao kwa njia zilizotajwa nami na wadau wengine hapo juu?

Na hili swala la makelele mtaani ya promotions zao, litabidi nalo likomeshwe pia