Mashindano ya KUUCHUNA.

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Sep 2, 2011
4,873
1,216
Wanaume flani walikuwa wanatambiana kuhusu uwezo wao wa kuuchuna, wa kwanza akasema kuna siku alimpigia simu mkewe akapokea lakini hakusema hallo kwa hiyo nae akauchuna hakukata simu wala kuongea mpaka credit ikaisha, wapili akasema yeye kuna siku alirudi toka kazini baada ya kugonga mlango mkewe akafungua mlango lakini hakusema 'karibu mume wangu' basi akasimama palepale mlangoni mpaka kesho yake na akageuza na kurudi kazini, watatu akasema siku alipooa mkewe akawa anaona aibu kuvua nguo, na yeye akauchuna hakumgusa mapaka leo, wenzie wakamjia juu mbona mna watoto wawili, akajibu mpaka leo nimeuchuna sijamuuliza kawaokota wapi. Nani mkali?
 
Mkali mode kauchuna tu while thread hii inarudiwa mara ya pili



-device not compatible
 
Back
Top Bottom