Mashemeji wangapi?............

MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,470
6,562



Wapendwa,

Najiuliza hivi bado kuna wanaume wanaodanganywa kwa kubambikiziwa mashemeji/madada wa bandia kama anavyolalamika Mbaraka Mwinshehe hapa?

Je kuna limitation yoyote ya shemeji/ madada ambayo unafikiri mwenzi wako akikuintroduce au kuwa karibu nao unakuwa na wasiwasi?
(Kina dada kuna wale huyu ni mfanyakazi mwenzangu, dadayangu tunatoka kijiji kimoja n.k kuna mipaka?

Otherwise ..........enjoy the music!
 
Last edited by a moderator:
MJ1.... mara nyingi huwa na tabia ya kumjudge mtu kupitia watu alionae karibu sasa kama hao mashemej hawaeleweki wasiwasi lazima
 
MJ1.... mara nyingi huwa na tabia ya kumjudge mtu kupitia watu alionae karibu sasa kama hao mashemej hawaeleweki wasiwasi lazima
Loh chauro yaani nimejikuta tu ninajiuliza ama sivyo nahisi mapenzi ya siku hizi yako more westerned hahahah yaani mambo ya nuclear family mpaka kwenye mashemeji hahaha mashemeji zangu ni wale unaozaliwa nao tumbo moja mke wangu siwatambui sijui makaka zakeo upande wa baba waloshare shangazi aloolewa na rafiki yake baba hah
 
Watu wamekua wajanja sana siku hizi...
Wote wadanganya na wadanganywaji kwahiyo ni ngumu kidogo kumbambikia mtu ushemeji.
Yani wale wepesi kudanganya wanashindana na ugumu wa kuaminika hivyo hawawezi kurahisi uongo wao kwa kuwapachika wapenzi wao wa pembeni undugu wa damu.
 
Yaani kama ni kushuku utashuku wangapi? Mwishowe unasahau kufurahia raha za maisha unakuwa binti wasiwasi! Waje tu introduction mawifi kwa mafungu, kama wana ubaya wao watakuja umbuka mchana kweupee.kazi ya kuwasaka kina osama wataifanya wamarekani
 
MJ1.... mara nyingi huwa na tabia ya kumjudge mtu kupitia watu alionae karibu sasa kama hao mashemej hawaeleweki wasiwasi lazima

hahahahaaaa Chauro bana! Unatambulishwa Kipipi as mtoto wa ba'mdogo, basi ndo kila saa mmeo anapokea simu ya Kipipi, hajakaa hajapumua wifi yako Kipipi anakusalimia, mara utasikia honi wifi yako Kipipi kampitisha mumeo nyumbani! Khaaa!!! Ina maana Kipipi ka-occupy ndugu wote wa mumeo?? Lazima moyo ukwende mbio hata kama ulitambulishwa ni wifi!! (just thinking aloud, sijui nimechakachua manake MJ1 ameongelea mashemeji)
 
Inawezekana kabisa, lakini hiyo ni tabia ya baadhi ya watu. Ni ngumu kuhofia mashemeji ila jitahidi kuwa muangalifu kuchagua mwenza mwenye tabia nzr na mwenye hofu ya Mungu, na pia umuombe Mungu ktk hilo pengine itasaidia kupunguza hizo hofu ulizonazo na hatimaye kumpata mwenye tabia njema.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom