janja pwani
Senior Member
- Jul 27, 2011
- 104
- 9
wakiongea na kuwasiliana na masheikh wa mkoa wa tabora katika kipindi maalumu cha Radio IMANI wamesema kitendo alichofanya said kubenea kwa kuandika habari isiyokuwa na uhakika huku ni kuudhalilisha uislamu, katika habari "DC Fatuma kimario si muislamu" wamesema kwanza mwenyewe aliishasema "kwa mujibu wa dini yangu ya UISLAMU kitendo cha kunivua hijabu ni kama wameniwacha uchi" naye sheikh wa Mkoa anasema bi fatuma ni muislamu safi na huwa tunasali naye hapa msikitini na hata Ijitimayi iliyofanyika Nairobi mwaka jana tulikwenda naye, na shughuli zote za hapa msikitini huwa anashiriki hata usafi wa msikiti huwa anashiriki na wakina mama wenzie, siku ya ijumaa huwa anafika mapema hapa msikitini, kwa hiyo nashangaa mtu anaposema mama huyo ni Mkristo, alisema sheikh huyo wa mkoa wa Tabora.