Mashehe vs. Maaskofu: Tumegawanywa, Tukagawanyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashehe vs. Maaskofu: Tumegawanywa, Tukagawanyika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kisendi, Jan 21, 2011.

 1. K

  Kisendi JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 700
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  WIKI iliyopita vyombo vya habari viliandika kwa kina juu ya machafuko na mauaji ya Arusha.

  Kila kundi kati ya wanasiasa, viongozi wa dini, wana habari na hata wananchi wa kawaida, wanajadili suala hili kwa misisitizo tofauti.

  Tofauti za misisitizo zinaweza kutokana na ulevi wa itikadi fulani, ufinyu wa kuelewa, na hata umbali wa mtu na tukio lenyewe. Tofauti iliyojitokeza baina ya viongozi wa dini ya kikiristo na kiislamu katika suala la machafuko ya Arusha inasikitisha wengi.

  Viongozi wa dini kwa kawaida hutofautiana katika mimbari, lakini huunganishwa mahali popote penye harufu ya dhuluma na uonevu. Kilichotokea Arusha na kusababisha upotevu wa amani na uhai wa watu kilipaswa kiwaunganishe viongozi wetu wa dini badala ya kuwagawa.

  Mgawanyiko huu katika suala linalohusu uhai wa mwanadamu unawadhalilisha viongozi wetu wa dini na historia tu ndiyo itakayowahukumu. Hata mpagani asiye na dini, hawezi kuacha watu wanakufa, akaanza kushangilia anayewaua hata kama anayeuawa anaonekana ana makosa.

  Kwa nini tulijenga mahakama? Mbona tumesikia watawala na hata baadhi ya viongozi wa dini wakidai chama cha siasa kinachodhani kimeonewa katika uchaguzi kiende mahakamani? Kama mahakama inafanya kazi, kwa nini waandamanaji wasikamatwe wakapelekwa huko badala yake wanauawa?

  Nilijadili wiki iliyopita, haja ya Serikali kuunda tume huru ili isaidie kuweka sawa jambo hili. Nimesikia sasa Jeshi la Polisi ambalo ni watuhumiwa, ndilo limeunda tume ya “kujichunguza”. Hili ni kosa kubwa. Serikali imepoteza fursa ya maana sana kwa kushindwa kutumia tume iliyo huru katika suala linalohusu uhai wa raia wake.

  Tofauti za mtizamo katika suala hili zinaruhusiwa, lakini inatia shaka pale viongozi wa dini nao wanapotofautiana katika suala hili. Kinachoonekana wazi hapa ni tabia fulani ya viongozi wa dini kujifanya wao ndio wako zamu ya kupendwa na “bwana” mwenye wake wengi. Viongozi hao wanasahau kuwa wao si wa kwanza kupendwa. Ndoa ya viongozi wa dini na serikali, haijawahi kuwa ya kudumu mahali popote duniani. Wahenga walisema, ukiona mkwaju uliomtandika mke mwenza hapo jana, uokote na kuutupa mbali, maana yawezekana ukakutandika na wewe.

  Awali tulisikia viongozi wa dini ya Kikiristo jijini Arusha wakitoa tamko lililolaani mauaji ya raia, na likatoa mwongozo wa namna ya kutatua tatizo hili. Katika tamko lile, Serikali iliguswa, CCM iliguswa, CHADEMA iliguswa, na Polisi waliguswa. Katika mkutano na waandishi wa habari, Askofu Lebulu akaulizwa ikiwa viongozi wa dini wanamtambua Meya wa Arusha. Kwa kuzunguka sana, akatoa jibu lililomaanisha hawawezi kumtambua na wakabaki na heshima ya kuwa viongozi wa dini.

  Kinachoshangaza, ni kuwa baada ya hapo, wanasiasa wengi wameshikilia jibu hili lililoibuka hapo mkutanoni na kuacha mambo mengi ya muhimu katika tamko lile. Hii imekuwa kawaida ya watawala wetu, kuibua masuala yasiyo na msingi pale wanapobaini masuala ya msingi yanaanza kujadiliwa kwa umakini.

  Mathalani, tuliona siku ya kongamano la katiba mpya lililoandaliwa na UDASA, likaandaliwa kongamano jingine la mashehe kujadili tamko la maaskofu. Hizi ni njia za kitoto katika kushughulikia masuala ya kitaifa na zinaligawa Taifa badala ya kulileta pamoja.

  Watu wengi hivi sasa wanamung’unya maneno na kusema kuna “dalili” za mgawanyiko katika Taifa. Wanasisitiza kuwa dalili hizo zinaonekana zaidi katika suala la dini.

  Mimi natamka kimsingi kuwa, si dalili za kugawanyika, bali tumegawanyika tayari baada ya kukubali wenyewe kugawanywa na watawala wetu. Tunayo migawanyiko mingi, na huu wa kidini ni mdogo sana japo wa hatari.

  Magawnyiko wa msingi unaoonekana wazi ni huu wa Serikali kujichukulia likizo isiyo na utaratibu na kuliacha Taifa mikononi mwa wasanii. Serikali yoyote makini, ina wasemaji wake wanaofahamika na kazi yao ni kuisemea serikali kila wakati. Lakini hivi sana, hatuna msemaji mmoja wa Serikali hasa katika masuala ya msingi.

  Chukulia suala la machafuko ya Arusha yaliyosababisha mauaji ya watu watatu na kujeruhi wengi. Ndani ya wiki moja tumesikia kauli za Serikali kutoka kwa watu tofauti zikieleza masuala kwa namna inayoacha mashaka mengi.

  Waziri wa Mambo ya Ndani Shamsi Vuai Nahodha anasema vyake, Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Kamillius Membe anasema vyake, Kamishna wa Polisi Paul Chagonja akaja na yake, chama tawala kikaja na migawanyiko yake; Waziri Stephen Wasira akaharibu nauli yake kwenda Arusha bila maandalizi na hata Rais Jakay Kikwete akadokeza fikra zake zisizokidhi haja ya waathirika wa machafuko yale.

  Hali ya kila mtu kuwa msemaji wa Serikali inajitokeza kuashiria ombwe la uongozi ambalo limejadiliwa mara nyingi katika vyombo vya habari.

  Hebu tujiulize, maaskofu wakatoa tamko lao na kueleza msimamo wao dhidi ya Serikali na vyombo vyake. Mashehe nao wakaibuka na tamko lao kulaani maaskofu. Wazee wa Dar es Salaam wakaja na tamko lao kulaani maaskofu. Tamko la maaskofu halikuwalenga mashehe wala wazee wa Dar es Salaam, lakini mashehe na wazee wa Dar es Salaam wakawajibu maaskofu kana kwamba wao ni wasemaji wa Serikali.

  Serikali yetu ikasemewa na mashehe na wazee wa Dar es Salaam lakini kwa gharama kubwa ya kuingia katika mgongano na maaskofu. Maaskofu nao wanaweza kujiona wamedharauliwa na Serikali inayotumia mashehe kuwadhalilisha maaskofu.

  Mzunguko huu unasababisha vidonda pande zote tatu: Serikali inawanunia maaskofu wanaoisema; maaskofu wanainunia Serikali inayowadharau na kuwapuuza; mashehe wanawanunia maaskofu wanaoisema serikali “yao” wanayoipenda na kuitetea kwa gharama ya kukosana na viongozi wa dini wenzao; na maaskofu wanawanunia mashehe kwa kuiteka Serikali na kuisemea kwa mambo ya msingi.

  Wakati haya yanapotokea hatuelezwi masuala ya msingi katika machafuko haya ya Arusha. Mashehe hawatuelezi kama wanaunga mkono mauaji yale, badala yake wanakuwa kama wanamaanisha kuwa, kwa vile watu walikufa Mwembechai na Zanzibar, basi acha hata hawa wafe!

  Mashehe hawatuelezi wazi lakini wanakuwa kama wanamaanisha kuwa, kwa vile CUF iliibiwa kura 2001 na Amani Karume akatangazwa Rais wa Zanzibar, basi, acha hata huyu Meya wa Arusha ambaye utaratibu wake wa kuchaguliwa ulikuwa na kasoro, acha awe Meya tu!

  Dhana hii ya wote tukose ni ya hatari na inalimbikiza visasi visivyo na tija kwa Taifa. Mashehe hawatuelezi ikiwa wako tayari kuupokea utamaduni wa matumizi ya nguvu za dola dhidi ya raia wanaoeleza fikra zao kwa uhuru katika Taifa huru. Hata kama mashehe wana tatizo na CHADEMA kama chama, au wana tatizo na Dk. Willibrod Slaa kama mgombea Urais aliyeshindwa, wanapaswa waone ng’ambo ya tofauti zao na watu binafsi ili kujijengea hata huo uhalali wa kuisemea Serikali.

  Nalisema hili kwa sababu, mashehe hawa wanapaswa kujua kuwa hakuna dola (serikali) isiyodhulumu. Hata katika nchi zinazotawaliwa kwa misingi ya dini, bado kuna wanaharakati na watetezi wa wanyonge.

  Serikali hii wanayoisemea leo, kesho inaweza kuja na jipya la kuwaudhi mashehe na hapo ndipo watakapojikuta njia panda. Serikali na watawala wanaowaambia maaskofu kuvua majoho, hawawezi kuwaheshimu mashehe kwa vile tu katika suala la machafuko ya Arusha walisimama kidete kuitetea Serikali – tena inawezekana hiyo imefanyika baada ya Serikali yenyewe kwa siri kuwaomba waisemee.

  Huu ni uswahiba wa muda na wa bandia uliojengwa katika maslahi yanayopita. Mimi naamini kuwa hata serikali dhalimu ina wajibu wa kuwaheshimu viongozi wote wa dini kwa sababu uhalalali wa dola yoyote ni zaidi ya ushindi wa kwenye sanduku la kura.
   
 2. K

  Kisendi JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 700
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Mimi nafikiri kuna watu wanatumwa, Kwani kusemea serikali ni Kosa, Mashehe wanatuboa
   
 3. P

  PWAGU Member

  #3
  Jan 21, 2011
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Iliposemwa siasa isichanganywe na dini watu wengi hawakuelewa maana yake. Sasa tunaona maaskofu wakisema hiki, masheikh wanasema kile.kwa kifupi hakukuwa na sababu ya maaskofu kusimamia directly upande wa upinzani pia hakuna sababu ya masheikh kuisimamia serikali, yote haya ni malumbano ya dini.
  Kwa mwenendo huu hata kwenye katiba tutashuhudia vurugu kubwa kati ya watu wa dini. Hivyo watu wa dini wasiingie direct kwenye siasa wabaki kuwa washauri na siyo kama wanavyofanya sasa.
   
 4. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Hii ni misconcemption. Kwa hiyo ikitokea chama fulani kinasema ukweli ambao unakubalika na dini basi tuchukulie kuwa chama hicho kinaungwa mkono na dini????

  Kwa hiyo hapa tuseme mashehe (which implies na "dini" wanayoisimamia hali kadhalika) wanaunga mkono mauaji? On a second thought may be this is the case in relation to what happened in Arusha.
   
Loading...