Mashauriano ya kiroho: Hifadhi hii mada itakusaidia kwa mengi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,869
Reaction score
828,386
Naweka summary/reviews za mada nyingi nilizoandika na kushauriana na watu mbali mbali ndani na nje ya JF.. Sina ruhusa yao hivyo siwezi kumtaja yoyote
Nitakaribisha na maswali pia

1. Tiba ya kiroho yenye nguvu iliyobaki ni tiba ya chumvi ya mawe maana mpaka sasa haijanajisiwa wala kuchakachuliwa

2. Wakatae madalali wa ulozi na ushirikina.. Wale wanaokusifia kwamba mganga fulani ni kiboko.. Wakati huyo anayekusifia umemzidi vingi

3. Epuka kafara ya aina yoyote hasa ya kumwaga damu.. Unatengeza madhabahu itakayobeba roho zitakazokutesa sana!

4. Epuka waganga wa mazingaombwe.. Kumbuka mganga ni mchawi pia.. Anaweza kukufanyia michezo ili aendelee kukutumia

5.Epuka kuchanganya falme mbili.. Ufalme wa nuru na ufalme wa giza! Badala ya kusaidika utazidi kuharibikiwa maana falme hizo zitatumia mwili wako kama uwanja wa mapambano

6. Usikubali kupeleka mnyama wa mnyama yeyote.. Mganga atafaidi nyama wewe utafungamanishwa na roho ya huyo mnyama

7. Usidanganywe na visomo. Utapoteza muda na mali.. Kisomo cha kweli kina maandalizi magumu na kila mshiriki anapaswa kuwa msafi mno kiroho asiye na mawaa

8. Epuka kupakwa madawa kuchanjwa chale na kuvukizwa mafusho ya giza. Unaunajisi mwili wako na kuufanya makazi ya maroho

9. Usijaribu kufanya zoezi lolote la kuitisha pesa za majini kwa maelekezo ya mganga.. Utageuzwa mateka kwenye ulimwengu wa roho

10. Usijaribu kamwe kufanya ibada, tambiko ama uganga unahusisha ngono! Ulinzi, uasherati na ulawiti ili ufanikiwe! Hupati tiba hapo bali unakaribisha mapepo machafu ya kila aina

Mwili wako ni helaku takatifu uliosimwikwa kwenye ardhi uliyopewa na Muumba wako! Kitendo chochote cha kutaka kutumia nguvu kutoka nje yake ni sawa na kukaribisha uvamizi uliojaa najisi na kuharibu utakatifu wa hekalu

Unapopata shida yoyote ya kiroho tumia utakaso kinga na uamsho wa chumvi ya mawe
Achana kabisa na clip za mitandaoni zinazofundisha mambo ya giza! Badala ya kukusaidia zitakumaliza
Naweka kituo hapa... Karibuni sana!
 
naomba ufafanuzi kwenye hii point.
hizo pesa za majini zikoje ?
 
Kuna watu wanadanganywa kwamba kuna majini yanagawa pesa! Lakini hakuna shuhuda hata mmoja zaidi ya story za mitandoni
Jini haamrishwi na binadamu bali yeye huchagua wa kumpa
Ikitokea kweli ukapata hizo pesa utaishi kwa masharti na maelekezo ya aliyekupa.. Utakuwa sio wewe tena

Majini: Viumbe vyenye roho hatari na wivu uliopitiliza | JamiiForums Majini: Viumbe vyenye roho hatari na wivu uliopitiliza
 
Naweka summary/reviews za Nada nyingi nilizoandika na kushauriana na watu mbali mbali ndani na nje ya JF.. Sina ruhusa yao hivyo siwezi kumtaja yoyote
Nitakaribisha na maswali pia

1. Tiba ya kiroho yenye nguvu iliyobaki ni tiba ya chumvi ya mawe maana mpaka sasa haijanajisiwa wala kuchakachuliwa

2. Wakatae madalali wa ulozi na ushirikina.. Wale wanaokusifia kwamba mganga fulani ni kiboko.. Wakati huyo anayekusifia umemzidi vingi

3. Epuka kafara ya aina yoyote hasa ya kumwaga damu.. Unatengeza madhabahu itakayobeba roho zitakazokutesa sana!

4. Epuka waganga wa mazingaombwe.. Kumbuka mganga ni mchawi pia.. Anaweza kukufanyia michezo ili aendelee kukutumia

5.Epuka kuchanganya falme mbili.. Ufalme wa nuru na ufalme wa giza! Badala ya kusaidika utazidi kuharibikiwa maana falme hizo zitatumia mwili wako kama uwanja wa mapambano

6. Usikubali kupeleka mnyama wa mnyama yeyote.. Mganga atafaidi nyama wewe utafungamanishwa na roho ya huyo mnyama

7. Usidanganywe na visomo. Utapoteza muda na mali.. Kisomo cha kweli kina maandalizi magumu na kila mshiriki anapaswa kuwa msafi mno kiroho asiye na mawaa

8. Epuka kupakwa madawa kuchanjwa chale na kuvukizwa mafusho ya giza. Unaunajisi mwili wako na kuufanya makazi ya maroho

9. Usijaribu kufanya zoezi lolote la kuitisha pesa za majini kwa maelekezo ya mganga.. Utageuzwa mateka kwenye ulimwengu wa roho

10. Usijaribu kamwe kufanya ibada, tambiko ama uganga unahusisha ngono! Ulinzi, uasherati na ulawiti ili ufanikiwe! Hupati tiba hapo bali unakaribisha mapepo machafu ya kila aina

Mwili wako ni helaku takatifu uliosimwikwa kwenye ardhi uliyopewa na Muumba wako! Kitendo chochote cha kutaka kutumia nguvu kutoka nje yake ni sawa na kukaribisha uvamizi uliojaa najisi na kuharibu utakatifu wa hekalu

Unapopata shida yoyote ya kiroho tumia utakaso kinga na uamsho wa chumvi ya mawe
Achana kabisa na clip za mitandaoni zinazofundisha mambo ya giza! Badala ya kukusaidia zitakumaliza
Naweka kituo hapa... Karibuni sana!
Kwahiyo wale wanaodai kuwa na pesa nyingi wanazopata kwa njia za asili au waganga sio uhalisia mkuu
 
Sio kweli kwanza hizo pesa hazitangazwi.. Wengi wanalipwa illi kuongea shuhuda za uongo
 
Unaweza kudhani ni habari za kufikirika au za redio mbao lakini hili pepo la chuma ulete lipo na linafanya mambo yake ila ni pepo Fukara na la kipuuzi kabisa

Chuma ulete halikupi utajiri wala mali za maana chuma ulete halitaki vitu vizuri chuma ulete halitaki elimu wala maarifa chuma ulete ni pepo chafu lenye mzio na usafi

Ukitembelea maduka ya wahindi kariakoo na posta na miji mingine yenye hii kabisa hutakosa kuona wamefunga kamba yenye majani ya mwembe na wengine kufuga kasuku(msema kweli na msema chochote) hawa wanaamini kuwa hiyo ni dawa ya chuma ulete

Kwa wale wasiojua chuma ulete ninini iko hivi unafanya biashara tangu asubuhi mpaka jioni unauza kama kawaida lakini inapofika wakati wa kufunga mahesabu pesa iliyopo na tofauti na vitu ulivyouza au ulikuwa na laki moja mfukoni anatokea mtu na kukuomba chenchi unampa lakini baadae kila ukipiga mahesabu haibalance..! Hiyo ndio chuma ulete

Pepo la chuma ulete linakaa kwenye noti unayopewa na mhusika mara nyingi akitaka chenchi hapo ndio chuma ulete hufanya kazi vizuri na kwakweli chuma ulete ni mazingaombwe tu ambayo hayana faida yeyote kwa mmiliki zaidi ya kumpatia vitu vya kipuuzi kabisa na vya kifukara

Chuma ulete ni pepo lisilo na faida kwa mmiliki lakini lakini likimtia hasara mlengwa ndio maana chuma ulete ni maarufu zaidi uswahilini kwenye biashara za kawaida kuliko zile biashara kubwa kubwa zenye faida nono na kwakweli chuma ulete ni kitu cha kufikirika zaidi kuliko uhalisia
 
Sawa @M
shana Jr, mwalimu wa mambo ya kiroho.

Kipekee sana napenda kukiri kuwa miaka ya 2012 - 2018, nilikuwa ninasona karibu mada zako zote na kupinga ulichiandika, kisa tu mengi yalikuwa ya kichawi chawi na sikuwa naamini kama uchawi upo/una nguvu.

Baadaye mada hizo zimekuwa za msaada sana katika maisha yangu hasa kukwepa vimitego vya kichawi chawi.

Keep it up.
 
Asante sana mkuu Baluma
 
Hivi hii chuma ulete ningependa kuilewa zaidi, huyo mtu anachukuaje pesa ya mwingine? Yaani aliyekuwa na laki yake haioni, huyo amechukua anaiba au anaipataje iwe yake na kuitumia?

Lingine kuna ile watu nilisikia wakisema kuwa na mtu katibu wao wanafanikiwa kwa kumtumia target yao bila yeye kujijua.. Target anakuwa hafanikiwi Mtu au watu wajuayo nini kinaendelea wanafanikiwa. Target anakuwa nao kila mahala yaani haijui hata pesa zake anatumia juu ya mtu huyo yeye hajui ni maisha magumu ila anajiona hao ndio wanamuweka kijijini alipo. Shamba mazao akiuza anakuwa bado kama masikini kila pesa eti inafaidisha maadui bila kujijua.. Hii nayo ipoje?
 
Back
Top Bottom