Mashati ya Batiki kwa bei rahisi.

Mashati ya Batiki kwa bei rahisi.

Secret Star

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2011
Posts
1,857
Reaction score
2,088
Kuwa mzalendo kwa kuvaa nguo za kiafrika..
Toleo jipya la Mashati ya Batiki limetoka
Wahi ujipatie shati kwa size na rangi upendayo kwa Tsh 42,000 tuu!!


IMG-20140724-WA0001.jpg IMG-20140724-WA0000.jpg IMG-20140724-WA0002.jpg

Kama unahitiji oda maalum unaweza kuniPM
 
acha wizi weweeee..hamna boya humu... wenzio wanauza hizo tshirt elfu 18-20.. na bado watu wanakimbia..
 
wizi mtupu,
hizo tshirt ni sh 7000 bei ya jumla,


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu hizo za 18-20 zinapatikana wapi? Nazihitaji

Kuna huyu jamaa aliweka bandiko lake facebook.. leo umenipa kazi ya kulichimbua..maana nsingekujibu ningeonakana muongo..FUNGUA ATTACHMENT HIYO
 

Attachments

  • 1406535667012.jpg
    1406535667012.jpg
    60.2 KB · Views: 406
safi saana Babu Kidude,Vanmed,Fisher nk,jamaa anafikiri fesha zinaokotwa tuuu

Watu huwa wanadhani hili ni soko la watalii walio out of touch na realities za nchi hii, angetoa bei ya kawaida saa hizi angekuwa anahesabu faida na mimi ningekuwa mteja wa kwanza, sasa yeye kajiona mjanja kuliko mtu yeyote matokeo yake thread yake haina maana.
 
Watu huwa wanadhani hili ni soko la watalii walio out of touch na realities za nchi hii, angetoa bei ya kawaida saa hizi angekuwa anahesabu faida na mimi ningekuwa mteja wa kwanza, sasa yeye kajiona mjanja kuliko mtu yeyote matokeo yake thread yake haina maana.

Huwa nachukia..mtu akinichukulia mjinga tena mbaya zaidi kwenye kuniumiza kinamna yoyote ile... sasa huyu jamaa aliona humu kuna mazunde kibao atu'take for granted.. pathetic
 
Huenda kichwani haupo sawa, Nenda kawauzie wajinga wenzio. 42,000/=???!!! Wenzako wanauza 18 na zina chacha. Nyambaf......uuuuuu.
 
kama hamna pesa mnyamaze msitukane biashara za watu hii ni biashara huria.Nyie ndio mtaweza kununua ticket ya kumuona Kansiime laki 7 kwa meza!!

mtoa mada/mleta tangazo usikate tamaa wenye pesa watakupm.
 
kama hamna pesa mnyamaze msitukane biashara za watu hii ni biashara huria.Nyie ndio mtaweza kununua ticket ya kumuona Kansiime laki 7 kwa meza!!

mtoa mada/mleta tangazo usikate tamaa wenye pesa watakupm.
Stunah hata kama ni soko huria huyu kapitiliza ila siungwi mkono atukanwe ...aelimishwe kuwa kuna bidhaa kama zake sokoni ,hivo ajipange
 
kama hamna pesa
mnyamaze msitukane biashara za watu hii ni biashara huria.Nyie ndio
mtaweza kununua ticket ya kumuona Kansiime laki 7 kwa meza!!

mtoa mada/mleta tangazo usikate tamaa wenye pesa watakupm.

Kuhoji uhalali wa bei ya kitu si kutokuwa na pesa, bei ya kitu inapaswa kulingana na vitu vya aina yake katika soko, ni ujinga kununua kilo ya unga wa mahindi kwa 5000 kwenye duka la vyakula wakati inaeleweka kuwa unga huo unauzwa kote kwa bei isiyozidi sh. 1500.
Kingine ni kuwa bei ya kitu inapaswa kulingana na ubora wake na si kuuziwa kitu cha ubora wa kawaida au wa chini kwa bei kubwa kisa eti una hela ya kulipa. Hii inaexclude exceptional cases kama pale bidhaa inapokuwa inauzwa katika eneo ambalo muuzaji analipia pango kubwa kupita kiasi kitu kinachomlazimu kufidia gharama kwa kupandisha bei ya bidhaa zake kidogo tofauti na zile zinazouzwa maeneo mengine.
Kingine ni kuwa 700,000 inaweza kuwa hela nyingi sana kwako lakini ni hela ya kawaida sana ila kuitoa kwenda kumwangalia Kansiime ni maamuzi binafsi kwani si wote wanaovutiwa na shoo za mtu kama yeye ambae kwako anaweza kuwa mtu wa ajabu sana. Karibu
 
Back
Top Bottom