Mashamba ya kulima Ruvu

Mashamba ya kulima Ruvu

Twin_Kids

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2016
Posts
3,997
Reaction score
5,969
Habari zenu.
Nimewahi kuuliza swali kuhusu mashamba ya kulima Ruvu,nikabahatika kupata maelezo,nikaenda na nimeanza. Lakini,uzi ulioniongoza nimeutafuta sijauona,ila nimetumia muongozo niliopewa.

Ruvu kwa kweli kama una nia ya kulima ni pazuri,maji yapo ya uhakika,mito ni miwili, Ruvu na Msuya.

Pamoja na hayo lakini kuna changamoto kubwa mbili:
1.Usimamizi unahitajika na kama umeamua,hamia au tafuta mtu wako wa karibu.Wajanja huku ni wengi,tena bora niwaite wahuni.Ukituma hela kwamba kazi utafanyiwa utaishia kulia tu.

2.Upatikanaji wa mashamba:
+255 658 899 195.Kuna mtu siku za nyuma alitoa hii number kwamba atafutwe mwenye nayo,atawapa maelezo.Hakika aliyepost hii number wanashilikiana asilimia mia.

Jamani,mtu kama yule unawezaje kuomba watu,walioacha familia zao,wampelekee pesa,awatapeli? Nawasihi sana,nimeona mengi.

Kama unataka shamba huko,kuna sehemu mbili.Kuna kilimo cha mpunga,kinafanywa na shirika,huyu anawapeleka watu na kuwauzia mashamba ya watu,mwisho wa siku mnaishia kugombana na hela unapoteza. Anauza shamba lililopandwa mpunga kwa laki 5,na lisiti atakupa. Za kughusho,mwisho wa siku unakumbana na mwenye shamba sasa.

Kama umeamua kulima huko,nenda ofisini,gharama za ofisi ni 442,000(pesa ya kukodi shamba kwa mwaka,unalimiwa,unapewa maji,mbegu ya mpunga ni ya kwao unauziwa kiasi kidogo si kama madukani nje,mbolea ni za ruzuku,ukihitaji utapewa kwa gharama nafuu)Ukipita pembeni shauri yako.Labda uonane na mwenye shamba mtajuana wenyewe lakini kupitia mtu mwingine utalia.

Mashamba mengine unakodi kwa watu,na kama utakodi la hivo,hakikisha mnaandikishana kwenye uongozi wa kijiji.Tofauti na hapo,utajua mwenyewe.

Ukihitaji maelezo zaidi,nambie,kama kukusindikiza ntakusindikiza,ugharamie usafiri. Ila, kama hujajipanga kulima,usiharibu hela yako.
 
Habari zenu.
Nimewahi kuuliza swali kuhusu mashamba ya kulima Ruvu,nikabahatika kupata maelezo,nikaenda na nimeanza.
Lakini,uzi ulioniongoza nimeutafuta sijauona,ila nimetumia muongozo niliopewa.
Ruvu kwa kweli kama una nia ya kulima ni pazuri,maji yapo ya uhakika,mito ni miwili,Ruvu na Msuya.
Pamoja na hayo lakini kuna changamoto kubwa mbili:
1.Usimamizi unahitajika na kama umeamua,hamia au tafuta mtu wako wa karibu.Wajanja huku ni wengi,tena bora niwaite wahuni.Ukituma hela kwamba kazi utafanyiwa utaishia kulia tu.
2.Upatikanaji wa mashamba:
+255 658 899 195.Kuna mtu siku za nyuma alitoa hii number kwamba atafutwe mwenye nayo,atawapa maelezo.Hakika aliyepost hii number wanashilikiana asilimia mia.
Jamani,mtu kama yule unawezaje kuomba watu,walioacha familia zao,wampelekee pesa,awatapeli?
Nawasihi sana,nimeona mengi.
Kama unataka shamba huko,kuna sehemu mbili.Kuna kilimo cha mpunga,kinafanywa na shirika,huyu anawapeleka watu na kuwauzia mashamba ya watu,mwisho wa siku mnaishia kugombana na hela unapoteza.Anauza shamba lililopandwa mpunga kwa laki 5,na lisiti atakupa.Za kughusho,mwisho wa siku unakumbana na mwenye shamba sasa.Kama umeamua kulima huko,nenda ofisini,gharama za ofisi ni 442,000(pesa ya kukodi shamba kwa mwaka,unalimiwa,unapewa maji,mbegu ya mpunga ni ya kwao unauziwa kiasi kidogo si kama madukani nje,mbolea ni za ruzuku,ukihitaji utapewa kwa gharama nafuu)Ukipita pembeni shauri yako.Labda uonane na mwenye shamba mtajuana wenyewe lakini kupitia mtu mwingine utalia.

Mashamba mengine unakodi kwa watu,na kama utakodi la hivo,hakikisha mnaandikishana kwenye uongozi wa kijiji.Tofauti na hapo,utajua mwenyewe.
Ukihitaji maelezo zaidi,nambie,kama kukusindikiza ntakusindikiza,ugjaramie usafiri.Ila,kama hujajipanga kulima,usiharibu hela yako.
Wow asante sana huwa nafikiria kulima vitunguu
 
Nimependa namna ulivyowasilisha ujumbe wako. Haina kubembelezana wala kupakana mafuta kinafki, safi sana

Asante;napenda nachokihitaji iwe hivo kwa mwenzangu.Unayemsaidia leo ndo barozi wako kesho,na unapoamua kuwa tapeli,basi unaiangamiza familia yako na wanaojutegemea.Sipendi
 
Wow asante sana huwa nafikiria kulima vitunguu

Jiandae,na ukalime kweli(usimamie)sio uambiwe tuma hela kesho tunavuna njoo na gari huku mara ya mwisho watu kufika shamba ni siku ya kumpanda.
 
Vipi mihogo na mahindi, vinalimwa hapo hapo ?
 
Kilimo ni kizuri lakini mwanzo wake ni sawa na kutambaa Kisha kusimama na halafu kutembea. Huwezi kuanza na faida. ASANTE KWA UJUMBE MZURI
 
Jiandae,na ukalime kweli(usimamie)sio uambiwe tuma hela kesho tunavuna njoo na gari huku mara ya mwisho watu kufika shamba ni siku ya kumpanda.
Katika swala la kuwekeza huwa sinaga kutumana ili hasara ikitokea nisiwe na wa kumlaumu na faida ikipatikana nijisifie mwenyewe,
 
Mihogo sijaona,mahindi yapo yanapandwa kwa wingi.Kwa sababu ya uhakika wa maji,mbogamboga na matunda ndo vinavyolimwa kwa wingi,na mpunga
Hayo mahindi yanalimwa msimu wa mwezi gani au wanafanya umwagiliaji ?
 
Pale kilimo si cha msimu ndugu.Unajua mito inavyotema,maji yanakaa ardhini mda mrefu,na ardhi ya huku inatwamisha maji,hivyo bado unyevunyevu wa kuosha upo,na pia kwa vile maji yapo,ukihitaji unamwagilia.Kiwe tu kilimo ambacho unahitaji mazao mengi,kwenye eneo dogo.Maji na dawa na mbolea ni mhimu
 
Unaweza kutoa direction labda tunaweza kwenda kutembea huko siku moja mkuu. Unapanda magari ya wapi ?
 
Haya sasa vijana changamkieni fursa sio kulalama mtaani hakuna ajira, kajiajiri Ruvu
 
Habari zenu.
Nimewahi kuuliza swali kuhusu mashamba ya kulima Ruvu,nikabahatika kupata maelezo,nikaenda na nimeanza.
Lakini,uzi ulioniongoza nimeutafuta sijauona,ila nimetumia muongozo niliopewa.
Ruvu kwa kweli kama una nia ya kulima ni pazuri,maji yapo ya uhakika,mito ni miwili,Ruvu na Msuya.
Pamoja na hayo lakini kuna changamoto kubwa mbili:
1.Usimamizi unahitajika na kama umeamua,hamia au tafuta mtu wako wa karibu.Wajanja huku ni wengi,tena bora niwaite wahuni.Ukituma hela kwamba kazi utafanyiwa utaishia kulia tu.
2.Upatikanaji wa mashamba:
+255 658 899 195.Kuna mtu siku za nyuma alitoa hii number kwamba atafutwe mwenye nayo,atawapa maelezo.Hakika aliyepost hii number wanashilikiana asilimia mia.
Jamani,mtu kama yule unawezaje kuomba watu,walioacha familia zao,wampelekee pesa,awatapeli?
Nawasihi sana,nimeona mengi.
Kama unataka shamba huko,kuna sehemu mbili.Kuna kilimo cha mpunga,kinafanywa na shirika,huyu anawapeleka watu na kuwauzia mashamba ya watu,mwisho wa siku mnaishia kugombana na hela unapoteza.Anauza shamba lililopandwa mpunga kwa laki 5,na lisiti atakupa.Za kughusho,mwisho wa siku unakumbana na mwenye shamba sasa.Kama umeamua kulima huko,nenda ofisini,gharama za ofisi ni 442,000(pesa ya kukodi shamba kwa mwaka,unalimiwa,unapewa maji,mbegu ya mpunga ni ya kwao unauziwa kiasi kidogo si kama madukani nje,mbolea ni za ruzuku,ukihitaji utapewa kwa gharama nafuu)Ukipita pembeni shauri yako.Labda uonane na mwenye shamba mtajuana wenyewe lakini kupitia mtu mwingine utalia.

Mashamba mengine unakodi kwa watu,na kama utakodi la hivo,hakikisha mnaandikishana kwenye uongozi wa kijiji.Tofauti na hapo,utajua mwenyewe.
Ukihitaji maelezo zaidi,nambie,kama kukusindikiza ntakusindikiza,ugharamie usafiri.Ila,kama hujajipanga kulima,usiharibu hela yako.
Ahsante mkuu. Namba ya ofisi?
 
Back
Top Bottom