Mkuu CityHunter1 asante kwa taarifa ila naomba ufafanuzi kidogo kwenye hiyo shs 442,000 ni kwa ajili ya kukodi ekari moja au hekta moja? Na ni kwa msimu au kwa mwaka? Na maximum ni ekari/ hekta ngapi kwa mtu mmoja?
100,000 ni malipo ya maji utakayokuwa unawekewa kwenye mpunga mpaka utakapovuna.
342,000; kuna pesa ya kujiunga na uanachama,kuna mshahara wa wanaowaita watermen(wana kazi ya kufungulia maji mashamba yote na kukagua ampapo hayafiki na kurekebisha,kama ni mifereji mikubwa).Kuna pesa ya vibarua wanaofyeka nyasi kwenye mifereji mikubwa ya chama na kuisafisha.
Humo kuna pesa ya kulipa wanaochabanga,na kupiga halow(kusawazisha udongo na kuuweka level ili maji yakiachiwa yawe level moja).
Kwa kule zinaitwa heka,lakini siyo size ya heka unayojua wewe,zinakuwa ni blocks.Kwa hiyo unakuwa na shamba la ukubwa wa 80*50m limekatwa vipande viwili ndo wanavyoviita heka.
Unakodi kwa mwaka mmoja tu.Ila,kama we ni mwanachama,mwaka ujao hutolila hiyo 442,000 tena.
Mashamba kama utachukuwa kama mwanachama,kila jina linapewa tu shamba moja.Kwa hiyo kama unajiweza,majina mengine utatumia ya familia yako,na kila jina utalilipia hiyo 442,000.
Vinginevyo ukimpata mwanachama muaminifu unaweza kulima kwa jina lake.
Kumbuka,ni kilimo cha umwagiliaji.Hivyo,ka eneo kadogo,mavuno mengi.Ukiweza kulihudumia,hilo unaweza kuvuna sawa na aliyelima acre 3 nje. Mhimu dawa,mbolea,usimamizi na maji