Mashairi ya Mrisho Mpoto-CCM mnayaelewa lakini?

cement

JF-Expert Member
May 5, 2012
581
218
Huyu jamaa ni bigwa wa kutumia kiswahili vizuri
Anaposema

Mjomba ww wapake wanja harafu wao wakupake pilipili na kwenye kombolela iwe zamu yako kuzinga ccm mnayaelewa haya maneno???

Au mtu mzima kutapika nyogo harafu akailamba watu wanamwangalia tu?

Maneno ya kitoto mtoto kumwambia mtoto mwenzie tunasema wanacheza!

Na maneno kitoto mtoto kumwambia mtu mzima tunasema anakua mfano baba ile ndege yangu baba hata kama hana baiskeli atasema ikitua nitakuletea!

Lakini maneno ya kitoto mtu mzima kumwambia mtu mzima mwenzie kuna uwalakini?anasema yeye safari imemshinda!tumedanganywa sana na serikali hii!

Maneno ya huyu jamaa ni mazito sana!

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
vp pale anaposema waliopo hatuwataki wanaotaka kuchukua nchi hatuwaamini....vp cdm mmeelewa hapo?
 
Lakini kwa nini alaumiwe dobi kutakasa kaniki hali tunajua rangi ya nguo.....
Ndugu zangu ukiona paka kakubali kulala chali, anza kuomba ruhusa kazini.......
 
mtoto akikuomba kiatu unakaa baada ya miaka 5 halafu unarudi kumuuliza ulitaka kiatu cha saizi gani
 
wanaokupigia makofi ni wanafiki na wazandiki tu, ili kujua ukweli yarekodi usikilize ukiwa umetulia. Pia anaposema wameshka vitambaa vya rangi moja na vyote vimeloa
 
Utawaulizaje watu fimbo zanini wakati ulisema kuna nyoka?
CCM mnamuelewa na propaganda yenu ya UDINI? Alafu mnamshangaa PONDA?
 
Mrisho Mpoto nyimbo zake zinahitaji utulie na uwe mchambuzi mzuri wa mambo! Kuna wimbo wa siku za karibuni unaitwa CHOCHEENI KUNI,jamaa anaweza!
"Pepo haina sifa bila kuwepo jehanamu"
 
Duh Mrisho mpoto ni noma kwa kweli jamaa anajua sanaaaaa mashairi yake ni noma kwa kweli!
 
Mjoooomba tulifundishwa na mwl kuwa ukisikia kengele na azana ujue..........
Na ukisikia M4C ujue.........!
 
Mrisho Mpoto nyimbo zake zinahitaji utulie na uwe mchambuzi mzuri wa mambo! Kuna wimbo wa siku za karibuni unaitwa CHOCHEENI KUNI,jamaa anaweza!
"Pepo haina sifa bila kuwepo jehanamu"

That's Nietzsche in Swahili, or Zoroastrian duality. Glad to see classic philosophical concepts translated. Sio kila siku I got this, I got that, Im the best sharobaro etc.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom