Mashairi ya kimapokeo na ya kisasa

Mashairi ya kimapokeo na ya kisasa

Akademician

Senior Member
Joined
May 20, 2015
Posts
143
Reaction score
36
Habari zenu wakuu.

Pamoja na kuhamasika na kazi za waandishi mbalimbali kama vile Kezilahabi, Shaaban Robert, Mohamed Said, Andanenga, Penina Mhando, Haji Gora, Charles Mloka, Theobald Mvungi n.k,
Mimi ni kijana niliyebahatika kuwa na kipaji na mapenzi ya dhati katika uandishi wa kazi za kifasihi, hasa utanzu wa Ushairi

Mapenzi yangu kwenye uwanja wa fasihi ni makubwa sana kiasi kwamba siwezi kupoteza siku bila kuandika beti kadhaa (za kimapokeo &/ za kisasa/mamboleo) zenye maudhui yenye tija kubwa kwa jamii yetu,
zikiangazia nyanja mbalimbali za maisha.

Hii imepelekea watu wengi wa karibu wanaonizunguka kuona kuwa ni hasara kubwa kwa kazi za fasihi zilizoandikwa kwa umahiri kuishia kimyani,
Na hivyo wakanishauri nifanye haya, au kimoja kati ya haya yafuatayo;

1. Nifanye jitihada za kuonana na kampuni za uchapishaji wanisaidie kutoa diwani(kitabu cha mashairi kwa makubaliano fulani.
Au
2. Nionane na wamiliki/wahariri wa magazeti nizungumze nao vema ili nipate fursa ya kuchapisha shairi 1 lenye beti 8 au 10 gazetini kila wiki, kwa makubaliano fulani pia.

Nimeona ni mawazo mazuri kuyafanyia kazi,
Ila kutokana na kutokuwa na 'channel' pana ya masuala hayo,
Nimeona nilifikishe hili hapa JF labda naweza kupata msaada wa mawazo, mwongozo au mchango wa aina yoyote uwezao kusaidia ufanikishaji wa hili.

Nipo Dar,

Ahsante.
 
hebu kwanza kajifunze kuandika vizuri kwa kuzingatia KANUNI ZA UANDISHI halafu njoo hapa tutakushauri
 
Mkuu upo sahihi kabisa kuwa kuna makosa ya kiuandishi yalijitokeza,
Ila sio makusudi.
Kuna kitufe nilikosea kubonyeza kikaharibu mpangilio wa maandishi.

Hata hivyo nimekwisha hariri vema,
Na sasa ujumbe unasomeka vizuri bila makosa ya kiuandishi.
 
Mkuu kama kweli unajihahakisha uko vizuri, hebu jaribu kufuatilia huko uliko waulize watu unaodhani wanaweza kukushauri mahala sahihi pa kwenda, uende unaweza pata msaada, pia jaribu kuwauliza walimu wa fasihi advance, labda wanaweza kukupa msaada. Pia subiri wadau wanaojua vizuri watakuja kukushauri.

Nilitaka nikwambie uende BAKITA lakini nadhani itakua ni hatua ya juu ya sana, tafuta walimu wa fasihi uwaulize. Inaweza kuwa kuwa ndio njia yako ya kutoka. Kila lakheri
 
NiPM na unipatie mawasiliano yako,nami naandika mashairi.
Tuwasiliane.
 
Back
Top Bottom