Mashabiki waliamsha baada ya mwamuzi wa kati kutoa penati dakika ya 90+2

Doctor Stranger

JF-Expert Member
Oct 31, 2020
4,202
6,143
Mashabiki wa klabu ya Unisport FC de Bafang walivamia uwanja na kuwapiga waamuzi baada ya mwamuzi wa kati kutoa penati dakika ya 90+2 dhidi ya Victoria United katika mchezo wa mzunguko wa 13 wa Ligi ya Daraja la Pili nchini Cameroon 🇨🇲 maarufu kama MTN Elite Two.

Hadi kufika dakika hiyo Unisport walikuwa wanaongoza 1-0.

Katika hatua nyingine Golikipa wa timu ya Victoria United Idris Youssouf ametuma ujumbe wa sauti kwenye kundi la WhatsApp la timu hiyo akithibitisha kuwa ni kweli wananunua mechi.

"Kama Rais wao hanunui mechi hilo ni tatizo, sisi tunanunua na tutapanda daraja, kama wao hawataki kuwapa marefa pesa wakae watulie, sisi tunafanya hivyo kwasababu pesa tunayo" alisema Golikipa huyo ambaye amedumu Victoria kwa miaka miwili.

Victoria United hivi karibuni walinunua basi lao jipya kwaajili ya kurahisisha safari zao.

Kabla ya mchezo huo msimamo wa Ligi ulikuwa hivi:
1️⃣ Victoria Utd (Pts 22) Mechi 12
2️⃣ Bafoussam (Pts 21) Mechi 13
3⃣ Unisport FC de Bafang (Pts 21) Mechi 12

Chanzo: KICK422. COM

#sokaonlineupdates
 
🤣🤣
1676446357421.jpg
1676446353013.jpg
 
Nilishtuka, nikadhani mashabiki wa yanga wamezinduka kuhusu uhuni wa engineer hersi na gisiemu..
 
Botafogo walitaka kusepa na kibendera aliyejifanya haoni Offside na hapo keshagongwa mitama kama minne ndani ya muda mfupi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom