DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,470
Mashabiki wengi wa Yanga hata hawa ambao siku za hivi karibuni wamekengeuka na kupinga kitendo cha klabu yao kujiingiza katika shughuli za siasa, wanaamini kabisa kwamba klabu yao ina historia, mashirikiano na ukaribu na chama tawala pamoja na serikali.
Yanga ni kitengo cha michezo ndani ya UVCCM. Mashabiki wa Yanga toka wakiwa wadogo wanajifunza na wanafundishwa kuwa Yanga ni "klabu dola" na hauwezi kuwabadilisha hawa watu wakishakuwa wakubwa. Wanaona, wanafundishwa na kuamini Simba ni vibaraka wa nje. Huu siyo utani, ni jambo lililo ndani ya fikra zao.
Labda itokee mtu apate maarifa binafsi ya kutosha na afahamu ni jinsi gani klabu yake inatumika katika shughuli za siasa na apate upeo wa kufahamu ni jinsi gani maendeleo ya uchumi na kijamii yanakwamishwa na mahusiano hayo ndiyo hapo anaweza kufanya maamuzi mengine ila bila hivyo ndiyo unakutana na hawa wasiojitambua wanatamka "No Reform No Election" na "Free Lissu" halafu ni Yanga lia lia.
Anyway, nimekutana na hii video hapo juu. Msikilize huyu binti. Anachokisema ni mentality iliyopo ndani ya kila mwanayanga, wakubali au wakatae. Na wameikata hii video hapo mwisho, najua amesema mengi zaidi ambayo yapo vichwani mwa wanayanga wengi.
Kuitenganisha Yanga na CCM siyo jambo lililo rahisi kama mnavyodhani. Hata wasipoonyesha wazi, mafungamano haya yana mizizi mirefu sana. Magufuli alitambua nguvu ya Yanga ndani ya CCM ndiyo maana aliipiga pini na alijua inaweza kutumika na maadui wake ndani ya chama kumtikisa.