Mashabiki wa Q Chief Tukutane hapa.....

Lavit

JF-Expert Member
May 16, 2011
13,110
26,997
Naamini huyu jamaa ana mashabiki wa kutosha katika rika zote, sijajua mafanikio yake kiuchumi ila katika muziki namuona ni moja ya wasanii waliofanikiwa sana katika tungo zao pamoja na muziki wao kiujumla...

Kifupi Q Chief nilianza kumsikia katika wimbo wa Mzimuni Family ulioitwa Mpiga Debe, baada ya hapo ikawa kama milango imefunguka kwa Q...hapo akaja na vibao kama Aseme, Si Ulinikataa na Zamani ambavyo vilitikisa kila kona ya nchi hii...

Q Chief aliendelea kutoa vibao vingi vikali kama My Boo, Uhali gani, Natawala, Cheers, Naogopa, weiper, Umaskini Wangu, Ninachokipata, Sexy, Zaidi Jana, Mariam, Naijutia Nafsi, Mwana Mnyonge, Nisengenyeni na nyingine nyingi...

Kwenye Collabo pia hakuwa nyuma, kaimba na mastar kibao mapka underground, Q chief kaweza kufanya kazi na Ay na Fa(Asubuhi), Wako wapi(Dataz), Msinitenge (Prof J), Sintobadilika (Mike T), Jay Moe (Kama unataka Demu),Vaa Tutoke ya Black Rhyno....

Hivi karibuni Q chilla amekuja Kibao matata kabisa cha Chuma Kisamvu achilia mbali Mau na Delilah zilizotoka kabla yake...

Hakika hiki ni kipaji kikubwa kabisa katika Bongo Fleva...
Ebu tujumuike hapa kumpa support, pia tukumbushane jinsi tulivyoguswa na vibao vyake...
Kwa kifupi mimi nimewahi guswa na nyimbo hizi..

*Aseme
*Mwana Mnyonge
*Umaskini Wangu na
*Ungeniumiza...

Je kwako nyimbo bora za Q chief ni zipi..zipi zilikugusa zaidi??

"NIKILALA NAOTAA,NAOTA KAMA UNANIITA,ILA NAFSI INASITA MPENZI,IPO SIKU NITAITIKA."
Huyu ndo alikuwa Q chief naemkubali.Huyu wa siku hizi sijui ni nduguye au kopi yake
 
Kati ya nyimbo alizoimba huu ndio wimbo mbovu hasa!! Jamaa aliimba nyimbo zenye akili Sana Kwa sauti yake halisi. Tatizo kaanza kuimba Kwa kubana pua!! Nyimbo hazina akili!!, rithimu au biti sio za mdundo Kama Rege Fulani ivi. Sauti yake Ya kukwaluza ndio ilitushika Mbaya. Ni sawa na 20% kimuziki. Q Chief aludie mziki wake hakuna wa kumshika Africa mashariki, na zaidi apate meneja alie vizuli.
 
Apunguze kingereza kwenye nyimbo zake za Sasa!
Wabongo Wengi hiyo Lugha ni tatizo

Ila bado yupo vizuri sana sema aache pombe
 
Jamaa anajua ila tatizo ni kwamba apunguze vingereza vingi kwenye nyimbo zake maana kipindi yuko kwenye peak hakuwa anawaimbia vingereza watanzania. Na pia apunguze mashauzi kama ya mademu akiwa anaongea full mashauzi utadhani Miss Tanzania na tone za kuongea Kiswahili kama vile kadondoka kutoka kwa Trump.
Mwisho kabisa apunguze kujiona yuko juu na kutokuwa na heshima maana kwa sasa kila mtu ambaye angependa kummanage Q-Chief anaogopa kuanzia WCB na wengine. Unakumbuka alivyoondoka kwa QS Mahonda na kumtusi na kumsema vibaya akasahau kuwa alikuwa kapotea walau yeye alimrudisha kwenye game kwa kumgharamia akatengeneza nyimbo na video S.A akamlipia collable na patoranking na kumpa sehemu ya kukaa. Mwisho wa siku akamtusi na kumdharirisha atleast angeondoka bila kumsema vibaya jamaa.
 
Naamini huyu jamaa ana mashabiki wa kutosha katika rika zote, sijajua mafanikio yake kiuchumi ila katika muziki namuona ni moja ya wasanii waliofanikiwa sana katika tungo zao pamoja na muziki wao kiujumla...

Kifupi Q Chief nilianza kumsikia katika wimbo wa Mzimuni Family ulioitwa Mpiga Debe, baada ya hapo ikawa kama milango imefunguka kwa Q...hapo akaja na vibao kama Aseme, Si Ulinikataa na Zamani ambavyo vilitikisa kila kona ya nchi hii...

Q Chief aliendelea kutoa vibao vingi vikali kama My Boo, Uhali gani, Natawala, Cheers, Naogopa, weiper, Umaskini Wangu, Ninachokipata, Sexy, Zaidi Jana, Mariam, Naijutia Nafsi, Mwana Mnyonge, Nisengenyeni na nyingine nyingi...

Kwenye Collabo pia hakuwa nyuma, kaimba na mastar kibao mapka underground, Q chief kaweza kufanya kazi na Ay na Fa(Asubuhi), Wako wapi(Dataz), Msinitenge (Prof J), Sintobadilika (Mike T), Jay Moe (Kama unataka Demu),Vaa Tutoke ya Black Rhyno....

Hivi karibuni Q chilla amekuja Kibao matata kabisa cha Chuma Kisamvu achilia mbali Mau na Delilah zilizotoka kabla yake...

Hakika hiki ni kipaji kikubwa kabisa katika Bongo Fleva...
Ebu tujumuike hapa kumpa support, pia tukumbushane jinsi tulivyoguswa na vibao vyake...
Kwa kifupi mimi nimewahi guswa na nyimbo hizi..

*Aseme
*Mwana Mnyonge
*Umaskini Wangu na
*Ungeniumiza...

Je kwako nyimbo bora za Q chief ni zipi..zipi zilikugusa zaidi??

Mbona huu haujauweka kwenye list?

Aache Kula Unga Aisee.
 
Back
Top Bottom