Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

MASHA ANA ufalme wa kumtosha, hahitaji JK... pia uelewe JK ana less than 50% influence kwenye serikali iliyo madarakani

wewe unaangalia juu, kazi zote zipo local government....

komaa-komaa ujue maisha,

inatia aibu sana mtu kama muhingo, a well seasoned journalist anakubali kuwa DC, what a waste!!

tubadilike, we can sustain our families bila hata political appointments

Zamani nilifikiri UDC ni cheo kikubwa cha maana, lakini leo nimeona unavyogawiwa bila kupima kiwango cha uwezo wa mtu na wa kujuana, sasa tutegemee nini kwa maendeleo ya nchi? Masha analijua sana hili kutokana na uwepo wake katika wizara nyeti, alivyoongea amejitahidi sana kuweka ukweli hadharani, wachache wenye kufanya alichofanya Masha wakati wangali bado kwenye minyororo ya CCM.
 
Zamani nilifikiri UDC ni cheo kikubwa cha maana, lakini leo nimeona unavyogawiwa bila kupima kiwango cha uwezo wa mtu na wa kujuana, sasa tutegemee nini kwa maendeleo ya nchi? Masha analijua sana hili kutokana na uwepo wake katika wizara nyeti, alivyoongea amejitahidi sana kuweka ukweli hadharani, wachache wenye kufanya alichofanya Masha wakati wangali bado kwenye minyororo ya CCM.
kilikua cheo cha maana kwasbabu ya siasa za chama kimoja

u-DC ni sawa na u-CD tu kisiasa.... hasa kutokana na matendo ya baadhi ya ma DC kudhani kazi yao ni kusimamia interest za chama badala ya interest za wilaya
 
Anamtafutia Nchi ili amteuwe kuwa BALOZI.

Nafasi aliyo nayo kiuchumi Masha kuingia kwenye siasa nadhani ni kuteremka. Anatengeneza pesa nzuri inayomfanya aishi kwa utulivu na amani bila hewalahewala kwa mtu. Hizi pesa za siasa hazinogi ndugu yangu. Una mwona Mengi hata mkuu wa nchi anamvulia kofia kumwalika waongozane kwenye makongamano ya biashara za kimataifa? Ujasirimali umemwinua na hana haja ya CCM.
 
Kama ni kweli kwamba vijana hawaipendi ccm kwa sababu hawakufundishwa historia ya Tanzania, ni afadhali kwa faida ya ccm hawakufundishwa, maana wangefundishwa wangeshaipindua hii serikali ya kihuni zamani sana. Ametolea mfano kenya, kwamba walifundishwa historia. Ndiyo maana kanu haipo madarakani, ni kwa sababu waliijua historia ya kenya.
 
Masha hana jipya kama ni maadili au kuwa na histori mbona wewe ulikuwa kwenye system hushauli hata kudhubutu kufanya? acha siasa za maji machafu hapa
 
Mkuu huyu alikuwa ndani ya Serikali kwa miaka mitano hakuliona hili la elimu yetu kuwa duni na kulizungumza hadharani wakati akiwa Waziri mpaka yuko nje ya Serikali ndio analiona? Kwa maoni yangu namuona ni msanii tu ambaye sasa amekosa ulaji ndio anaziona kasoro ndani ya Serikali.

huko ni kujikosha, kwa na yeye pia si fisadi tu, ndiye aliyeanzisha vitambulisho vya kitaifa, leseni mpya n.k
 
Kama ni kweli kwamba vijana hawaipendi ccm kwa sababu hawakufundishwa historia ya Tanzania, ni afadhali kwa faida ya ccm hawakufundishwa, maana wangefundishwa wangeshaipindua hii serikali ya kihuni zamani sana. Ametolea mfano kenya, kwamba walifundishwa historia. Ndiyo maana kanu haipo madarakani, ni kwa sababu waliijua historia ya kenya.

Umeona Chadema wamewaelimisha vijana na sasa wameamka na kuikimbia CCM?
 
Hajaulizwa kitendo alichokifanya cha kuondoka na baadhi ya vitu ktk ofisi ya mbunge akidai ni vyake?
 
ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Nyamagana, Lawrence Masha, amesema vijana wengi nchini hawataki CCM kwa sababu hawaoni kilichofanyika tangu kilipoanzishwa.

Masha alisema wananchi wanahitaji kuona mabadiliko na kwamba, hali hiyo inatokana na kutosoma vizuri historia ya Tanzania. Akizungumza kwenye kipindi cha Mkasi kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha EATV, alisema hatua ya kutopenda chama hicho imetokana na vijana kutosoma historia.
“Vijana wengi hawaipendi CCM, wengi wanataka mabadiliko… siyo kosa lao, hawakufundishwa. Kuna wakati nilikuwa Chuo Kikuu cha St Augustine Mwanza nazungumza, kijana mmoja akasimama akasema nyie, wazee ndiyo wanarudisha nyuma nchi. Nikaangalia nyuma nikajiuliza huyo mzee yuko wapi... Nikagundua kumbe na mimi ambaye nilikuwa najiona kijana kniko kwenye kundi la wazee” alisema Masha.

Masha ambaye ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe nchini, Dk Fortunatus Masha, alisema vijana wengi wanapenda mabadiliko ya haraka jambo ambalo hawalioni ndani ya CCM na kuongeza kuwa, hali hiyo inasababishwa na kutokuwapo kwa mkakati wa kuwafundisha historia ya mafanikio ya Serikali na viongozi wake. “Leo hii ukienda Nairobi ukitaka kitabu kuhusu maisha ya Raila Odinga utaipata, ukitaka historia ya (Daniel) Moi .. Kenyatta utaipata. Mimi kijana wangu ana miaka 17 anasoma South Africa (Afrika Kusini) alikuja hapa anaomba kitabu ili nijue Tanzania imetoka wapi,..Hakuna,” alisema Masha na kuongeza:

“Sasa kama mtoto ambaye anataka kujua nchi yake, anakosa hata pa kuipata, nchi yake ikoje, marais waliotawala, tumefikaje hapa? Lazima waseme tumekuwa maskini kwa sababu ya chama ambacho kiko madarakani.”

Kuhusu kushindwa kwake ubunge mwaka 2010, Masha alisema amekubali kushindwa na anaendelea na kazi zake nyingine. “Ukiingia kwenye uchaguzi ni sawa tu na kuingia kwenye mpira, kuna kushinda na kushindwa, kikubwa ukishashindwa kubali matokeo endelea na maisha. Tatizo watu wengi na hasa wanasiasa wenzangu hawana kazi nyingine za kufanya,” alisema Masha.

Alipinga madai kuwa kipindi chake cha ubunge na uwaziri hakufanya lolote katika jimbo lake, badala yake alitoa mifano ya kazi alizofanya na kwamba, wanaoeneza hayo ni watu wenye fitina. “Sidhani kama ni kweli, unajua kwenye siasa kuna fitina imani yangu ni kwamba kazi yangu nilifanya na kazi yangu ya uwaziri niliifanya. Of course (bila shaka) kutokana na mfumo tulionao, mwenzako lazima akumalize ili akushinde,” alisema Masha na kuongeza:

“Leo hii tunapoongelea Nyamagana kuna chuo cha polisi kimejengwa, kuna Sekondari ya Mkolani imejengwa nje ya bajeti ya Serikali… ni kutoka kwa wafadhili na marafiki, there’s a lot of works (kuna kazi nyingi).” Alisema alikuwa akisomesha watoto 236 kwa mshahara wake wa ubunge na kwamba, tangu alipoingia bungeni mshahara wake ulikuwa ukipelekwa jimboni kusaidia wasiokuwa na uwezo.

“Leo hii ndiyo watu wanakumbuka, ndiyo nasema leo hii hata mke wangu na watoto wangu nao wafurahi kidogo kile ninachokipata, nipeleke kwenye maendeleo ya familia,” alisema. Hata hivyo, Masha alisema kazi za siasa zinahitaji uvumilivu hivyo alijitahidi kuvumilia changamoto hizo kipindi chote cha uongozi wake.


Mwananchi
 
huyu alikuwa akishinda mwanza jioni anarudi kula bata dsm
aliwahi kusema mwanza hapafai kulala
 
hana nyimbo huyo. Vitabu kibao vinaielezea tanzania. Asituzingue maana inaonesha hata maduka ya vitabu hayajui yaliko. Haoni hata haya kusema hakuna vitabu. Ny am bafu zake
 
Binafsi nimependa uchambuzi wake, kuna mambo mazuri ya msingi ambayo ameongelea hapa, ukweli unajieleza. Hata hapa JF utakuta watu hawana nafasi ya kujadili mada, ila kutoa maneno mawili matatu ya mipasho tu. Unaweza kugundua kitu kinakosekana kwetu ambacho ni elimu. Elimu haiji peke yake ila kwa kujishughulisha kuujua ulimwengu na malimwengu. Kuna njia nyingi siku hizi, badala ya hizi network kutumika ku-browse elimu sisi tunatumia kwa ajili ya maridhio ya urafiki mitandaoni na ku-browse pics za mahaba ndo elimu wengi tunayoipenda, je itatufikisha wapi kama si kutudumaza kiakili?

Kwa hili mkuu uko sahihi,kuna tatizo la kujadili hoja na hata definition ya hoja yenyewe. Tunabakiza kuangalia spelling za mleta hoja na vitu vidogo vidogo nje ya hoja yenyewe. Huenda ni uwezo mdogo tulionao ki elimu kudadavua mambo haya kwa upana wake.
Lazima tujisahihishe ili tupige hatua stahili.
 
It is not correct to say, as Masha does, that there is a complete dearth of books about contemporary Tanzania. It is my ardent hope that Masha will find time to read the following three books, in the order given:
1. The Making of Tanganyika, Judith Listowel, London, Chattto & Widus, 1965.

2. From Goatherd to Governor: The Autobiography of Edwin Mtei, Edwin Mtei, Mkuki and Nyota
Publishers, 2009.
3. Tanzania in Transition From Nyerere to Mkapa, Kjeli Havnevik and Aika Isinika (eds.), Mkuki and
Nyota Publishers, 2010.

 
. Mimi kijana wangu ana miaka 17 anasoma South Africa (Afrika Kusini) alikuja hapa anaomba kitabu ili nijue Tanzania imetoka wapi,..Hakuna,” alisema Masha na kuongeza:
.

Sasa hizo shule za kata mliwajengea kina nani kama nyie watoto wenu wanasoma nje?
 
hakuwa na mfano mzuri zaidi ya huo qa mtoto wake anayesoma south africa? juzi nimeona habari itv wanafunzi wanasomea kwenye zizi la ng'ombe bagamoyo, afu anatuletea usharobaro wake hapa. kama anataka mtoto wake aijue tz amrudishe asomee hapa tz ataijua tu wala hatahitaji kitabu.

sijui kwa nini hawa watu huwa hawajui waongee nini wanapokuwa kwenye public... anyways i dont wanna spoil my day,
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom