Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jun 13, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Masha: Vijana wengi hawaipendi CCM


  ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Nyamagana, Lawrence Masha, amesema vijana wengi nchini hawataki CCM kwa sababu hawaoni kilichofanyika tangu kilipoanzishwa.

  Masha alisema wananchi wanahitaji kuona mabadiliko na kwamba, hali hiyo inatokana na kutosoma vizuri historia ya Tanzania. Akizungumza kwenye kipindi cha Mkasi kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha EATV, alisema hatua ya kutopenda chama hicho imetokana na vijana kutosoma historia.

  "Vijana wengi hawaipendi CCM, wengi wanataka mabadiliko… siyo kosa lao, hawakufundishwa. Kuna wakati nilikuwa Chuo Kikuu cha St Augustine Mwanza nazungumza, kijana mmoja akasimama akasema nyie, wazee ndiyo wanarudisha nyuma nchi. Nikaangalia nyuma nikajiuliza huyo mzee yuko wapi... Nikagundua kumbe na mimi ambaye nilikuwa najiona kijana kniko kwenye kundi la wazee" alisema Masha.

  Masha ambaye ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe nchini, Dk Fortunatus Masha, alisema vijana wengi wanapenda mabadiliko ya haraka jambo ambalo hawalioni ndani ya CCM na kuongeza kuwa, hali hiyo inasababishwa na kutokuwapo kwa mkakati wa kuwafundisha historia ya mafanikio ya Serikali na viongozi wake.

  "Leo hii ukienda Nairobi ukitaka kitabu kuhusu maisha ya Raila Odinga utaipata, ukitaka historia ya (Daniel) Moi .. Kenyatta utaipata. Mimi kijana wangu ana miaka 17 anasoma South Africa (Afrika Kusini) alikuja hapa anaomba kitabu ili ajue Tanzania imetoka wapi,..Hakuna," alisema Masha na kuongeza:

  "Sasa kama mtoto ambaye anataka kujua nchi yake, anakosa hata pa kuipata, nchi yake ikoje, marais waliotawala, tumefikaje hapa? Lazima waseme tumekuwa maskini kwa sababu ya chama ambacho kiko madarakani."

  Kuhusu kushindwa kwake ubunge mwaka 2010, Masha alisema amekubali kushindwa na anaendelea na kazi zake nyingine.

  "Ukiingia kwenye uchaguzi ni sawa tu na kuingia kwenye mpira, kuna kushinda na kushindwa, kikubwa ukishashindwa kubali matokeo endelea na maisha. Tatizo watu wengi na hasa wanasiasa wenzangu hawana kazi nyingine za kufanya," alisema Masha.

  Alipinga madai kuwa kipindi chake cha ubunge na uwaziri hakufanya lolote katika jimbo lake, badala yake alitoa mifano ya kazi alizofanya na kwamba, wanaoeneza hayo ni watu wenye fitina.

  "Sidhani kama ni kweli, unajua kwenye siasa kuna fitina imani yangu ni kwamba kazi yangu nilifanya na kazi yangu ya uwaziri niliifanya. Of course (bila shaka) kutokana na mfumo tulionao, mwenzako lazima akumalize ili akushinde," alisema Masha na kuongeza:

  "Leo hii tunapoongelea Nyamagana kuna chuo cha polisi kimejengwa, kuna Sekondari ya Mkolani imejengwa nje ya bajeti ya Serikali… ni kutoka kwa wafadhili na marafiki, there's a lot of works (kuna kazi nyingi)."

  Alisema alikuwa akisomesha watoto 236 kwa mshahara wake wa ubunge na kwamba, tangu alipoingia bungeni mshahara wake ulikuwa ukipelekwa jimboni kusaidia wasiokuwa na uwezo.

  "Leo hii ndiyo watu wanakumbuka, ndiyo nasema leo hii hata mke wangu na watoto wangu nao wafurahi kidogo kile ninachokipata, nipeleke kwenye maendeleo ya familia," alisema.

  Hata hivyo, Masha alisema kazi za siasa zinahitaji uvumilivu hivyo alijitahidi kuvumilia changamoto hizo kipindi chote cha uongozi wake.
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nimekubaliana na majibu ya Masha pamoja na mchepuo wa maisha yake baada ya kubwagwa ubunge. Kimsingi siasa ni mchezo mchafu, ukiamua kuuendeleza unaweza kushtukia hata umekufilisi kama kama hukufanikiwa nafasi uliyogombea. Na walioshinda ndio maana wanafanya jitihada kubwa na kutumia njia haramu kurudisha gharama walizotumia kupata nafasi hizo.

  Kama nafasi inaruhusu bora kuamua kuendesha shughuli binafsi zinazokupatia lishe na kuyaendesha maisha kwa utulivu kuliko haya ya nafasi za kisiasa za kunyoosheana vidole kila kukicha bila kikomo.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,786
  Trophy Points: 280

  Duh! Kwa hiyo huyu anadhani vijana wa Kitanzania wakifundishwa na kisha kupatiwa vitabu vya kusoma kuhusu historia ya nchi yetu na tumefikaje hapa tulipo basi vijana wataipenda magamba!!! Kazi kweli kweli!!!!
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Jun 13, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  There's a lot of works?
   
 5. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  hapana, umemiss his point

  anazungumia knowledge... wakiwa na knowledge watafanya better decisions
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,786
  Trophy Points: 280
  Hiyo knowledge itatoka wapi ikiwa shule zenyewe midabwado, walimu midabwado, vifaa mbali mbali mashuleni midabwado na pamoja na kuanguka elimu yetu bado Serikali inapunguza bajeti ya Elimu!!!..
   
 7. samilakadunda

  samilakadunda JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 1,700
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Dah mashaaaah kama unataka kujivua gamba vile unakaribishwa waliko vijana wenzio,au ww ulisoma vitabu vya nyerere,mwinyi, mkapa na huu ni upepo tu utapita? Na huyo mwanao kasha shitukia ubabaisha wenu na ulafi wa magamba.
   
 8. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  i think that was his point....

  kusema tu vitabu haimaanish vitabu, bali elimu kwa ujumla
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Jun 13, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mimi nadhani tatizo si kutojua historia kwa upande wa vijana wetu. Tatizo ambalo Masha hakulizungumzia ni kwamba CCM iliyopigania uhuru na kumtetea kabwela, siyo CCM hii ya leo ambayo imetamalaki kwa rushwa, matabaka ya walio nacho na kutojali raia wake.
   
 10. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #10
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,841
  Likes Received: 2,772
  Trophy Points: 280
  Hivi hicho kidhungu amesema Masha au wandishi wetu makanjanja? Eti works! Shame!
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,786
  Trophy Points: 280
  Mkuu huyu alikuwa ndani ya Serikali kwa miaka mitano hakuliona hili la elimu yetu kuwa duni na kulizungumza hadharani wakati akiwa Waziri mpaka yuko nje ya Serikali ndio analiona? Kwa maoni yangu namuona ni msanii tu ambaye sasa amekosa ulaji ndio anaziona kasoro ndani ya Serikali.
   
 12. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #12
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  yawezekana aliona na alizungumza, ila nijuavyo mimi si kila wanachozungumza kinaenda media
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hayo ndiyo anayosema Masha, kuna kitu cha msingi ambacho vijana wamekosa. Elimu imekuwa ya mabadiliko badiliko kila mwaka, hakuna mtaala wa kudumu, kila waziri akija na yake. Sijui tuna vitabu gani vya kiada ambavyo mwanafunzi anaweza kutumia na vikarithishwa kwa wanaomfuata, kwani kesho yake mtaala utabadilika.

  Uandishi wa mambo ya historia ya nchi yetu umetupiga kikumbo, ni Nyerere aliyeweza kuishi kwa kuandika mengi ya kutufunza. Marais wengi huandika mengi lakini viongozi wetu wa siku hizi wamekuwa wazururaji, sijui watapata lini nafasi ya kuandika ya kutufunza wananchi kutokana na uzoefu wao wa uongozi.
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Jun 13, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thanks mkuu
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Binafsi nimependa uchambuzi wake, kuna mambo mazuri ya msingi ambayo ameongelea hapa, ukweli unajieleza. Hata hapa JF utakuta watu hawana nafasi ya kujadili mada, ila kutoa maneno mawili matatu ya mipasho tu. Unaweza kugundua kitu kinakosekana kwetu ambacho ni elimu. Elimu haiji peke yake ila kwa kujishughulisha kuujua ulimwengu na malimwengu. Kuna njia nyingi siku hizi, badala ya hizi network kutumika ku-browse elimu sisi tunatumia kwa ajili ya maridhio ya urafiki mitandaoni na ku-browse pics za mahaba ndo elimu wengi tunayoipenda, je itatufikisha wapi kama si kutudumaza kiakili?
   
 16. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #16
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hivi JK kamsahau kabisa Masha ktk ufalme wake?
   
 17. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #17
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Jamani wengi wetu kidhungu ni lugha ya tatu kutoka mother tongue, national language na kisha hii ya kiairishi taabu tu, tunajiuma ulimi. Tuache tu.
   
 18. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #18
  Jun 13, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Candid Scope,
  Unataka kuniambia kuwa tungekuwa na elimu bora kuliko tuliyo nayo hivi sasa vijana wetu wangeshabikia CCM? I think there is more to it than simply blaming it on education. CCM imewapoteza vijana kwa sababu kimegeuka kuwa chama cha kulaghai. Angalia ahadi alizozitoa Kikwete katika uchaguzi wa 2010. Hivi kweli unaamini Kigoma itageuzwa kuwa Dubai wakati wa utawala wa Kikwete, ambao amebakiwa na miaka mitatu tu?
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  MASHA ANA ufalme wa kumtosha, hahitaji JK... pia uelewe JK ana less than 50% influence kwenye serikali iliyo madarakani

  wewe unaangalia juu, kazi zote zipo local government....

  komaa-komaa ujue maisha,

  inatia aibu sana mtu kama muhingo, a well seasoned journalist anakubali kuwa DC, what a waste!!

  tubadilike, we can sustain our families bila hata political appointments
   
 20. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #20
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160


  Thanks Jasusi, elimu ni pana na wala tuizungumzayo hatumaanishi ya vitabuni tu na wewe unafahamu fika juu ya niongeleacho. Mfano makamanda wa Chadema wanavyozunguka nchi nzima kutoa somo la uraia kwa wananchi na jinsi wananchi wanavyowaelewa na kuitikia kiasi cha kubadili kabisa wimbi la mtazamo wa kisiasa za mageuzi nchini mwetu. Hii ni moja wapo ya elimu ambayo wananchi wameikosa na CCM imefanya kila jitihada kuwanyima kwa ajili ya wachache wabaki kuwa katika nafasi wanazotaka bila kunyoshewa vidole na wananchi.

  Serikali haijawa na mfumo wa kuwafunda watu namna ya kutoa elimu ya kujitegemea kama enzi za awamu ya kwanza ambapo vijijini kulikuwa na msukumo wa kujitegemea na watu baada ya kuhitimu shule walikuwa na mwelekeo wa uzalishaji vijijini. Leo elimu hiyo imekosekana, vijana toka vijijini baada ya kuhitimu shule wanakimbilia mijini. Ukiona vijana walivyojaa mijini huwezi kuamini wanakula nini na wanaajiriwa wapi na ndio maana wako waitikiaji wazuri sana kwenye mihadhara kwa kuwa hawana cha kufanya. Nenda vijiji wamebaki vijana wachache wana ambao nao wengi wanatafuta nafasi ya kwenda mijini na vijiji vimebaki makazi ya wazee tu.

  Amini nisemayo kwani nimefanya utafiti na kushuhudia hali ilivyo vijijni na mijini. Shule za kata zimesaidia kuwashika walio mashuleni kubaki huko, na wakishahitimu wanatimkia mijini, ni dalili ya kukosa somo la elimu ya kujitegemea ambalo nio muhimu kwa mazingira ya kujiajiri vijijini ingawa nako kuna changamoto nyingi zinazotokana na kukosekana kwa miundo mbinu mbalimbali na kukosekana kwa utility.
   
Loading...