Masha adai wawekezaji wa madini waligoma

Na Frederick Katulanda, Mwanza


NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha amesema wawekezaji katika sekta ya madini nchini waligoma kubadilisha mikataba yao kwa madia ni makubaliano hali yaliyokuwa yamekwa kwa mujibu wa Sheria ya Madini.


Masha alisema hayo, wakati akijibu hoja mbalimbali zilizoibuka katika kongamamo la kuadhimisha Siku ya Wananfunzi Duniani katiika Chuo Kikuu cha Matakatifu Augustino (SAUT).


Alisema kosa lilifanyika awali wakati wa kuandaasheria ambapo sheria hiyo iliwekwa kwa lengo la kuwavutia wawekezaji wa sekta ya madini.


Masha alisema sheria iliyokosewa katika kukaribisha wawekezaji hao wa madini ni kuwekwa kwa sheria iliyoruhusu mwekezaji kusamehewa kulipa kodi kiasi cha

asilimia 15 ya mtaji wake (15 % addition capital allowance).


?Mimi nikiwa Naibu Waziri wa Madini na Nishati nilikuwa miongoni mwa

wajumbe waTume ya kwanza ya kupitia sheria hiyo, tulikwenda kwa wawekezaji lakini waligoma wakidai kuwa tulishaingia mikataba nao na kutisha kwamba

watatutangaza kuwa sisi ni wababaishaji na vigeugeu,? alieleza.


Alieleza kuwa tatizo la madini katika nchi kutoinufaisha nchi yetu lipo katika sheria

na wala siyo viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuongeza kuwa sheria hiyo ndiyo inayosababisha nchi hii kutonufaika na madini na kudai kuwa kuibadili ni jambo gumu kutokana na mikataba kufungwa toka zamani.


Alifahamisha kuwa katika kamati yao ambayo iliundwa na rais walikuwa wakipitia mikataba ya migodi yote ipatayo sita na kwamba katika hiyo mgodi uliokubali ni wa Barrick na wengine waligoma na kudai kuwa wataishitaki nchi yetu.


Masha alisema katika kamati yao walifanikiwa kuwashawishi baadhi ya wawekezaji na kisha kuufuta sheria hiyo kwa mgodi wa Barrick na kudai kuwa migodi hiyo pia ilikubali kulipa kodi na kwamba kamati iliyoundwa sasa ni muendelezo wa kamati yao ambayo ilivunjika baada ya rais kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.


Alisema kwa sasa watu wamekuwa wakipiga kelele kutokana na hisia na siyo hali halisi, hivyo kuwataka wasomi wa chuo hicho kutopenda kuzungumzia mambo bila kufanya utafiti.

Source: Mwananchi Newspaper
Jf embu fanyeni kupitia upya ushauri Wa wana jf miaka kumi Leo iliyopita 2007-2017 na maana maakala ya mapitio ya Jf kuhusu shauri la sheria za madini Tanzania .
 
Back
Top Bottom