Masha adai wawekezaji wa madini waligoma

Zee la shamba

Member
Oct 17, 2007
55
3
Na Frederick Katulanda, Mwanza

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha amesema wawekezaji katika sekta ya madini nchini waligoma kubadilisha mikataba yao kwa madia ni makubaliano hali yaliyokuwa yamekwa kwa mujibu wa Sheria ya Madini.

Masha alisema hayo, wakati akijibu hoja mbalimbali zilizoibuka katika kongamamo la kuadhimisha Siku ya Wananfunzi Duniani katiika Chuo Kikuu cha Matakatifu Augustino (SAUT).

Alisema kosa lilifanyika awali wakati wa kuandaasheria ambapo sheria hiyo iliwekwa kwa lengo la kuwavutia wawekezaji wa sekta ya madini.

Masha alisema sheria iliyokosewa katika kukaribisha wawekezaji hao wa madini ni kuwekwa kwa sheria iliyoruhusu mwekezaji kusamehewa kulipa kodi kiasi cha

asilimia 15 ya mtaji wake (15 % addition capital allowance).

?Mimi nikiwa Naibu Waziri wa Madini na Nishati nilikuwa miongoni mwa

wajumbe waTume ya kwanza ya kupitia sheria hiyo, tulikwenda kwa wawekezaji lakini waligoma wakidai kuwa tulishaingia mikataba nao na kutisha kwamba

watatutangaza kuwa sisi ni wababaishaji na vigeugeu,? alieleza.

Alieleza kuwa tatizo la madini katika nchi kutoinufaisha nchi yetu lipo katika sheria

na wala siyo viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuongeza kuwa sheria hiyo ndiyo inayosababisha nchi hii kutonufaika na madini na kudai kuwa kuibadili ni jambo gumu kutokana na mikataba kufungwa toka zamani.

Alifahamisha kuwa katika kamati yao ambayo iliundwa na rais walikuwa wakipitia mikataba ya migodi yote ipatayo sita na kwamba katika hiyo mgodi uliokubali ni wa Barrick na wengine waligoma na kudai kuwa wataishitaki nchi yetu.

Masha alisema katika kamati yao walifanikiwa kuwashawishi baadhi ya wawekezaji na kisha kuufuta sheria hiyo kwa mgodi wa Barrick na kudai kuwa migodi hiyo pia ilikubali kulipa kodi na kwamba kamati iliyoundwa sasa ni muendelezo wa kamati yao ambayo ilivunjika baada ya rais kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.

Alisema kwa sasa watu wamekuwa wakipiga kelele kutokana na hisia na siyo hali halisi, hivyo kuwataka wasomi wa chuo hicho kutopenda kuzungumzia mambo bila kufanya utafiti.

Source: Mwananchi Newspaper
 
Nilisha sema hili tangu mwanzo, contract is a "promise", Tanzania tuna option chache sana hapa, moja labda twende WTO tuka fail complains ambazo huchukua miezi kabla hazija jadiliwa, na haigeretii kushinda. Option ya pili ni kunationalize hiyo migodi, madhara yake ni wawekezaji wote watakimbia, and Tanzania will be another Zimbabwe. So, only thing tulicho nacho ni kujadiliana na hao wawekezaji.
 
Mimi nikiwa Naibu Waziri wa Madini na Nishati nilikuwa miongoni mwa wajumbe waTume ya kwanza ya kupitia sheria hiyo, tulikwenda kwa wawekezaji lakini waligoma wakidai kuwa tulishaingia mikataba nao na kutisha kwamba watatutangaza kuwa sisi ni wababaishaji na vigeugeu,? alieleza.
Pamoja na kugomewa na kutishiwa bado mnaendelea tu kusaini mikataba mingine!!!! Shame, masha,shame kikwete, shame ccm

You need to be seious to issues like this
 
na wala siyo viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuongeza kuwa sheria hiyo ndiyo inayosababisha nchi hii kutonufaika na madini na kudai kuwa kuibadili ni jambo gumu kutokana na mikataba kufungwa toka zamani.
Na hii mipya??????????
tuna na mazero serikalini na hata bungeni
 
watatutangaza kuwa sisi ni wababaishaji na vigeugeu,? alieleza
Bora fedheha kuliko hasara!!!!!!!
Mtanzania bora afe lakini msionekane vigeugeu????
Tanzania hali hii tunakufa na tai yetu shingoni!
 
Masha alisema katika kamati yao walifanikiwa kuwashawishi baadhi ya wawekezaji na kisha kuufuta sheria hiyo kwa mgodi wa Barrick na kudai kuwa migodi hiyo pia ilikubali kulipa kodi na kwamba kamati iliyoundwa sasa ni muendelezo wa kamati yao ambayo ilivunjika baada ya rais kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.
Futeni hiyo sheria ktk sheria za madini si kufuta ktk mgodi mmja hapo ndiyo mianya ya ufisadi. Kwamba ukiongea vizuri tunakufutia!!!shame
Ukidabili balaza la mawaziri na kamati au tume zinavunjika? zimetumia pesa mingi halafu zinavunjika tu!!!
what kind of administration is this!!!!shame Kikwete Govt;
 
Watu wamepiga kelele wee, wamekaa kimya. leo kamati nyingine imeundwa, Masha anaibuka. hii ndiyo madhara ya kukalia kimya ripoti za tume. haya maelezo yangetolewa mapema watu tungejadili jinsi gani ya kujinasua kutoka kwenye sheria hiyo ambayo kimsingi iliandaliwa na viongozi hao hao na kupitishwa na wabunge walewale na wa chama kile kile.

Lack of vision, kwa viongozi wetu Kesho haipo na hata kwenye vitabu vyao neno kesho lilishaondolewa kitambo.
 
Angalau amesema yaliwasibu! Kuhusu kusaini hii mipya. Naibu waziri hana ubavu wa kuzuia, labda aamue kujiuzulu.
 
Bora fedheha kuliko hasara!!!!!!!
Mtanzania bora afe lakini msionekane vigeugeu????
Tanzania hali hii tunakufa na tai yetu shingoni!

..acha mchezo wewe na usifikiri wanavyosema kutanganzwa kuwa kigeu geu basi ni maneno tuu hapo,kisheria watatushinda na tutalipa pesa nyingi sana na ukumbuke budget 40% inatoka kwao,tukubali tuu ujinga wetu ndio umetuponza sasa sijui ilikuwa ni rushwa au akili ndogo tuu.
 
At last mtu kaongea ukweli kwa hiyo Kikwete aache kutuzuga na hivyo vijikamati eti vya kupitia mikataba,sasa wakae chini wabadilishe sheria za madini kwa mikataba ijayo ila iliyopita hakuna kitu wanaweza kufanya zaidi ya kuomba tuu
 
..acha mchezo wewe na usifikiri wanavyosema kutanganzwa kuwa kigeu geu basi ni maneno tuu hapo,kisheria watatushinda na tutalipa pesa nyingi sana na ukumbuke budget 40% inatoka kwao,tukubali tuu ujinga wetu ndio umetuponza sasa sijui ilikuwa ni rushwa au akili ndogo tuu.

Koba

Kweli umekata tamaa kiasi hiki??
 Koba

Kweli umekata tamaa kiasi hiki??

...Yebo yebo i wish ungekuwa Kikwete tuone ungefanya nini,nakuhakikishia muungwana anajua kila kitu na ninaamini hakula rushwa hapo na anajua hakuna kitu anachoweza kufanya hapo zaidi ya kuomba tuu ila hasemi tuu kwetu kwa sababu za kisiasa ila kama unataka kurudishwa stone age ya kina Castro,North Korea,Mugabe. wafukuze hao jamaa uone,bora sasa tuanze tuu kubadilisha sheria zilizopo ili tusiendelee kula deal mbovu maana naamini bado tuna vitu vingi sana ardhini
 
Mtanganyika,

Ni sahihi kabisa unachozungumza.................lakini unamuona huyu Masha anavyozungumza kwa dharau!!.......eti usizungumze/kulalamika bila kufanya utafiti wakati wao wenyewe wanaificha hiyo mikataba......wanaificha kwa nini?.............shame on Mwasha.
Pili kwa nini wanaendelea kusaini mikataba mingine kutumia sheria zinazotuumiza..............huyu nikiongozi mmojwapo walioridhika baada ya Azimio la Zanzibar kuwaruhusu kutufisadi.........and now he he does not care!!.....................yaani amezungumza kama ndio end of the world and we can't do nothing.

Mikataba ya madini na iwekwe wazi hata mitandaoni watu waione waijadili na kama kuna maoni watu watachangia.....................hivi sisi tuna wazimu gani jamani?.....shame on you Masha!.....................hiyo mikataba muliifanya sirii ndio maana mmetuingiza ktk TOTAL LOSS......kwa sababu ya choyo/ubinafsi...................lakini mngeweka maslahi ya Taifa mbele mngeandaa mikataba mapema na kuwashirikisha wananchi ili wachangie wajue haki zao na faida na hayo MADUDU wala yasingekuwepo na wala kusingekuwepo na hayo unayoita malalamiko bila utafiti...shame on you Masha! you better KEEP QUITE than to talk nonsense...wakati mmeuza rasilimali ya nchi kwa bei ya kutupa
 
Sasa kama anavyosema Masha ndivyo ilivyo, haya makamati ni ya nini? ni kuzuga sio? hawa wanafunzi wa siku hizi wamekuwa uncritical sana, yaani kulikuwa na maswali ya follow up mengi sana kutoka kwenye speech ya huyu bwana.
 
Kusimamisha kusaini mikataba mipya ili tubadili sheria ndiyo jambo linalotakiwa kufanyika. Hatuzuiliwi kutangaza kuwa tumesimamisha kusaini mikataba mipya mpaka itakapo tangazwa.

Hebu mulizeni huyo mwanasheria Masha kama hata kusimamisha kusaini mikataba mipya na kubadili sheria bado hao mwabwana mkubwa wao wana say ya aina yoyote???

Sisi ni nchi huru, kama kuna nchi au makampuni yatapinga kusimamisha kusaini mikataba na basi tuvunze uhusiano nao. Madini ni yetu Watanzania...vizazi vilivyopo na vitakavyo kuja hapo baadaye.

Hatuna haraka kwani sasa hivi tunapata faida gani kutoka kwenye madini???

Ni kiasi gani cha kujitegemea kuandaa bajeti yetu kumebadirika kabla na baada ya kuwakaribisha hawa wawekezaji wa sekta ya madini.
 
huyu masha mcheza madili na disko anawadanganya kampuni yake ya uwakili ilipewa pesa za rushwa leo akaambiwa atolewe maana watu wameshtuka hawezi kuwabana wazungu, wote waliotoka marekani ndio wezi wetu, Hosea pccb, balali na hao kina masha.
 
Futeni hiyo sheria ktk sheria za madini si kufuta ktk mgodi mmja hapo ndiyo mianya ya ufisadi. Kwamba ukiongea vizuri tunakufutia!!!shame
Ukidabili balaza la mawaziri na kamati au tume zinavunjika? zimetumia pesa mingi halafu zinavunjika tu!!!
what kind of administration is this!!!!shame Kikwete Govt;
Ulichangia Jana kama Leo vile baada ya miaka mingi tukiendelea kuibiwa
 
Watu wamepiga kelele wee, wamekaa kimya. leo kamati nyingine imeundwa, Masha anaibuka. hii ndiyo madhara ya kukalia kimya ripoti za tume. haya maelezo yangetolewa mapema watu tungejadili jinsi gani ya kujinasua kutoka kwenye sheria hiyo ambayo kimsingi iliandaliwa na viongozi hao hao na kupitishwa na wabunge walewale na wa chama kile kile.

Lack of vision, kwa viongozi wetu Kesho haipo na hata kwenye vitabu vyao neno kesho lilishaondolewa kitambo.
Nakupongeza Leo miaka kumi baadae 2017 laiti ccm wangesikia
 
Back
Top Bottom