Masanja Umechemsha bro!!

Nawashangaa sana wasanii wa Tanzania. Hivi huwa wanasahau kwamba wanapenda na watu wa aina tofauti tofauti? Wangejua nafasi yao kwenye jamii hata wasingesimama kwenye majukwaa ya siasa wangehamasisha tu watu kupiga kura!
 
Kolabo la wasanii wa bongo fleva kumpongeza Mh Rais, limetiwa doa na maneno ya Masanja Mkandamizaji.

1.Eti JPM ndiye Rais pekee duniani anayemuamini Mungu 100%. Hivi ana takwimu gani na Imani za Ma rais? Toka lini kumwamini Mungu imekuwa sifa ya urais hapa TZ? Huyo Mwl. Nyerere anayemsema yeye alisema hata asiyekuwa muumini tutamuapisha kuwa Rais. Hapa Masanja umechemka.

2. Kwamba kwa miaka mitano Mh. Rais passport yake haijachafuliwa na mihuri ya Ulaya kwa maana kwamba hajasafiri toka achaguliwe kuwa rais. Hii Masanja ni aibu kuisema mbele ya wageni hasa Marais walioziwakilisha nchi zao, maana kusafiri kwa rais sio kosa wala kutokusafiri sio jambo la kujivuna mbele ya wageni. Ni kama vile unawapiga vijembe, mimi hilo halijanibariki kabisa.

3. Kwamba hakuna mtu aliyevaa barakoa nalo hukuhitaji kulisema kabisa wakati mbele ya wageni maana hao wageni wamevaa barakoa.

Kibaya zaidi umejisahau kwamba huo sio mkutano wa campaign. Eti unawapiga vijembe wanaopinga mataokeo na kutaka uchaguzi urudiwe na unatumia neno baya sana eti urudiwe huu ni" Uchaguzi wa baba yako"? Mbona Mh. Magufuli katumia hekima wala hakutaka kufika huko?

Wewe kama msanii unatakiwa ujue hadhira unayozungumza nayo, uwe na busara na kiasi. Kujipendekeza kwako kumetia doa wimbo wa wasananii wenzako.
"mimi sio bro wako acha kujipendekeza" massanja mkandamizaji
 
Inasikitisha sana yaan pamoja na wizi wote ule halafu mtu anasema eti chaguo la Mungu, Mungu gani anataka watu waibe. Yaani mimi nikimkuta magu peponi mimi natoka kwa dhulma zake za wazi.
 
Kolabo la wasanii wa bongo fleva kumpongeza Mh Rais, limetiwa doa na maneno ya Masanja Mkandamizaji.

1.Eti JPM ndiye Rais pekee duniani anayemuamini Mungu 100%. Hivi ana takwimu gani na Imani za Ma rais? Toka lini kumwamini Mungu imekuwa sifa ya urais hapa TZ? Huyo Mwl. Nyerere anayemsema yeye alisema hata asiyekuwa muumini tutamuapisha kuwa Rais. Hapa Masanja umechemka.

2. Kwamba kwa miaka mitano Mh. Rais passport yake haijachafuliwa na mihuri ya Ulaya kwa maana kwamba hajasafiri toka achaguliwe kuwa rais. Hii Masanja ni aibu kuisema mbele ya wageni hasa Marais walioziwakilisha nchi zao, maana kusafiri kwa rais sio kosa wala kutokusafiri sio jambo la kujivuna mbele ya wageni. Ni kama vile unawapiga vijembe, mimi hilo halijanibariki kabisa.

3. Kwamba hakuna mtu aliyevaa barakoa nalo hukuhitaji kulisema kabisa wakati mbele ya wageni maana hao wageni wamevaa barakoa.

Kibaya zaidi umejisahau kwamba huo sio mkutano wa campaign. Eti unawapiga vijembe wanaopinga mataokeo na kutaka uchaguzi urudiwe na unatumia neno baya sana eti urudiwe huu ni" Uchaguzi wa baba yako"? Mbona Mh. Magufuli katumia hekima wala hakutaka kufika huko?

Wewe kama msanii unatakiwa ujue hadhira unayozungumza nayo, uwe na busara na kiasi. Kujipendekeza kwako kumetia doa wimbo wa wasananii wenzako.
Ametuaabisha afu usaniii wake wa kusifia kitu bila kujuaa hadhira ni kukusa maarifa ameabisha wasaniii wrote sijui walimwogopa wenzake wakati wa mazoezi au ni nini ni madudu Yale afu yanpromotiwa kwenye taarifaa ya habari...
 
Maendeleo yapi? Kwani maendeleo ni Hisani za CCM? au pesa za walipa kodi?
Maendeleo yanatokana na usimamizi bora wa Kodi za wananchi. Wenye uwezo wa kusimamia vema Kodi ya wananchi kwa Sasa ni CCM. Wengine mlikuwa mnapata pesa nyingi za ruzuku inayotokana na Kodi za wananchi wanyonge pia, lakini mmeshindwa kujenga hata ofisi ya chama. In other words Kodi yote ya wananchi iliyoelekezwa kwenu iliishia kwenye mifuko ya wachache.
 
79 Reactions
Reply
Back
Top Bottom