Masanja Umechemsha bro!!

crome20

JF-Expert Member
Feb 5, 2010
1,130
721
Kolabo la wasanii wa bongo fleva kumpongeza Mh Rais, limetiwa doa na maneno ya Masanja Mkandamizaji.

1.Eti JPM ndiye Rais pekee duniani anayemuamini Mungu 100%. Hivi ana takwimu gani na Imani za Ma rais? Toka lini kumwamini Mungu imekuwa sifa ya urais hapa TZ? Huyo Mwl. Nyerere anayemsema yeye alisema hata asiyekuwa muumini tutamuapisha kuwa Rais. Hapa Masanja umechemka.

2. Kwamba kwa miaka mitano Mh. Rais passport yake haijachafuliwa na mihuri ya Ulaya kwa maana kwamba hajasafiri toka achaguliwe kuwa rais. Hii Masanja ni aibu kuisema mbele ya wageni hasa Marais walioziwakilisha nchi zao, maana kusafiri kwa rais sio kosa wala kutokusafiri sio jambo la kujivuna mbele ya wageni. Ni kama vile unawapiga vijembe, mimi hilo halijanibariki kabisa.

3. Kwamba hakuna mtu aliyevaa barakoa nalo hukuhitaji kulisema kabisa wakati mbele ya wageni maana hao wageni wamevaa barakoa.

Kibaya zaidi umejisahau kwamba huo sio mkutano wa campaign. Eti unawapiga vijembe wanaopinga mataokeo na kutaka uchaguzi urudiwe na unatumia neno baya sana eti urudiwe huu ni" Uchaguzi wa baba yako"? Mbona Mh. Magufuli katumia hekima wala hakutaka kufika huko?

Wewe kama msanii unatakiwa ujue hadhira unayozungumza nayo, uwe na busara na kiasi. Kujipendekeza kwako kumetia doa wimbo wa wasananii wenzako.
 
Jamani Ajira Hakuna ndio Maana Wanasiasa walioko madarakani Wanasifiwa utadhani waliokuwepo hapo awali Hawakuwa Viongozi sahihi. Kila mtu ni Kufagilia tu ili aweze kukumbukwa maana mda si mrefu teuzi zitaanza. So ni Muda muafaka wa Kufagilia hata inaelekea kwa wateule Wengine kufuru Mungu.

Kwa mfano Msaka tonge mmoja ameonekana akinukuu Maandiko ya toka vitabu vitakatifu kwa Ushindi/Kushindwa kwa mtu fulani Kuwa Mungu ametenda. In short Kufanya vile si-afya kwa Binadamu na Mungu pia. Walioshinda Washerekee Kwa Staha vile vile Walioshindwa Wahuzunike kwa Staha.

Mungu Pamoja na Kwamba Wasahau Waafrika Wajifanyie watakavyo bila upendo Kuna siku Moja Anaweza Kugeuzia jicho lake na Wenye Kuonewa Wakaiona Nuru.
 
Back
Top Bottom