Omutwale
JF-Expert Member
- Feb 4, 2008
- 1,429
- 1,053
Tanzania ilikuwa inaelekea kuwa Kijana anayehisi kuwa na akili nyingi sana na maamuzi sahihi kuliko mtu au taasisi yoyote. Na mwenye kuhisi anaweza kujiongoza bila kufuata muongozo, sheria, kanuni wala taratibu husika za Jamii au Taasisi iliyomuweka kusimamia maslahi ya umma wake. Ghafla Kijana anaamka anajikuta ameishi maisha ya hisia na ndoto huku akichorwa unyayo mpaka kucha na mwenye akili. Waswahili wasema ukidhani nyangumi ndiye mbabe baharini unakosea. Papa hao wapo! Kwa wahaya huwa tunasema Ako Ogaya, Niko Kabutosa! (Tafsiri isiyo rasmi-Mwiko Udharauliwao, Ndiyo Huivisha Ugali).Kamanda Mwita Maranya yaani Prezoo akimsikia Kamanda Ben Saanane anatetemeka mwili mzima.