maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Fikiria umeacha kazi zako kwenda benki kutoa pesa kwa ajili ya kununua bidhaa za biashara yako.Huko benki unakuta wateja zaidi ya 100 huku wakiongezeka kadri muda unavyosonga.
Pamoja na kufurika wateja, dirishani kuna wahudumu wawili tu madirisha mengine matatu yakiwa yamefungwa tangu saa nne asubuhi mpaka saa nane hii, benki hii ya tawi la Kenyatta road haina kiti wala fomu za kukaa wateja, ni shida tupu hasa kwa wazee na akina mama wasioweza kusimama kwa muda mrefu.
Hivi kweli benki hizi hazina uwezo wa kuweka benchi au viti kwa ajili ya kukaa wateja wake? Kibaya zaidi hata wale wanaojaribu kuketi nje kwenye msingi wa benki baada ya kuchoka kusimama ndani wanatimliwa ili mradi ni shida tupu.
Ebu NMB Kenyatta road ongezeni ubunifu, kwanini mtu kuja kuchukua au kuweka pesa yake asimamishwe masaa manne bila huduma?