Kati ya madirisha sita ya teller wa NMB, manne TEMPORARILY CLOSED. Hii tabia inakera!

Doctor Ngariba

JF-Expert Member
Jan 28, 2020
480
765
Mambo vp wakuu,

NMB acheni ushamba na uzee

1. Hivi kwa dunia ya leo yenye furniture za bei chee mnashindwa hata kuweka utaratibu wa wateja wenu kuketi kwenye viti wakiwa wanasubiri huduma? Hebu jifunzeni kwa wenzenu na mtambue kuna baadhi ya wateja hawawezi kusimama kwa muda mrefu.

2. Huu utaratibu wenu wa "TEMPORARY CLOSED" kwa bank teller wenu ni fasheni au ndo kwa kuwa mna wateja wa kutosha?

Yaani madirisha 6 ya teller manne TEMPORARY CLOSED mawili tu yanafanya kazi? Na hili siyo mara moja labda tuseme dharura lakini ndio utaratibu wenu.

Acheni hizi tabia mnaboa mno!

Povu ruksa hata hivyo nitakuja kuongezea makandokando yenu mengine.
 
Huduma za kibenki zimehamia mtandaoni na mitaani.

Mawakala kila Kona, Unaweza kuhamisha miamala Kwenye simu,Unaweza kufanya direct transfer bank to bank mwenyewe.

Kwayo
Haina haja ya kua na utitiri wa TELLER ndani ya benki
 
Inawezekana unachozungumza ni kweli ila tambua kwamba hizo huduma kupitia simu ni wachache wanaozitumia.

Tembelea hizo bank ujionee mwenyewe zaidi ya hapo kama mtu anataka kudeposit 200m ataenda kwa wakala au ataenda bank?
 
Kwa NMB na benki nyingi

Mtu wa BULK (mzigo mkubwa) hawezi kaa foleni dirishani kwa teller

Wana mlango wao maalum huingia kuhudumiwa na kuna kiti unakaa unahudumiwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom