Mary Chatanda: Sheria kali itungwe kupambana na Ushoga, ikiwezekana wahasiwe

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye Sherehe ya Kilele cha Miaka Miwili ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita iliyoandaliwa na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT) katika Uwanja wa Uhuru Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam leo tarehe 19 Machi, 2023.



Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT), Mary Chatanda amesema wamefanya sherehe hii ili kumpongeza Rais kwa kuifanya nchi ipige hatua kubwa kiuchumi na kisiasa katika kipindi cha miaka 2 aliyoongoza.

Amemshukuru Hayati Magufuli kwa kuwaamini wanawake kwenye fursa nyingi za kisiasa pamoja na kumpa nafasi Rais Samia kuwa mgombea mwenza kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na 2020.

4801CF2D-B961-445A-9A8E-F7912B20511E.jpeg

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT), Mary Chatanda
Amemshukuru Rais kwa kuhudhuria kongamano la Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA), tendo linaloonesha kuwa siasa sio uadui. Pia, kukubali kuikwamua katiba mpya pamoja na kushiriki kwenye maridhiano ni mambo yanayoonesha uongozi mzuri wa Rais Samia.

Aidha, amesema UWT ipo kwenye hatua za mwisho za kuleta ripoti ya uchunguzi wa Ukatili wa kijinsia na watoto uliofanyika kwenye vituo vya polisi ili hatua kali zichukuliwe kwa wahusika. Pamoja na hilo, amesema mipango endelevu ya kukemea mapenzi ya jinsia moja (Ushoga) iwepo, sheria kali zitungwe kuwaadhibu wahusika kwa kuwa tabia hiyo ni kinyume cha utamaduni wa kitanzania.

“Hapa, Serikali ifanye marekebisho ya sheria hizi, na kuleta sheria kali kabisa Mhe. Rais, ikiwezekana hawa watu wakipatikana Wahasiwe, maana kuendelea kuwaacha hivihivi hawa, wataendelea kuliharibu taifa letu”

RAIS SAMIA
Amesema wakati wanapewa Madaraka alibezwa sana. Jambo hili lilimpa ujasiri wa kupuuza maneno hayo na kumpa nguvu na ujasiri wa kuchapa kazi na kusonga mbele. Hadi sasa, hakuna mradi uliosimama kutekelezwa.

F33B9374-1B07-46A3-9BB0-0F110D571B72.jpeg

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Amewashukuru BAWACHA kwa kuandaa kongamano kubwa na zuri kwenye kilele cha Siku ya Mwanamke Duniani. Amevitaka vyama vingine vya siasa kuiga mfano huo, ikiwezekana waandae pia miaka ijayo na yeye atakubali kushirikiana nao.

Rais amewapongeza Simba na Yanga kwa kutumia vizuri fursa aliyowapa ya kununua kila goli kwa Milioni 5. Kwa hesabu alizonazo, Simba wamelamba milioni 35 siku ya jana baada ya kuishinda Horoya FC. Amesema aliona utani Mtandaoni akimpigia Msigwa kuwa amwambie refa amalize mpira kuwa pesa haipo, sio kweli. “Wekeni mpira kwenye wavu, pesa bado zipo”

Amewataka wanawake kushiriki kikamilifu kwenye kupiganja fursa mbalimbali pasipo kusubiria wasemewe na wanaume.

Kuhusu Utawala bora na Demokrasia, Rais samia ameendelea kusisitiza kuwa yupo tayari kubadili Katiba ya Nchi kama ambavyo watu wengi wanataka. “Sifa ya mwanamke ni kujiamini, nami kama mwanamke wa CCM najiamini”. Yupo tayari kujadiliana na watu wa vyama vingine ili mambo yaende sawa.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye Sherehe ya Kilele cha Miaka Miwili ya Uongozi wa Serikali...
Ma Janamke ya CCM sio Mabunifu kabisa.

Sherehe ya Miaka Miwili ya Uongozi ndio nini sasa.

Yaani yameona hii ndio best Counterattack Kwa Kongamano la BAWACHA kwenye siku ya WANAWAKE Duniani
 
Ni ngumu kuamini mtu anaadhimisha cheo cha kurithi...

JK alisema, mtu huacha legacy muhula wa pili wa uongozi wake...

Safari bado ni ndefu...
Ma Wanawake ya ma CCM ndio yamemuandalia, Kwa Minajili ya Kuwajibu BAWACHA
Na yeye kakubali kaukubali huo Ujinga
 
Ma Janamke ya CCM sio Mabunifu kabisa.
Sherehe ya Miaka Miwili ya Uongozi ndio nini sasa.
Yaani yameona hii ndio best Counterattack Kwa Kongamano la BAWACHA kwenye siku ya WANAWAKE Duniani
Wanawake mna wivu Sana. Hapo shida ipo wapi UWT wakiandaa?
 
Ni ngumu kuamini mtu anaadhimisha cheo cha kurithi...

JK alisema, mtu huacha legacy muhula wa pili wa uongozi wake...

Safari bado ni ndefu...
Kwahiyo hata mtanguliz wake ilipaswa amalize muhula wa pili ili aache legacy? Kwann humu kuna wapambaniaji wa legacy yake?
 
Back
Top Bottom