Dream Queen
JF-Expert Member
- Nov 4, 2015
- 8,247
- 17,988
Wow!Marc anaugonjwa wa akili, unaitwa dissociative identity disorder. Ilikuwaje akawa nao,
*kutokana na kifo cha mdogo wake, mama yake marc akawa anamlaumu marc kwamba ndio sababu ya mdogo wake kufa. Mama'ke akapunguza mapenzi kwake na akawa anampiga piga kwa sababu ndogo sana.
*Kiafya/tiba zaidi, inafahamika kwamba ubongo wetu unaweza ku-process matukio tofauti sana, ikiwamo ikihitaji kukulinda wewe muhusika mwenyewe, unaweza kupoteza kumbukumbu muhimu sana, au ukatengeneza kumbukumbu mpya ambazo haujawahi kuzipitia kabisa, lakini ubongo wako ukakutaarifu kuwa hizo kumbukumbu mpya ndio uhalisia wenyewe.
*kuna scene inamuonesha marc alikimbilia chumbani baada ya mama yake kuanza kuwa mkali bila sababu, pale chumbani ukutani kulikuwa na jariba limebandikwa, jarida lile ukiliangalia lina picha ya mtu , the jina la huyo mtu ni "Steven Grant", mtu mashuhuri wa kuvumbua mambo ya kale, hasa hasa ya watu wa misri(yaani explorer).
Sasa, ubongo wa marc ukataka kumlinda "mtoto marc" kutokana na manyanyaso aliyokuwa anayapitia kutoka kwa mama yake, ndio hapo ukaunda kumbukumbu mtu (tuseme personality) mpya kabisa ambayo ndio hiyo "steven grant". Bila shaka huyo steven grant(wa kwenye jarida, alikuwa anatokea uingereza na kuongea lafudhi ya uingereza, wakati marc anaongea lafudhi ya kimarekani).
Pia sababu steven grant wa kwenye jarida ni "explorer" wa mambo ya zamani hasa hasa ya watu wa misri, ndo hiyo inamfanya alter ego ya marc spencer(yaani steven grant wa marc spencer) kuwa mjuaji sana wa mambo ya wamisri na hadithi zao za kale..
Kwa hivyo basi, sio kwamba yeye Marc Spencer ndo alimtengeneza Steven Grant kwa hiari yake, hapana, ni ubongo wake katika jitihada za kumuokoa kutokana na kile alichokuwa anapitia kutoka kwa mama yake wakati wa utoto.
Shukrani sana kwa kweli nimeelewa sasa nitazidi kuifatilia Moon Knight kwa karibu zaidi kama ninavyoifatilia Halo.